Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

wakuu
Ni miezi sita sasa imepita tangu nilipojitokeza hapa jamvini nikiwa na kiasi cha shilingi milion 1 pesa nikiwaomba mnipatie muongozi wa kufungua banda la chipsi zenye ubora wa kiwango cha juu na kukamata soko dhidi ya wapinzani wanouza chipsi locally

Aiseeeee, nilijuta na mpaka sasa najutia uamuzi wangu wa kulileta lile bandiko langu humu
Kiukwrli sikuweza kuendelea na lile wazo kwasababu wananchi wengi humu walinipinga na kunikatisha tamaa sana kwamba wazo halitekelezeki, hii ilinikatisha tamaa

Ile pesa niliamua kutulia nayo, hii ndio ilikua mistake kubwa
pesa haitulii kabisa, nilijaribu kuituliza lakini wapi mwishowe yote ikapukutika kwa sababu tu ya ushauri butu wa wajf walionikatisha tamaa

mbaya zaidi kilichosababisha nilete mrejesho humu, leo nimekatiza ile mitaa niliyokuwa naiplan kufungua ile biashara nimekuta mtu mwingine amefungua biashara ileile ya chipsi tena kama kahamisha mawazo yangu na kuyatekeleza
nimejaribu kumuuliza ni kiasi gani kainvest kasema kaweka milion 1 tu, hii imeniuma sana

Nimeamua kula chips kuku tena tamu kweli na kuishia kufyonya tu huku nikikumbuka michango ya wadau wa humu

Humu kuna watu hawapendi wengine tufanikiwe!
Humu kuna watu wanajifanya ni wataalamu wa kila kitu
Humu kuna watu kila uzi lazima wakoment

Tafadhalini sana, Jf tutoe mawazo bora na kujenga na si kukatishana tamaa kiboya tu na kuziacha pesa zipigwe na wengine
 
Ukiwa na wazo lifanyie utafiti wewe binafsi ingia field kusanya taatifa za kutosha fanya upembuzi wa kutosha kama utaweza au lah! Kamwe usiweke mezani wazo lako
Mwingine atakujib milioni moja kauzie karanga barabarani wakati anatype hivyo yupo sebuleni kwa dada ake anasubiri chai na maandazi.
 
kweli mkuu but jf pia ni sehemu ya kufanya utafiki ingawa kwenda field moja kwa moja ni muhimu zaidi nimetambua hilo@fdizzle,
 
Sasa Kama Uliogopa Kufungua Banda Kwamba Utapoteza Hela Yako, Mbona Hujafungua Na Hela Ushapoteza ?

Sana Sana Umebaki Na Mzigo Wa Majuto !
 
Ina maana ulitafuta ushauri humu tu pekee?! Kama ndivyo kosa ni lako mwenyewe
 
Mkuu ulimuuliza mtaji alotumia Je ulimuuliza changamoto alizo kumbana nazo na zimemfanya atumie kihasi gani ?

Biashara hiyohiyo unaona ipo unaweza kuta mmiliki analia.
 
nilijaribu kumuulizia kiwango alichowekeza hakina utofauti na nilivyokuwa nimepanga but issue ya changamoto sikuuliza
Kiufupi jamaa amefanikiwa
Mkuu ulimuuliza mtaji alotumia Je ulimuuliza changamoto alizo kumbana nazo na zimemfanya atumie kihasi gani ?

Biashara hiyohiyo unaona ipo unaweza kuta mmiliki analia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…