Biashara unazoweza kuanzisha ukiwa na milioni moja ( Tsh 1,000,000)

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Leo sitakuwa na maneno mengi.
Ukiwa na milioni Moja hizi ni biashara unazoweza kuzifanya;

1. Fundi Nguo!
Chukua sherehani tatu za 250,000/= inayobakia tafuta Frem ya elfu 50. Nunua vifaa kisha anza kupiga kazi.
Cherehani zingine mbili tafuta mafundi, piga kazi.

2. Saluni ya kiume au ya kike.
Fungua saluni ya kawaida, vifaa havitazidi laki 7. kiti chongesha ni 200k. Vioo viwili laki 120k mashine mbili 100k Feni 50k, Sabufa 80k, kikabati 100k kisha lipia pango. Anza kazi.

3. Biashara ya maziwa!
Nunua Friza la kati 450k, nunua madumu au ndoo ya maziwa au gallon 150,000/= bajeti za umeme kwa mwezi weka 100,000/= bajeti za matangazo mtandaoni kwa mwezi weka 100,000/= piga pesa.

4. Social media management (SMM)
Nunua simu za kuanyia 500k, yenye kamera kali, Yenye storage nzuri, download app zitakzokusaidia katika SMM na content Creation.
Nunua vifaa vya kunasa sauti na kurekodi 250,000/= anza kupambana upige hela.

5. Biashara ya Delivery.
Nunua Pikipiki second hand(used) ya 800k to 900k nunua page mtandaoni yenye followers kuanzia 30k, kwa Tshs 50k, Tangaza Ad kwa kuanzia elfu 30k hiyo iliyobaki weka mafuta.
Piga pesa.

6. Biashara ya Sanaa ya maigizo au vipaji
Chukua simu 500k, hapo mtaani anzisha kikundi cha watu watatu mpaka saba cha kuigiza. Hakikisha unajua unalenga vijana na maudhui ya kitanzania. Nunua page FB, YouTube, Au Tiktok piga pesa.

7. Kwa mwalimu wa Martial Arts.
Hiyo milioni Moja, nenda pale Upanga au Mikocheni Azura. Omba short course ya kujifunza kupigana Martial arts. Ukihitimu omba Field kisha nawe kaanzishe mafunzo basic ya self defense. Piga pesa.

8. Kuwa Mwalimu wa kuogelea
Hiyo Milioni Moja, nenda pale Udsm, au kule Mikocheni, au Masaki, soma shortcourse ya kuogelea. Hakikisha muda mfupi ujue kuogelea huku unafuatilia mbinu zingine mtandaoni na AI.
Baada ya hapo anzisha Club ya kuogelea, andaa programu ya mafunzo ya uokozi katika maji, hizo ziwe sehemu ya plans zako, nenda Coco beach kule utapata wanafunzi wa kuwafundisha huku ukiwa na nidhamu na maadili. Ni vizuri ukiwa mtandaoni. Pesa Ipo.

09. Kuwa mwalimu, mkufunzi wa Mbwa au Farasi.
Ajira za ualimu wa watu ni chache lakini fursa ya ualimu wa wanyama kama Mbwa au farasi kwa Tanzania utajipigia pesa mpaka ulie.
Bahati nzuri hizi wateja wako wengi ni wakishua na wakueleweka

10. Kuwa Msusi na Makeup Artists hasa kwa Mwanaume.
Ingawaje kazi hii inaweza kukuletea shida kutokana na mitazamo hasi na dhana potofu za watanzania wengi ambao kimsingi hao hawatakuwa wateja wako.
Kwa upande wa Watoto wa kishua, Foreigners soko lako litakuwa Juu.

11. Kwa Mwanamke, Kuwa mtafsiri Filamu kama DJ Mark, Murphy na Afro.
Dunia ya sasa ni nyepesi sana. Usiwe Limited wakati dunia haiko limited.
Tanzania bado hatuna madj wa kukalimani movies. Hii kwa wanawake wenye kuona fursa kwao ni fursa na itakuwa historia kuwa miongoni mwao madj wa kwanza kwanza nchi wakike.
Hiyo milioni Moja, itumie kujifunza na kununua vifaa vya kurekodia.
Kisha piga pesa.

Ninaendelea, ngoja nikale kibulu kwanza.
Ukiwa na swali uliza, wali wenye stress zenu pia uwanja huu ni wenu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
13. Mwalimu wa Mtaani wa Muziki.
Utahitaji kujifunza muziki na ala za muziki. Kisha kazi kwako kuiingilia jamii kwa kuandaa matukio na kushirikisha jumuiya, taasisi, na matukio ya kijamii. Kisha piga pesa
 
Maisha sio marahisi kiasi hicho.

Maisha ni mindset yako tuu.
Kwa wengine maisha ni rahisi kwa wengine Magumu, wengine maisha hawana time nayo, wengine maisha hawayaelewi.
So ni suala la vile utakavyo iruhusu akili yako itafsiri maisha
 
Hamjambo!

