masai dada
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 16,207
- 14,343
Inategemea na eneo ulipo pia, kama ni dar Kinondoni hata saa kumi na moja alfajiri unapata chips tena za moto tu, sehem nyengine mwisho saa tano na chips kwa kawaida zinaanza kuuzwa jioni kwaio suala la mda nalo linazingatiwa ili 'tajiri' achungue ngapi
Niliifanya kitaa ila palikua na mzungu wa watu, viaz km viaz havina faida xana, endapo utakua mjanja kuweka vifuatavyo utakua na uhakika zaid; mishikaki, ndizi, soseji, samaki, kuku na vinywaji km vile juic za matunda na soda na maji...
wewe pia ni kijana13 nimekujibu pm naona kimya ongeza 10niulete mzigo itakuwa ni kila siku wa kwako mi unaleta nyt tu na cash
nijibu huko tumalizzane nimekujibu naona kimya
je utamuanzishia na ngapi???utampa kila kitu viazi,mayai and the like alafu atalipa au inakuaje elaborate kidogo hapo
sitaweza nina majukum chungu nzima yaaani wakoloni wamekua wakali na wakikuongezea hata 100 katika salary basi ndo inakua shughuli si ya kitoto si umeona hata uwepo wangu humu umekua magumashi tangu january ni shidaa
MI NAONA HIVI KWA SIKU MI NAMWAMBIA ANILETEE LETSAY 30000 nitamuanzishia kwa kumnunulia labda kuku 10,viazi gunia moja,na mayi tray kazaa so kutoka pale nitakua nachukua ela tu kiasi flani yeye hata akipata laki ngapi jitachukua tu kiwango cha ela nilichopangiana nae
kama alivyoshauri bwana utafiti hapo juu
Changamoto kubwa ni wanawake wenzio, sijui chips wanaipendea nini kiasi cha kukubali "kuliwa" sababu ya chips na soda tu.
Watamrubuni kijana wako mpaka wajiwekee uhakika wa kupata chips za bure kila siku jioni! Sasa uombe Mungu awe mwanamke mmoja maana wakiwa watano waliofanikiwa kumrubuni kijana wako ujue umeumia.
Unampa kila kitu kinachohitajika, kwamaana kwamba hapo mtaji ni wako, thn kama wiki moja hivi unaangalia biashara inaendaje, vikiisha vile vitu vya mwanzo, yaani mafuta, viazi, mkaa, ndio utapata jibu. Utakua unajua mauzo na matumizi kwa siku ni shingp, na inayobaki ni ngapi, kama una na vinywaji basi uwezekano wa 'tajiri' kupata 25 mpka 30 kwa siku upo...
Hapana mimi sio kijana13.
nicee
so vitu vya kwanza vikiiisha nitanunua tena mimi au tunafanyaje hapo
Hapana, ukishakamilisha KILA KITU kuanzia hapo biashara inajiendesha yenyewe, tomato ikiisha anatoa kwenye hela aliouza jana anaenda kununua, na sikweli kua mauzo yote anaenda kununua vitu, hua haviishi kwa pamoja, leo mafuta kesho mkaa, na hivi sio kila siku, vyakila siku ni ile kachumbari tu
asante sana utafiti umenifungua pakubwa sana
Karibu masai dada,
Mimi nikija usiniwekee pilipili nyingi sipendi.....
Nafikiri umepata mengi ya kuanzia natumaini utafanikiwa, kwa mimi ninavyojua mbali na kuuza kila kitu lakini huduma ikiwa nzuri kwa wateja I mean kukaribisha watu kwa uso mkunjufu, pindi unapoona mtu amefika, Karibu na tabasamu na kumuonyesha pa kukaa inasaidia sana. Badala ya kumwacha customer anazubaa na au kuondoka,
Ni biashara nzuri ila uaminifu kwa mhudumu ni jambo la msingi. Niliwahi kuifanya maeneo ya Mabibo hostel-Dar kitambo 2003 si unajua kupandisha bumu, ila sikuwa na mhudumu mzuri kwasababu baada ya kuona inaenda vizuri siku hiyo kauza sana, mimi ikiwanakomaa na nyanga za slub akaamua kutoroka na vitu kuviuza. Nilimtafuta nabaada ya wiki nikamata na kumpeleka polisi hana hata shiligi. ilibidi niwe mpole tuu na kuachana nae!
asante sana utafiti umenifungua pakubwa sana