Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,962
- 70,576
Mimi nadhani ni sehemu za kuuza vitu vingi vingi kwa bei nafuu kiasi. Mimi naamini ukiamua kukomaa na minada unaweza toka na hela nzuri sana tu.
Nadhani kuna mikoa na mikoa yenye minada mizuri, nyie vijana ambao hamjui mfanye nini fanyeni biashara za vyombo vile vya bei ya chini.
Jana nilienda mnada mmoja nilikuwa nahitaji vyombo vingi vingi kwa mishe za hapa na pale! Vyombo vya plastic ni bei nafuu na watu wananunua mno mno! Muda niliokaa pale yule dogo aliuza sio chini ya laki 3, na nilikaa muda mfupi sana!
Mnaotaka kukuza mitaji au kutafta mitaji mizuri hii nayo msiidharau, wale mnaoona aibu ohh mimi nimemaliza chuo basi jichanganyeni mikoani kwenye minada mpige hela.
Imagine unanunua bakuli anakuuzia 500 na hata ukiomba kwa 300 hakatai!
Kama kawaida yangu nikaamua kumpeleleza dogo; aliniambia biashara yake anapata shilingi kwa shilingi, anauza hadi sufuria. Sasa sufuria ya 23,000 aliniuzia kwa 17,000, na amesema yeye hakatai hela na anauza kwa kusoma sura ya mtu. Mtaji kasema laki 5 unaweza kufanya maajabu.
Kwahyo ukiamua kuanza na 500k unaweza izalisha kwa mwezi ukawa na 900k (mfano) na mnadani ushuru huwa mdogo sana (nimewahi uza mitumba so naongelea reality hapa) ukikomaa mwaka mmoja nadhani utapata mtaji mzuri sana hata wa kuchukua vitenge katoro ukapeleka mikoani au ukauza pia mnadani, vitenge vinatoka sana sana minadani.
Nimekutana na wakaka/wamama wengi sana wanauza vitenge. Hawana frem anavijengea tu banda analala humo!
Na ukishazoea maisha ya mnadani unaweza usitoke ukapange frem maana hela ni nje nje na matumizi yako ni kiduchu
Mnadani hela ni unagusa tu!
NB: Jiandaeni kisaikolojia kupigwa jua!