Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Asante Mkuu ukifanikiwa kupata taarifa yeyote nitashukuru sana.
Mkuu nmerudi.....
Nmeulizia huo uduvi juzi apaa nlipata nafasi nlikuwa sokoni kilo yake ilikua 7,000....Ila Kama upo tanga unaweza ukaweka order kwa wavuvi nadhani Bei itapungua zaidi ya hapa
 
Mkuu nmerudi.....
Nmeulizia huo uduvi juzi apaa nlipata nafasi nlikuwa sokoni kilo yake ilikua 7,000....
Ila Kama upo tanga unaweza ukaweka order kwa wavuvi nadhani Bei itapungua zaidi ya hapa
Asante sana Mkuu kwa taarifa nzuri kutoka kwako je nikiwa Tanga ni maeneo gani ya mwambao ninaweza kuwapata wavuvi wa uduvi?
 
Ahsante sana aiseee
 
Sasa hizo dagaa za mwanza naweza kuziptaje japokuwa soko cyo shida kwa kweli coz kwa dar Kila kitu kinaenda Ila ww tu na utayar wako
 
Hupatikan namba zte boss
 
Habarini wajasiriamali wenzangu, nimerudi mezani naomba msaada kuhusu biashara ya dagaa wa Mwanza. Natamani niwe nasafirisha mikoa ya Morogoro au Dodoma. Mtaji nilionao ni kama laki na nusu, je itatosha? Na je ni vitu gani vya kuzingatia na mimi kwa sasa nipo Mwanza nawaza niwe nazituma Moto/Dodoma.
 
Laki tano inatosha kwa kuanzia,itakuwa taratibu kama utakuwa na nidhamu ya fedha.,usilete kwanza mikoani...we we nenda kisiwa goziba,au kimoyomoyo,mlumo,ghana,ukawe unanunua dagaa wabichi unawaanika huko huko wakikauka unauzia huko huko mpaka mtaji utakapokuwa mkubwa kuweza kusafirisha mikoani,

AU huko huko visiwani nunua then safirisha uje uuzie kirumba mwaloni...usihangaike kupeleka mikoani...
Sina uchoyo na wazo la biashara kumsaidia mtu yoyoye.
Mwingine anayehitaji ushauri zaidi wa biashara ya kufanya sema hapa nitakupa cha kufanya ili mradi tu uwe na ule msukumo ndani ya moyo wako kufanya biashara bila kutafuta sababu.
 
Boss! Nimependa

Boss! Nimependa Sana ushauri wako,na nimependa Kwa jinsi ulivoonesha moyo wa kumsaidia mtu kimawazo.
Binafsi napenda Sana biashara ya dagaa Ila Mimi nafanya biashara ya dagaa chafu Kwa ajili ya chakula ya kuku. Niseme ukweli namtumia dalali ambaye nikinunua mzigo huku mwanza nafunga nakumkabidhi dagaa anapeleka kiwandani alafu akimaliza kuuza ananiletea mtaji na faida yangu.

Nafanya vile kwasabb nafanya kazi za serikali na siwezi kuzifanya mwenyewe. Wala siwezi kupata mda wa kupeleka dagaa mwenyewe,kwahiyo mwanza nachukua let say dagaa wa milion 3 au mil5 namkabidhi. Anaenda kuuza Arusha na sijui anapata faida kiasi gani Ila Mimi ninachojali aniletee faida nzuri. Na mpaka sasa dalali huyo Niko naye ndo tunafanya biashara wote,NAOGOPA KUMWAMBIA TWENDE WOTE MAANA ATAONA KAMA NIMEMSTUKIA NA ATAWEZA KUNIKIMBIA,KUSEMA KWELI SIJUI MASOKO YAKO WAPI ARUSHA NA SIJAWAHI KUFIKA JAPO NATAMANI NIFANYE MWENYEWE.

MWENYE KUNISAIDIA MAWAZO PLEASE 0764789563
 
Ila hii biashara nayo itakuwa inalipa sana,naona fuso kirumba mwaloni zinapakia daily,
kuna dada wa kikenya alikuwa anafuata mwaloni hao dagaa wachafu kwa ajili ya kupeleka nairobi kwenye viwanda vya chakula cha kuku ,alikuwa na pesa chafu ,
nadhani hao wanaopeleka arusha huwa wanavuka hadi Nai.

Kuna jamaa mkenya ana kampuni ya marketing research,yeye unamlipa pesa si nyingi anafanya legwork kuzunguka Nai kulitafuta chimbo,sema link yake ndo iko mbali nikiipata ntaiweka hapa,yeye anaweza kukupa infor zote kuanzia bei,procedure,mbinu na contact za hivyo viwanda vya chakula cha kuku na wala fee yake haizidi 20,000 ya kibongo
 


Duh..!kuna mtu anapeleka dar hao dagaa wa chakula cha kuku..anasema ukipeleka trip moja ww ni tajiri!bas kweli anakupiga!lakin km inakulipa sio mbaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…