Biashara ndogondogo zinaweza kukutoa mapema ukipeleka mnadani

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2018
Posts
34,962
Reaction score
70,576
Mimi nadhani ni sehemu za kuuza vitu vingi vingi kwa bei nafuu kiasi. Mimi naamini ukiamua kukomaa na minada unaweza toka na hela nzuri sana tu.

Nadhani kuna mikoa na mikoa yenye minada mizuri, nyie vijana ambao hamjui mfanye nini fanyeni biashara za vyombo vile vya bei ya chini.

Jana nilienda mnada mmoja nilikuwa nahitaji vyombo vingi vingi kwa mishe za hapa na pale! Vyombo vya plastic ni bei nafuu na watu wananunua mno mno! Muda niliokaa pale yule dogo aliuza sio chini ya laki 3, na nilikaa muda mfupi sana!

Mnaotaka kukuza mitaji au kutafta mitaji mizuri hii nayo msiidharau, wale mnaoona aibu ohh mimi nimemaliza chuo basi jichanganyeni mikoani kwenye minada mpige hela.

Imagine unanunua bakuli anakuuzia 500 na hata ukiomba kwa 300 hakatai!

Kama kawaida yangu nikaamua kumpeleleza dogo; aliniambia biashara yake anapata shilingi kwa shilingi, anauza hadi sufuria. Sasa sufuria ya 23,000 aliniuzia kwa 17,000, na amesema yeye hakatai hela na anauza kwa kusoma sura ya mtu. Mtaji kasema laki 5 unaweza kufanya maajabu.

Kwahyo ukiamua kuanza na 500k unaweza izalisha kwa mwezi ukawa na 900k (mfano) na mnadani ushuru huwa mdogo sana (nimewahi uza mitumba so naongelea reality hapa) ukikomaa mwaka mmoja nadhani utapata mtaji mzuri sana hata wa kuchukua vitenge katoro ukapeleka mikoani au ukauza pia mnadani, vitenge vinatoka sana sana minadani.

Nimekutana na wakaka/wamama wengi sana wanauza vitenge. Hawana frem anavijengea tu banda analala humo!

Na ukishazoea maisha ya mnadani unaweza usitoke ukapange frem maana hela ni nje nje na matumizi yako ni kiduchu
Mnadani hela ni unagusa tu!

NB: Jiandaeni kisaikolojia kupigwa jua!
 
Mnadani wanapiga sana hela...watu wengi sana....... Ilikuwa siku ya mnada jua kali zamani kidogo nikapelekaga vinywaji vyangu...... Vikaisha fyuu....kuna siku ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi


Bora umekiri hili!..ukiweka frem mjini ukauza nguo za mtumba ukiuza sana ni 50-90!@day..lakini mnadani nilikia naweza kutafta hela ya balo zima grade 1!mradi uweke watu wa kupiga debe!
Yes hata vimiminika vinaenda sana sana..km migodini tu. Hawajali ubaridi kbs mradi amekunywa!
 
Safi sana mkuu kwa kushare nasi ila kuna wabishi humu watakwambia tuletee business plan yako tuone kama kweli hiyo biashara inalipa!
 
Vijana wengi mkoani singida wamejikwamua kiuchumi kupitiaminada,
biashara kubwa simu na accessories zake
Batteries
Covers
Earphones
Chargers πŸ”Œ
SIM cards registration
Mpesa,tigopesa
Chakula
Urembo

Karibuni singida


Sasa kuna mtu anasema minadani kitu cha kuanzia 10000hawanunui...hv huna chaj au battery utaachaje kununua!mnadani mdomo wako tu kumshawishi mteja
 
manengelo kijana anakuja na elfu 20kununua cover ndogo ndogo za simu ananunua 10 sh 8000kwa zile simu zinazotrend,Battery 5 zenye quality ya chini 1000 ,memory cards 2quality ya chini 2500,jumla 5000
Cover atauza 3000/2500
Battery πŸ”‹ atauza 5000/4000
memory card 7000/5000
Kumbuka mtaji unakua A day anae sh ngapi a week?month?year?Unakuta anasajili na lines,mtaji ukiwa mkubwa anauza simu,mpesa Fursa zipo vijijini nyingi tuuu,Next year natafuta kijana awe anaenda mnadani kunifanyia kazi
Fursa ni nyingi hiyo ni kwa uchache tuu kuhusu phone πŸ“± and its accessories
 


Usemacho ni kweli tupu mkuu!ukiwa na malengo mtaji unaupata uutakao huko minadani!sema watu wanasubiri mitaji mikuubwa!eish!

All the best!
 


Usemacho ni kweli tupu mkuu!ukiwa na malengo mtaji unaupata uutakao huko minadani!sema watu wanasubiri mitaji mikuubwa!eish!

All the best!
 


Usemacho ni kweli tupu mkuu!ukiwa na malengo mtaji unaupata uutakao huko minadani!sema watu wanasubiri mitaji mikuubwa!eish!

All the best!
 


Usemacho ni kweli tupu mkuu!ukiwa na malengo mtaji unaupata uutakao huko minadani!sema watu wanasubiri mitaji mikuubwa!eish!

All the best!
 
Sasa kuna mtu anasema minadani kitu cha kuanzia 10000hawanunui...hv huna chaj au battery utaachaje kununua!mnadani mdomo wako tu kumshawishi mteja
mkuu ninaongea kwa experience,ninafanya biashara ya accessories na simu mjini,alfu 10 hawanunui?nasema ni uongo,ninauza tecno T528 jumla 45000 Zinauzika balaa vijana wanakuja nunua hapa unakuta mtu ananujua 10 3days amemaliza tena akienda mnadani anauza 60000/55000,na siyo aina moja ya simu,
Inote wametoa kasimu cha button na touch hpo hapo kana WhatsApp na kanatumia android Jumla 93000 kanauzika balaa wanunuzi wengi Vijana wanaofanya biashara mnadani
KUNA MADA ZA KUCHANGIA UKIWA NA INFORMATIONS ZILIZOKAMILIKA,
KARIBUNI SINGIDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…