Biashara ya Bodaboda

Nishafanya hii kazi Pikipiki zisizo za mkataba kutoboa mwaka ishu na ikitoboa haifai Pikipiki ya mkataba tu ndio huwa yatunzwa akijua ni Mali yake baada ya muda
 
Nyie ndio wale wasomi mlotoka chuo kaz hamtak mnabet tu mkitarajia muwe mamilionea sasa wewe faida ya 49500 unaona ndogo kwa siku tena kumbuka huyu ni kama kaweka ela yake kwenye mzunguko inaongezeka na hapo anasema Ana kazi anayofanya
Hili sio jukwaa la michezo la maneno tuu bila ushahidi muongeaji sana ndio mshindi!!!"yale ya kwa NKAPA HATOKI NTU" Naona kama umevamia jambo liliojuu ya uwezo wako!!faida ya 49,500 kwa siku kwenye uwekezaji wa 34M,ni utumiaji mbaya wa rasilimali fedha!!huo ndio ukweli mtupu japo mchungu!!hiyo faida ni ya muuza genge mwenye mtaji usiozidi laki 2!awe na kazi nyingine asiwe nayo bado ki biashara haikubariki!!mfano hiyo pesa angekuwa amekopa kwa returns hiyo ya 49,500 ,angeweza ku u service mkopo kweli?!!jibu ni hakuna!!
 
Yaani hata ukimtafuta kijana awe ana kuletea kila siku 7000/= jua tu kuna siku ana kwambia biashara mbaya wiki nzima anakuletea 30,000!! Na akianza kulimbikiza tu kosa!!!baada ya mwaka sio pikipiki tena!! Inakuwa kama zile za wazee wa kukalia tenki(wauza mkaa)!!kifupi hii biashara unaweza kuona faida yake kama utanunua halafu uendeshe mwenyewe kinachopatikana chote ni chako,na chombo utakitunza.
 
Mkuu zipo Hadi laki 8 Tena namba c, ila ni used ikiwa katika ubora. Mi nilinunua namba c kwa laki 7.6 mkuu
Mkuu kuna mtu kafungua kama kikampuni chake anauza pikipiki used. Kuna TVS ya cc125 anaiuza kwa laki 6 na 80! Kwa utalamu wako hii inaweza kuwa iko safi? Nataka kununua
 
Mkuu kuna mtu kafungua kama kikampuni chake anauza pikipiki used. Kuna TVS ya cc125 anaiuza kwa laki 6 na 80! Kwa utalamu wako hii inaweza kuwa iko safi? Nataka kununua
👉je unataka kufanya ya biashara au matumizi binafsi🤔🤔
👉mkuu zingatia haya ni namba ipi??a,b, au c
👉Imekaa muda gani??, Toka inunuliwe
👉Tafuta fundi mzuri na mzoefu, akakague injini. Maana ndo Roho ya chombo.
👉 Hakikisha haina Deni tra.
 
Nikutie moyo mkuu, hii biashara nzuri sana na tunapambana nayo, mimi ninazo 5 Kinglion mpya kabisa. Nimeenda nazo kwa mkataba na kwa mwezi jumla zinarejesha 1.5M

Pikipiki moja ni 2.6M mpaka inakaa barabarani, mkataba miezi 14, pesa yangu inarudi miezi nane, na miezi sita ni faida.

Mimi sijui kama haina faida ninachojua pesa ya pikipiki yote ipo bank na ikifika mwisho wa mwezi nachota iliyopo naweka Fixed account

Sijawahi tumia hata mia ya hii pikipiki (mfanyakazi serikalini) zikimaliza mkataba nitaagiza ndinga yangu maana ndo malengo


Make sure pesa hawakupi mkononi, iweke bank na uwekeze kweli usitangulize njaa.

Mahesabu ya boda natunza kwenye google sheet.
 
Yeah ni kitu sahihi, Kuna rafiki yangu ana biashara hii iya usafirishaji. Ila yeye amebase upande was bajaji.
👉Inamlipa Sana.
 
Asante mkuu, nataka kwa ajiri ya biashara ya bodaboda! Mi sio mtalaam sana ila hizo namba a,b,c ndo sijazielewa, zina impact gani kwenye kazi?
 
Mkuu kwenye hii excel/sheet kuna column naona umeweka rangi nyekundu, njano na light blue zina maana gani? Japo nimeipenda sana hii inasaidia kuwa na kumbukumbu ya mahesabu
 
Asante mkuu, nataka kwa ajiri ya biashara ya bodaboda! Mi sio mtalaam sana ila hizo namba a,b,c ndo sijazielewa, zina impact gani kwenye kazi?
a,b,c amemaanisha pikipiki zilizotumika na mtu mwingine kwa kipindi fulani kisha anakuuzia wewe kwa kifupi ni pikipiki chakavu.
Usijaribu hata kidogo kununua pikipiki iliyotumika utakuja kujuta yalishawahi kunikuta hayo nilinunua pikipiki kwa mtu nikaitumia wiki moja baada ya hapo ikawa inaenda gereji kila siku.
Labda huyo anayekuuzia awe ni mtu wako wa karibu uwe na uhakika ameitumia kwa miezi michache tu isizidi miezi 12,uwe na uhakika kweli anauza kwa sababu amepata dharura lakini pikipiki bado ni imara.
 
Aise umenitisha sana, kuna mahali nilitaka kununua pikipiki used ila nishaanza kuogopa sasa!
 
Dah! Asante sana kaka kwa ushauri! Ila si naweza nikabahatisha kupata pikipiki used ambayo iko vizuri eti?
Kuna Pikipiki used zimetumika mpka 3 Months unapata Hadi Kwa 1.6M - 1.8M, Cha msingi ni kuangalia RISITI ya Pikipiki usije ukapigwa na hapa.
 
Mkuu kwenye hii excel/sheet kuna column naona umeweka rangi nyekundu, njano na light blue zina maana gani? Japo nimeipenda sana hii inasaidia kuwa na kumbukumbu ya mahesabu
Mkuu hizo rangi huwa naziweka siku napopitia hesabu za mtu fulani, na piah kuweka kumbukumbu ya event husika
 
Dah! Asante sana kaka kwa ushauri! Ila si naweza nikabahatisha kupata pikipiki used ambayo iko vizuri eti?
Kaka ile juzi nilishindwa kukujibu, baada ya Jamaa kuzipondea pikipiki. Ila mbona used zipo nzuri Sana Tena namba b au c ilimradi injini I we vizuri.
👉Tafuta fundi was kukagua injini.
👉Baada ya kuinunua, ipige service ndogo I'll kuiboresha Zack j
 
Mkuu kwan hao tra unakuwa unalipa kodi kila siku ama ni kwa awamu (installments)?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…