hahaahh kweli The Boss kuna watu wanaoenda kachumbari kuliko chipshongera kwa ujasiria mali
nafikiri changamoto kuubwa mno ni kujua hasa viazi vizuri ni vipi
kuna muuza chipsi mmoja huwa najiuliza why chips zake ni nzuri kila siku na watu wanapita
watu weengi kumfuata.....siku moja nikamsikia kabisa anasema kuna viazi na viazi
yeye viazi vyake anavifuata sehemu na anavijua kwa macho....
kabla ya hapo mi nilifikiri viazi vyote ni sawa tu kumbe kuna siri hapo
kingine usafi wa dogo na vifaa na kachumbari iwepo nzuri na usiwajibu wateja 'kachumbari imeisha'
wengine kachumbari ndo muhimu kuliko chips.........
hahaahh kweli The Boss kuna watu wanaoenda kachumbari kuliko chips
yaa jumamosi nitakuwepo mara chache kuangalia biashara inavyokwenda
yaaa viazi vya kilimanjaro sio vizuri kwa chips vinanyonya maji sana hivyo hutumia mafuta mengi mpaka kukauka si unajua kilimanjaro ardhi yake ina maji vya mikoa mingine ndo vizur na pia kimi nikiviangalia kwa macho navijua vipi ni vipi......,nishalimaga sana
usafi wa dogo ni changamoto kubw sana si unajua ukidili na viazi plus mafuta plus moto
thanx nitakwambia mahala nipo one weekend uje na marafiki zako
Nyengine kabisa, usimbane dogo, wee mwambie tu kila jione akutumie m-pesa 25,000. Wewe unalipa kodi ya kibaraza ila garama nyingine zote juu yake, atajua ajilipe vipi. Hapo ikikaa sawa utaona faida yake
shee! ndito haya maswali unayouliza humu si ulitakiwa uwe umepata majibu ndo ukanunue karai la kukaangia hizo chipsi na kumtafuta dogo? Mi naona umeanzia mwisho kwenda mwanzo kwa hiyo unafanya biashara ya kubahatisha. Unataka sehemu classic? Anzia hapo hapo kibarazani ili ujifunze changamoto za chipsi kwa vitendo. Na brand yako ya chipsi unamaanisha kama kina merry brown na kfc? Si ndoto mbaya.
Changamoto kubwa ni wanawake wenzio, sijui chips wanaipendea nini kiasi cha kukubali "kuliwa" sababu ya chips na soda tu.
Watamrubuni kijana wako mpaka wajiwekee uhakika wa kupata chips za bure kila siku jioni! Sasa uombe Mungu awe mwanamke mmoja maana wakiwa watano waliofanikiwa kumrubuni kijana wako ujue umeumia.
Nyengine kabisa, usimbane dogo, wee mwambie tu kila jione akutumie m-pesa 25,000. Wewe unalipa kodi ya kibaraza ila garama nyingine zote juu yake, atajua ajilipe vipi. Hapo ikikaa sawa utaona faida yake
Nitakuja asante
wawepo na kuku wa kuchoma
watampwelepweta bure...
naomba aliyewahi kuifanya aniambie changamoto zake kulingana na eneo alilowahi kufanyia
nishanunua vifaaa na nishampata dogo mmmoja sehemu kuna mchanganyiko wa watu na ela ya kulipia kibaraza sio kubwa maan ninaeka na kafriji
sasa nataka kujua ni mambo gani ya kuzingatia lakini pia nilitaka niweke sehemu kubwa kidogo ila sijapta sehemu ambayo ni classic on the long run nitengeneze brand yangu ya chips
msaaada
sasa tatizo jingine nataka kujua changamoto za hii mambo japo hiii ni biashara yangu ya pili ya msosi ila sio nyanja hiii
plz msaada kwa aliyewahi ifanya
Hiyo biashara niliwah fanya bt changamoto ni dogo kuwa msafi, mwaminifu na mwenye kauli ya kumuita mteja na cyo kumfukuza...
masai dada ulidhamiria hii post ikae hapa?
hili nalo neno
hifi utafiti unajua suzuki carry kwa siku ni shingapi hapa dar??elfu 20
actually biashara ya chips inaingiza ela kubwa kuliko suzuki carry hapo USIIOMBEEE AJALI
Mie sijui bhana
changamoto kwenye biashara hii[hata kama utapata eneo lenye wateja 100,000 kwa siku] ni kuibiwa. inaibiwaje? ukimuajiri mtu utaibiwa kiufundi sana, wauzaji uliowaajiri watakuwa wanaleta viazi,mayai,kuku,nyama ya ng'ombe,mbuzi VYA KWAO.
sasa wewe kama uliwapa hela ya gunia mbili au ulileta gunia mbili watauza gunia lako nusu halafu wataleta gunia lao au hata magunia yao mawili ya vizi na watauza,wewe ukija jioni kuhesabu unakuta wameuza nusu gunia na gunia lako moja na nusu lipo. hivyo hivyo watafanya kwenye mayai na nyama.
solution ya wizi huu ni wewe kuwepo kwenye biashara yako.