Biashara United (Mara) | Special Thread

Biashara amepanda au bado ?.. Mwenye msimamo aweke
 
Tunapaswa kuwin game 1 kati ya 2 zilizobaki.. now tuna point 43
Kazeni watoto wa nyumbani
 
Kwanza mwakani watashiriki mashindano ya kimataifa ambayo ni hatua kubwa katika historia ya soka Mkoani Mara
Mimi nasikitika Mkuu wa Mkoa aliyekuwepo kwenda Tanga. Yule RC aliibeba Biashara United kama Timu yake, alitumia mbinu zoooote kuwapata wadhamini, kuwapa moyo wachezaji na njia nyinginezo za Kidiplomasia timu kuwa Imara. Hongera sana Mhe. Malima.

Sasa Mkoa umepata Bw.Mdogo mpuuzi, aliiiona LIPULI FC ikishuka daraja bila mbinu za Kiuongozi. Sasa kajja Mara, hatuna budi kuwa naye makini tangu mwanzo maaana huyu Mnyamwezi Bw.Mdogo hana busara za Uongozi zaidi ya jazba na mihemko.
Biashara Utd Aluta Continua
 
Hongera biashara kwa kufuzu kushiriki kombe la shirikisho Africa(Kimataifa)
 
Hongereni sana timu ya nyumbani fanyeni usajili makini kwa ajili ya mashindano ya shirikisho mwakani
 
Hongera sana biashara United,ushauri wangu tengenezeni structure nzuri ya uongozi,mpate viongozi wazuri,viongozi watengeneze mifumo mizuri ya kuendesha timu kwa ushirikiano na wanachama wao,watafute washirika wazuri a.k.a wadhamini,watengeneze miundombinu mizuri angalau viwanja vya mazoezi vya kueleweka,timu iwe na muendelezo isiwe ya msimu.Mwisho washirikiane na viongozi wa mkoa na viongozi wa ccm wakarabati uwanja wa kumbukumbu ya karume,ili mechi za kimataifa za nyumbani wachezee kwenye uwanja wao huo,itasaidia kuvuta mashabiki na kupata angalau fedha kidogo.
 
Ila bao 4 ni aibu kwa timu itakayowakilisha Tanzania Ligi Ya Afrika angalau basi wangefungwa hata bao 1
 
Azam wametuangusha washabiki wa biashara utd.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…