Biashara nyingi zina promotion package nzuri, lakini ukija kwenye uhalisia ni mbingu na ardhi

Biashara nyingi zina promotion package nzuri, lakini ukija kwenye uhalisia ni mbingu na ardhi

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Kuna biashara ukiona matangazo yake unaweza kujenga picha kubwa sana kichwani. Video ni nzuri, picha ni kali, maelezo yanavutia na kila kitu kinaonekana cha kiwango cha juu. Mwisho wa siku unafanya maamuzi ya haraka kwa sababu umeamini kila kilichoonyeshwa kwenye tangazo.

Lakini ukifika dukani au unapofikia hatua ya kulipia ndipo unapokutana na uhalisia. Unagundua kile ulichokiona kwenye promotion na kile kilichopo mbele yako ni vitu viwili tofauti kabisa.

Utakuta supplier ametangaza Free Delivery kila mahali. Ukishalipia mzigo unaambiwa gari zote zimeharibika, dereva hayupo, leo kuna order nyingi sana au eneo ulilopo halifikiwi. Mwishowe unaambiwa kama una haraka, tafuta usafiri wako mwenyewe.

Kuna biashara hupost bidhaa nzuri sana mitandaoni, lakini ukifika dukani unaambiwa zimeisha. Ukikubali kusubiri unaambiwa stock inakuja wiki ijayo. Wakati mwingine wanakuambia hiyo ilikuwa sample tu ya kuvutia wateja, halafu wanakuonyesha bidhaa nyingine ambayo hata ubora wake haulingani na ulichokiona kwenye matangazo.

Kuna wafanyabiashara wengine hupost bidhaa ambazo hawana kabisa kwenye stock. Lengo ni kukuvutia ufanye malipo kwanza. Baada ya kulipa ndipo unaanza kuambiwa wanaenda kuagiza, wanasubiri mzigo ufike au kuna changamoto upande wa supplier. Wewe unakuwa tayari umeshafunga fedha zako.

Wapo wanaohakikisha huduma ya haraka sana kwenye matangazo. Lakini baada ya malipo, simu hazipokelewi, WhatsApp zinajibiwa baada ya masaa mengi au siku kadhaa, na kila ukifuatilia unaambiwa "subiri kidogo." Ghafla huduma ile nzuri uliyoiona kwenye promotion inabadilika kabisa.

Kuna matangazo yanaonyesha bidhaa zikiwa kwenye mazingira mazuri sana. Picha zimepigwa kwa camera nzuri, zimehaririwa vizuri na zimewekewa mwanga wa kuvutia. Ukiona kwa macho yako ndipo unatambua bidhaa halisi haifanani kabisa na ile iliyokuwa kwenye picha.

Usikubali kufanya maamuzi kwa sababu umeona offer imeandikwa "Leo tu", "Stock zinakwisha", "Bei ya mwisho" au "Watu ni wengi." Wakati mwingine hayo ni maneno ya kukushawishi ufanye maamuzi kabla hujafanya uchunguzi wa kutosha.

Kabla hujalipia bidhaa yoyote, uliza maswali ya msingi. Hakikisha bidhaa ipo kweli, bei ni ile ile iliyotangazwa, delivery ipo kama walivyoahidi na muda wa kuipata ni ule waliokueleza. Kama inawezekana, soma maoni ya wateja wengine waliowahi kununua hapo.

Promotion nzuri si tatizo. Kila biashara inahitaji kutangaza ili kuwafikia wateja. Tatizo linaanza pale ambapo matangazo yanatoa ahadi ambazo biashara haiwezi kuzitimiza. Hapo ndipo wateja hupoteza imani na biashara huanza kujijengea sifa mbaya.

Kama wewe ni mnunuaji, usifanye maamuzi kwa kutumia hisia zilizojengwa na matangazo pekee. Tumia muda kidogo kufanya uhakiki kabla ya kulipia. Dakika chache za kufanya uchunguzi zinaweza kukuokoa hasara kubwa, usumbufu na disappointment ambayo ingeepukika.

Kumbuka, biashara bora si ile yenye matangazo makubwa zaidi. Biashara bora ni ile ambayo uhalisia wake unalingana na ahadi zake.
 
Utakuta supplier ametangaza Free Delivery kila mahali. Ukishalipia mzigo unaambiwa gari zote zimeharibika, dereva hayupo, leo kuna order nyingi sana au eneo ulilopo halifikiwi. Mwishowe unaambiwa kama una haraka, tafuta usafiri wako mwenyewe.
Hahaha Mjini shule
 
Back
Top Bottom