Biashara ni uchawi

Biashara ni uchawi

Saad30

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2020
Posts
2,737
Reaction score
5,464
Mambo vipi wakuu.

Wewe umeweka mtaji wako wa milion 10 dukani kwako.
Jirani yako ameweka mtaji WA milion 30.

Unaamua kwenda Kwa mganga alafu mganga baada ya kukuchekia Ramli yako anakwambia njoo na jogoo mwekundu na Nazi Saba kwajili ya kufungua.

Mwenzio anaenda Kwa mganga anaambiwa inabidi utoe kafala la mnyama kondoo au mbuzi.Jamaa anaamua kutoa Ng'ombe kabisa.

Sasa wewe mganga wako wa Kuku na Nazi ataongea nini hapo kwenye Ng'ombe?

Unaamua kufungua biashara au kuuza kabisa na kuhama mtaa au mkoa.Jirani anakusanya wateja wote kwakwe na Maisha yanaendelea.

Uchawi unazidiana Nguvu Bana.
Biashara inataka Dua Sana.
 
Kazi kuabudu ushirikina tuuu na hao waganga wenu matapeli kuna mwenzako kule moshi katapeliwa 6M hlf akaachiwa trunker lina magazeti na biskuti kua pesa zake zimeongezeka

Ushirikina ni Ushetani jiingize upotee
Huyo alitaka zile pesa za kuongeza zile tunaita gangalee.
 
Ukisoma somo la historia na ukajua kwanini wazungu waligombania bara la afrika, na kwanini wazungu na warabu walikuja afrika kisha zile sababu ukaziweka katika mfumo wa maisha u sasa utapata jibu kuwa biashara haitaji uchawi bali ni kuangalia sehemu yenye uhitaji na kupeleka huduma uko si kukomalia mijini tu eneo moja tu
 
Ila lazima utafute mvuto, iwe ushirikina au dua Kwa Mwenye Enzi Mungu
 
Kazi kuabudu ushirikina tuuu na hao waganga wenu matapeli kuna mwenzako kule moshi katapeliwa 6M hlf akaachiwa trunker lina magazeti na biskuti kua pesa zake zimeongezeka

Ushirikina ni Ushetani jiingize upotee
Sijaona Mchaga mzembe kama yule
 
Mambo vipi wakuu.

Wewe umeweka mtaji wako wa milion 10 dukani kwako.
Jirani yako ameweka mtaji WA milion 30.

Unaamua kwenda Kwa mganga alafu mganga baada ya kukuchekia Ramli yako anakwambia njoo na jogoo mwekundu na Nazi Saba kwajili ya kufungua.

Mwenzio anaenda Kwa mganga anaambiwa inabidi utoe kafala la mnyama kondoo au mbuzi.Jamaa anaamua kutoa Ng'ombe kabisa.

Sasa wewe mganga wako wa Kuku na Nazi ataongea nini hapo kwenye Ng'ombe?

Unaamua kufungua biashara au kuuza kabisa na kuhama mtaa au mkoa.Jirani anakusanya wateja wote kwakwe na Maisha yanaendelea.

Uchawi unazidiana Nguvu Bana.
Biashara inataka Dua Sana.
Physical business ni kweli ila sio digital
 
Wahindi walikuja tz kuuza rejareja mlipoyajua machimbo Sasa hivi wamefungua viwanda nyie mnaparuana kwenye kuvuta wateja...mitaji midogo mnagawana na waganga...wajinga wameenda kukimbiza wachaga kko...wachaga wapo mikoani...wa mikoani wakiamka wapo kwenye viwanda...waganga shida sana ..
 
Back
Top Bottom