Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

wengi walioshauri hawakufikiria hili....siku hizi huibiwi hela,wafanyakazi wanaleta vyao wanauza eneo lako ukija unaambiwa biashara ngumu na bidhaa zako unazikuta!!! huu huwakuta sana wenye baa.
Ndio maana kwenye biashara hatoshi kumuajiri mtu tu, hadi mwenye biashara anatakiwa awe muajiriwa hata wa part time. Usiache biashara luzi kwa kuwa umemuajiri mtu.
 
Zero what if naamua kusimamia mwenyewe hapo inakuaje? Yani mimi as mmiliki ndo nakua mpokea hela hapo nakaa hadi muda wa kufunga.
 
Kusimamia mwenyewe biashara ndio itakuwa stable kwa sababu kila kitu kitakuwa juu yako,

Sema kudumu na wafanyakazi itakuwa mtihani kwa sababu wengi wataona unawazibia mirija yao ya upigaji
Nimekuelewa. Asante sana.
 
Hii mishe yako ya kuua nguvu za kiume za vijana ishindwe kwa jina la Yesu!
 
kati ya deep fryer inayotumia gas na umeme ipi ni bora na nzuri katika kuleta faida?
na gharama zake ni kiasi gani

msaada wako tafadhari
Usinunue deep frier ya dukani ka una mipango ya muda mrefu kwenye hii biashara, Kachonge deep frier kubwa na zenye uimara na uwezo zaidi kwa wale wachonga majiko wa keko gerezani karibu na workshop ya Bakhresa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…