Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Daaaahhhhhh!!!!! Nashukuru broo kwa msaada wako !!!!
Ngoja nianze kuhangaika... baada ya wiki mbili nitaleta mrejesho hapa MUNGU AKIPENDA
 
GPA hata ingekuwa 5.0 kama huna hela ni boya tu. Fikiria kuuza Kitimoto ndo mwake-mwake. Hata wavaa kobazi wanamkubali mdudu japo kimya kimya
 
Kama mie kuna mahali naendaga kufata pilipili ya maji yenye kitunguu saumu ile. Nikifika cha kwanza nataka kujua kama ipo, incase haipo sili nasepa
 
Daaaahhhhhh!!!!! Nashukuru broo kwa msaada wako !!!!
Ngoja nianze kuhangaika... baada ya wiki mbili nitaleta mrejesho hapa MUNGU AKIPENDA
Watanzania hususani vijana tuna takiwa tuwaze hivi ili miaka kadhaa ijayo angalau asilimia kubwa tuta kuwa nasi tume punguza tatizo la ajira.. Wewe uki ajiri mtu mmoja..mwingine wawili..mwingine watatu..mwingine mmoja basi pole pole ndo mwendo.. Changamoto ya hiyo biashara n kumpata mtu sahihi kama hauifanyi wewe ila usivunjike moyo mm wali nisumbua sana mara ya kwanza kuleta hesabu ila sasa namshukuru Mungu nime wawekea utaratibu mpya tuna enda nao vyema tu
 
Ni kweli unachoongea broo!!!!... fursa zipo nyingi, imagine dar kuna population ya watu 5 million, hao wote wanahitaji kula na kuvaa
Inabidi tufikirie positive...

Nashkuru sana broo!!!! Nitakucheki kila changamoto nitakayoipata unisaidie kuitatua.
 
Kijana io pesa nikubwa sana...kama ulivyoshauriwa na mdau apo juu io pesa inatosha kabisa changamoto ni pango au sehem yakuuzia,
Kwa mfano mimi ilinilazimu kutumia jiko la gesi kwasababu ya mazingira (chuo) watoto wachuo wanapenda madoido kinoma..apo nlijaribu kusatisfy custumers wangu...
Otherwise ningepambana na hayo majiko ya pumba
 
Ila biashara hii usiwe mtu wa kushoboka na mademu. Maana utaishia kugawa chips-kuku bure kwao ujira wa KIPOCHI MANYOYA mwisho wa siku unabak na madeni kwa "supplier" wa viazi, mafuta, gesi n.k
 
Kuna dogo alikuwa ananipigia kazi maeneo ya Tabata alikuwa muaminifu sana,sema tu biashara eneo lile ilikuwa ngumu that's why nikaachana nayo.Kama utamhitaji mfanyakaz muaminifu uni pm coz dogo mpaka leo anahita kazi.
nipe nmba zake mkuu
 
Wakuu habari za mchana kwa anae fahamu vijana wa kukaanga chips malipo yao yanakua kiasi tafadhali anijuze...
 
Wakuu habari za mchana kwa anae fahamu vijana wa kukaanga chips malipo yao yanakua kiasi tafadhali anijuze...
Itakuwa vizuri kama utamwajiri bila kumlipa mshahara, bali chambua ufahamu gunia la viazi na gharama nyingine kama mafuta, mkaa n.k litanatoa shilingi ngapi, baada ya hapo awe anakulipa hesabu kwa siku kama Bodaboda, Bajaji au Daladala. Hiyo itamfanya aone kama naye ni sehemu ya kazi hiyo na atajituma zaidi. Changamoto ya kumlipa mshahara ni kwamba atakuwa na uhakika kuwa hata asipofanya kazi kwa bidii, mwisho wa mwezi atalipwa tu.
 
Shukrani mkuu kwa mchango
 
Umenikumbusha mambo za: piece rate na time rate
 
Mm pamoja na kuwafanyia njia hii lakini napo vijana wakashindwa biashara kichaa hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…