Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Wakuu heshima yenu.

Naomba mwongozo kidogo, ndoo kubwa ya viazi, inaweza toa sahani ngapi?
 
Ndugu naomba ufafanuzi juu ya biashara ya chipsi kwa yeyote anayefahamu na requirements zake.
Ukisoma huu Uzi ushauri wa msingi utakaoapata ni
1. Usiogope kuibiwa bali hakikisha faida inapatikana
2. Usimbane sana mtumishi wako maana naye ni binadamu na ana malengo zaidi ya hiyo 5000/- unayopanga kumlipa kwa siku, hivyo mpe hesabu akuletee kiasi gani kingine atajijua yeye
Na kadharika na kadharika
USHAURI WANGU; unaweza ukamkabidhi kijana Banda akuletee 25000 kwa siku wakati kwa mbinu za kibunifu na kibiashara (ambazo yeye anayefanya kwa mazoea hana) unaweza ukaikuza faida mara dufu na ndio ukamwachia
Yeye aandae na auze, wewe chukua jukumu la marketing
 
Hapa ndio nawakubali Ma Ras. I and I
 
Inategemea na hilo goli lenyewe, kuna ambao wanawekeza pakubwa.
 
Mswahili bana, we mwenyewe umechoka halafu unataka kujifanya ofisa uje kukusanya hesabu tu?

Hivi ni lini mtajifunza kwa wahindi? Hebu pita migahawa ya wahindi kama hujawakuta mke na mume wanakaba wenyewe cashier.
😂😂
 
Kuna dogo alikua anauza chips hapa kitaa, nafasi ndogo kutofautisha na wapinzani wake...
Ila ukionja mishikaki, kuku na chips zake kesho unarudi, binafsi nilikua mteja wa mishikaki.
Wadada wa mujini wamempurusa mtaji wote.

Dogo hakuwahi kulaza bidhaa.
 
😂😂
 
Assalamualaikum warahmatullah wabarakatu kwema ndugu zangu mi Nina changamoto Moja nafanya biashara ya chips lakini tangia nianze hakuna faida yyte ninayopata sasa nilikuwa naomba msaada wa ushaur Nini nifanye kuboresha biashara yangu Ili nipate faida
 
Pole sana mkuu.. hiyo biashara ni pasua kichwa. Kwanini usibadili ukafanya biashara nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…