Biashara ya Bodaboda

Biashara ya Bodaboda

Japo napendelea bajaji, ila boda zinalipa pia.
👉Vipi ushawai fanya, au unasikia kwa watu🤔
👉Kama ndio, ni changamoto zipi zilikukumba.
👉Kufeli kwako, unahisi na wengine itakuwa hivyo??
👉Vipi Kama waki/tukiboresha mbinu na mikakati ili kuendana na changamoto zilizopo🤔🤔
👉 Never say it's impossible coz the word it's self says I'm possible
Nyie ndo wale motivation speaker kaz yenu kubwabwaja tu Lima matikiti heka sjui nn ingieni field kwa vitendo unakuta ata boda boda hujui ata kuziba pancha
 
Sawa bro hebu nisaidie Biashara ya mtaji ya 30M unatakiwa kupata Faida ya kiasi Gani? Na REJESHO La per day unatakiwa kupata kiasi Gani?

Maana hapo Mimi nilianza na mtaji Wa 9M ndio ukafikia hapo kutoka Pikipiki 4 za kuanzia mpka kufika 15.

Hebu nyie watu Wa UCHUMI au BIASHARA mnisaidie hapa Biashara ya 30 millions inatakiwa kuingiza kiasi/ Faida gani per day?
Si bora ungenunua hata coaster ukawa unalaza hata 80k au laki
 
Taja uwekezaji wenye afya sawa na mtaji wenye thamani sawa na bodaboda.

Kama hakuna kaa kimya
Makasiriko ya nini mkuu!!mwenye ka bucha tu ka nyama mwenye mtaji wa kg 20 tu ambazo gharama yake ni 110,000,akiuza kwa 8000 tu kwa kilo anapata 160,000 hapo faida yake 50,000 kwa siku tena mapema tu!!!eti mtaji wa 2.3 milioni kupata 3300/ =au mtaji wa milioni 34. Kupata 49,500 kwa siku ni haki sio sawa hata kidogooo!!jipeni moyo tu.
 
Mkuu mbona bado ndogo, imagine Kuna mtu Ana bajaji namba b 5 na alinunua 1.7 Kila 1. Leo hi anakunja 20 per each ×5 SI ni laki 1 hiyoo
Uzuri wa gari hata kama unapata laki moja kwa siku,bado itaendelea kuwa ni mali yako hata baada ya miaka 3 inakuwa imesharudisha pesa yako,na bado ukiiuza utapata pesa nzuri tu.Tofauti na hizi pikipiki na bajaji zimapokuwa za mkataba baada ya mwaka inakuwa mali yake au kwa bajaji miaka 2 inakuwa yake.Hapo ndipo kwenye utofauti.
 
Biashara ya boda inahitaji wew mmiliki uwe na akili ya ziada kucheza na akili za hawa madereva.

Kwa sababu wengi wao hawana malengo ya wanacho kifanya wanafanya ili wale, wavae, na kufanya vitu vidogovidogo akishapata pesa ya kula kwa siku si ajabu akasahau pesa ya mwenye chombo.

Ukiwaacha waishi kwenye comfort zone watakuchezea sharubu vizuri tu, ni wanahitaji uangalizi wa karibu sana
 
Kwa mahesabu ya Bro hapo juu Faida ya Pikipiki Moja ni 3300/= Kwa Pikipiki 15 tu ni Faida ya 49,500/= Kwa Siku Moja tu. Kwa mwezi mzima una faida ya 1,485,000/=.

Cheers [emoji1635]
Kwahiyo pkpk 15 zenye thamani ya 2.3mil x 15 = 34.5 milioni. Kwahiyo milioni 34.5 inaleta faida ya 3300 x 15 = 49,500 Kwa siku!??, Na bado Kuna watu hapa wanaona ni biashara nzuri pamoja na risk zilizozunguka biashara hii.. Ukiwa na pikipiki 15 zinazoleta 49,500 Kwa siku. Pkpk moja ikaibiwa au kupata ajali,Ina maana umepoteza 2,300,000 /49,500 = 46. Umepoteza faida ya pkpk 15 Kwa siku 46. Hii biashara inalipa kama utaendesha mwenyewe FULL STOP 🛑. Kinyume na hapo ni ukichaa.
 
Nimesoma comment zote nimeona mvutano mkubwa sana, lakini pia nimeona kuna mawazo yenye afya na mengine ni hafifu sana, mie ni dereva boda boda, changamoto za boda boda nazifahamu sana, lakini nasema hivi siwezi kuchukua pesa yangu mfukoni nikaenda kununua pkpk ili nimpe mtu, na mtu anaetetea labda atakua hajui hiki akisemacho ila anasikia kwa watu, ili upate pesa ya boda boda nunua pkpk endesha mwenyewe hapo utapata hela ila sio ununue umpe mtu hapo ni sawa na kubet.


Naomba mtu mwenye kujua biashara ya mtaji mdogo wa ml 3 anisaidie mawazo hapa ili nitoke huku niliko sasa kwenye boda kabla sijakatiako miguu.

Sehemu yoyote naweza kwenda kufanya.

Asanteni[emoji120][emoji120]
 
Kweli hiyo bajaji si itakuwa CHOMBO YA FUNDI??saa moja kijiweni ,masaa 11 gereji?yaani ktk vyombo vya usafiri ambavyo havidumu ni bajaji!!tena ukute inafanyia kazi kwenye rough road miaka miwili kwisha habari!!
Sasa mkuu ilinunuliwa kwa 1.7m, rejesho la 20 per day kwa zaidi ya miezi 15= haya faida umeijua tayari
 
Back
Top Bottom