Huwa napokea PM nyingi sana za wadau wakitaka kujua mchanganuo wa biashara ya chipsi,
Yaani kuanzia vifaa, mtaji wake na Nk.
Kiukweli siwezi kujibu PM ya kila mdau kwa wakati sasa nimeona bora nipaste kile nilichowaambia baadhi ya wale waliotaka kujua hapa ili kila mtu anaehitaji kujua asome hapa,
Mchanganuo wa biashara ya Chipsi ni huu, hapa ni kwa ule mtaji wa kawaida kabisa,
Kwanza kabisa vifaa vyake muhimu
1: ile kabati ya kuhifazia chipsi inatakiwa iwe kubwa kiasi ngazi mbili au tatu itapendeza zaidi hapo kiasi ni 150k-250k
2:majiko mawili moja ya kuivishi chipsi nyingine ya kuchomea chipsi mayai mishikai N. K, hapo kila jiko itakost kuanzia 35k--45 kwa hiyo total pigia tu 90K,
3:vifaa vidogo vidogo kuna karai 10k--15k,sahani Dz 1 au 2 fanya 10K,koleo 3k,flampeni 2 5k, beseni dogo na kichujio chake kwa ndani 10K, vitu vidogo vidogo fanya 15K,
4:uje kwenye mazaga yenyewe.
Viazi gunia inategemeana na eneo ila bei kuanzia 45k--60k,mafuta ya kula ndoo ndogo 30k,mkaa gunia moja inategemeana na eneo ila approximately ni 25k--40k,mayai tray 3 24K
Kwa kifupi kama hauna kifaa ata kimoja unatakiwa usiwe na chini ya 500k, na hapa ni kibanda tu cha kishkaji.
Faida zake,
Chipsi zina faida sana kama ukikaa location inayoeleweka inayoweza kumaliza kuanzia nusu gunia la viazi mpaka gunia moja na uwe na msimamizi imara huwezi kosa kuanzia 25k--45k kwa siku kama faida,
Hapo weka vyuku vyuku mishikaki,juice na N.k faida inakuwa mara dufu
Onyo/NB.
kila biashara ina changamoto zake siwezi kuwa mchoyo wa kushindwa kukwambia haya, hii biashara ya chipsi ukitaka faida Usiwe na masihara ya kucheka na mademu, zingatia kipimo chako usisikie ya mteja anasema nini eti chipsi sishibi sijui chache mwambie aongeze hela umjazie ukileta utani unafunga kibanda.
CC Zero IQ