Leo sitakuwa na maneno mengi.
Ukiwa na milioni Moja hizi ni biashara unazoweza kuzifanya;

1. Fundi Nguo!
Chukua sherehani tatu za 250,000/= inayobakia tafuta Frem ya elfu 50. Nunua vifaa kisha anza kupiga kazi.
Cherehani zingine mbili tafuta mafundi, piga kazi.

2. Saluni ya kiume au ya kike.
Fungua saluni ya kawaida, vifaa havitazidi laki 7. kiti chongesha ni 200k. Vioo viwili laki 120k mashine mbili 100k Feni 50k, Sabufa 80k, kikabati 100k kisha lipia pango. Anza kazi.

3. Biashara ya maziwa!
Nunua Friza la kati 450k, nunua madumu au ndoo ya maziwa au gallon 150,000/= bajeti za umeme kwa mwezi weka 100,000/= bajeti za matangazo mtandaoni kwa mwezi weka 100,000/= piga pesa.

4. Social media management (SMM)
Nunua simu za kuanyia 500k, yenye kamera kali, Yenye storage nzuri, download app zitakzokusaidia katika SMM na content Creation.
Nunua vifaa vya kunasa sauti na kurekodi 250,000/= anza kupambana upige hela.

5. Biashara ya Delivery.
Nunua Pikipiki second hand(used) ya 800k to 900k nunua page mtandaoni yenye followers kuanzia 30k, kwa Tshs 50k, Tangaza Ad kwa kuanzia elfu 30k hiyo iliyobaki weka mafuta.
Piga pesa.

6. Biashara ya Sanaa ya maigizo au vipaji
Chukua simu 500k, hapo mtaani anzisha kikundi cha watu watatu mpaka saba cha kuigiza. Hakikisha unajua unalenga vijana na maudhui ya kitanzania. Nunua page FB, YouTube, Au Tiktok piga pesa.

7. Kwa mwalimu wa Martial Arts.
Hiyo milioni Moja, nenda pale Upanga au Mikocheni Azura. Omba short course ya kujifunza kupigana Martial arts. Ukihitimu omba Field kisha nawe kaanzishe mafunzo basic ya self defense. Piga pesa.

8. Kuwa Mwalimu wa kuogelea
Hiyo Milioni Moja, nenda pale Udsm, au kule Mikocheni, au Masaki, soma shortcourse ya kuogelea. Hakikisha muda mfupi ujue kuogelea huku unafuatilia mbinu zingine mtandaoni na AI.
Baada ya hapo anzisha Club ya kuogelea, andaa programu ya mafunzo ya uokozi katika maji, hizo ziwe sehemu ya plans zako, nenda Coco beach kule utapata wanafunzi wa kuwafundisha huku ukiwa na nidhamu na maadili. Ni vizuri ukiwa mtandaoni. Pesa Ipo.

09. Kuwa mwalimu, mkufunzi wa Mbwa au Farasi.
Ajira za ualimu wa watu ni chache lakini fursa ya ualimu wa wanyama kama Mbwa au farasi kwa Tanzania utajipigia pesa mpaka ulie.
Bahati nzuri hizi wateja wako wengi ni wakishua na wakueleweka

10. Kuwa Msusi na Makeup Artists hasa kwa Mwanaume.
Ingawaje kazi hii inaweza kukuletea shida kutokana na mitazamo hasi na dhana potofu za watanzania wengi ambao kimsingi hao hawatakuwa wateja wako.
Kwa upande wa Watoto wa kishua, Foreigners soko lako litakuwa Juu.

11. Kwa Mwanamke, Kuwa mtafsiri Filamu kama DJ Mark, Murphy na Afro.
Dunia ya sasa ni nyepesi sana. Usiwe Limited wakati dunia haiko limited.
Tanzania bado hatuna madj wa kukalimani movies. Hii kwa wanawake wenye kuona fursa kwao ni fursa na itakuwa historia kuwa miongoni mwao madj wa kwanza kwanza nchi wakike.
Hiyo milioni Moja, itumie kujifunza na kununua vifaa vya kurekodia.
Kisha piga pesa.

Ninaendelea, ngoja nikale kibulu kwanza.
Ukiwa na swali uliza, wali wenye stress zenu pia uwanja huu ni wenu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ukitufikia ya ufugaji mbuzi//kondoo na ndege aina zote nipo
 
Naomba ufafanuzi mrefu namba 7 hyo ni martial arts gan znazofundishwa, ada zipoje na inachukua mda gan hyo kozi
 
Inategemea na mwalimu wako anapackage zipi.
Normally, USD 150 kwa kozi ya wikimbili. Kumaanisha miezi miwili kwenye mafunzo ya self defence sio pungufu ya USD 400
 
Naomba ufafanuzi mrefu namba 7 hyo ni martial arts gan znazofundishwa, ada zipoje na inachukua mda gan hyo kozi

Kujua itagemeana na wepesi wa mwanafunzi.
Ila normal ndani ya miezi sita unakuwa umekwiva. Mengine ni ukakamavu na mazoezi.
Alafu mazoezi ndio huchukua muda mrefu kuliko Skills za mapigano
 
Back
Top Bottom