Asilimia kubwa ya biashara nyingi halali huzalisha faida ya kati ya 17% had 20% kwa mauzo. Faida ya 50,000 kwa siku ni mauzo ya kati ya 250,000 hadi 300,000 kwa makadirio. Kwenye hiyo faida tunatoa hapo gharama za uendeshaji ambazo siyo rafiki sana kwa nchi yetu. Unajikuta gharama za uendeshaji ni nusu ya faida unayopata. Hivyo inakulazimu kuuza walau 500,000 hadi 600,000 ili ulaze 50,000.
Tukija kwenye mauzo hayo, ni mtaji kiasi gani? Hapa itategemea na aina ya biashara na location. Mfano: Biashara ya jiko la chips, chomachoma, chapati za kisasa mix supu inakulazimu uwe na mtaji usiopungua 4 milion.