Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Itakuwa vizuri kama utamwajiri bila kumlipa mshahara, bali chambua ufahamu gunia la viazi na gharama nyingine kama mafuta, mkaa n.k litanatoa shilingi ngapi, baada ya hapo awe anakulipa hesabu kwa siku kama Bodaboda, Bajaji au Daladala. Hiyo itamfanya aone kama naye ni sehemu ya kazi hiyo na atajituma zaidi. Changamoto ya kumlipa mshahara ni kwamba atakuwa na uhakika kuwa hata asipofanya kazi kwa bidii, mwisho wa mwezi atalipwa tu.
Jibu Zuri zaidi
 
Wakuu habari za mchana kwa anae fahamu vijana wa kukaanga chips malipo yao yanakua kiasi tafadhali anijuze...
[emoji15] [emoji15] duh kwani hii kazi imekua kama zile za ualimu,udaktari n.m!!!? Malipo mnakubaliana wenyewe bhn, sasa kama kwa siku unaingiza 25k then tukakushauri umlipe 30k utamlipa? Tenga % ya mauzo kwa siku/mwezi yanayopatikana uwe unachukua wewe na % nyingine achukue yeye
 
Inategemea umepata kijana kutoka eneo gani, kama ni Mgogo hata ukimwambia kuwa asikuletee chochote bali pesa yote achuke, atashindwa tu.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] una utani na makabila ya watu
 
ZA asubuhi hii Wadau
Nimekuwa nikiwaza namna ya kuanzisha mghahawa kwa mda mrefu na sasa naona kama wakati umefika.
Ingawa nahitaji kuuza chakula ila nimeona nianze na chips halafu vigine vitafata pole pole..
Ninachohitaji kujuwa kutoka kwa wazoefu ni.
1. Namna ya kuboresha chips lakini ziwe na faida.
2. Faida ninayoweza kutegeneza.
3. Vitu gani nikiweka kama nyogeza mfano.. kachumbali.. vitaweza kuvutia wateja zaidi.
4. Wazo lolote zuri unaweza ukaniogezea.
Mimi sitakuwa kuwa mpishi kwa hiyo itabidi niweke mtu wa kupika..
Tayari nimepata eneo na ni karibu na stand ndogo hivyo kuna muingiliano wa watu.
Nakaribisha wazo na ushauri. Na kama unaona tunaweza kuongea kuliko kuandika. Basi sio mbaya ukanipa namba yako PM na nitakupigia.

Mwanza kwetu.
 
Chips zinalipa jipange tuu ziwe za ubora all the best
 
mkuu biashara hiyo si mbaya unaweza anza na chip na vinywaji baridi ili kuwavuta zaidi, ubora wa chips pamoja na mishikakina kuku ndo hutufanya tuje kila uchwao
 
Chips zimenye mapema uziloweke kwenye maji yenye chumvi

Mishikaki imarenate vizuri kuongeza ubora

Kuku loweka na ndimu,mint leaves chumvi na tangawizi +garlic halafu ukatie kitunguu maji, kuna mahali niliona wanawaloweka na unga wa ngano Ila bado Sijaelewa vizuri

Chagua siku uwe na special plate
Labda ya biriani ama mbuzi ama pidgin unique lisilopikwa na watu wengi

Offer delivery on time
Nunua microwave usilishe wateja vyakula vya baridi

La muhimu zaidi ni usafi wa mazingira,vyombo na wahudumu,
Weka maua nje ama ndani inaleta uhai wa eneo
 
Back
Top Bottom