Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Kumbuka ndo anaanza biashara
Biashara yenyewe dagaa wa kukaanga
Asifungue ofisi kwanza mpaka apate mzunguko mzuri wa biashara asijepoteza hela ya kodi bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elekeza unakopatikana na aina gani ya samaki maana wa magamba wako wengi
Au labda Kama unataka ufanye biashara na mtu mmoja sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni hatua kubwa na ya kupewa kongole kuweza kuweka akiba, pamoja na kufanya utafiti wa biashara unayotaka kuifanya.

lakini bado hujamaliza utafiti wako kelele za nn ? rudi na upande wa dar uone uhitaji wake na vile wauzaji wengine wanavyouza ili ujue kama na ww utapata faida.

Lakini mkuu endelea na utafiti vipi ukichukua wabichi na kukaanga mwenyewe gharama ni hizo hizo ? ebu jaribu kuwaza zaidi na zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kufanya haya.

1. Njoo Dar, Nenda soko lolote kodi meza then ukiagiza mzigo unauza mwenyewe.

2. Option 2, Tumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, WhatsApp na Twitter.
Ukipata mteja ndio utume mzigo.
 
Office sio lazima kupanga frem mkuu!! Anaweza kuwa na meza sehemu ila akaboresha muonekano wa iyo meza... Na kwa dar location zipo nyingi ni yeye mwenyewe kujipanga
Kumbuka ndo anaanza biashara
Biashara yenyewe dagaa wa kukaanga
Asifungue ofisi kwanza mpaka apate mzunguko mzuri wa biashara asijepoteza hela ya kodi bure

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bei ya ndoo Ni 40,000. Kama vipi nikupe hookup na jamaa,

Lakini SI uzame mwenyewe kisiwani,unanunua dagaa wabichi toka kwa wavuvi,unakaangaa na kuja nao town tayari kwa kusafirisha
 
Hilo nimewaza mkuu ngoja niendelee na utafiti kama ulivyonishauri nijue na gharama za mafuta pia. Thanks
 
Hilo nimewaza mkuu ngoja niendelee na utafiti kama ulivyonishauri nijue na gharama za mafuta pia. Thanks
 
Bei ya ndoo Ni 40,000,,Kama vipi nikupe hookup na jamaa,
Lakini SI uzame mwenyewe kisiwani,unanunua dagaa wabichi toka kwa wavuvi,unakaangaa na kuja nao town tayari kwa kusafirisha
Dah kumbe mkuu, vp kisiwani unamaanisha ukerewe? hiyo elf 40 wanakua wabichi sio ama wameshakaangwa? Naomba unijibu mkuu usichoke.
 
Ahsante
Jaribu kufanya haya.

1. Njoo Dar, Nenda soko lolote kodi meza then ukiagiza mzigo unauza mwenyewe.

2. Option 2, Tumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, WhatsApp na Twitter.
Ukipata mteja ndio utume mzigo.
sana mkuu🙏🏿
 
Ahsante sana mkuu nitamtafuta🙏🏿
 
Dah kumbe mkuu, vp kisiwani unamaanisha ukerewe? hiyo elf 40 wanakua wabichi sio ama wameshakaangwa? Naomba unijibu mkuu usichoke.
Yes ukerewe,lakini ukerewe Ni mjini,viko visiwa vingine arround,
Yes dagaa wamekaangwa tayari 40,000 Hapo kirumba mwaloni
 
It s
Jaribu kufanya haya.

1. Njoo Dar, Nenda soko lolote kodi meza then ukiagiza mzigo unauza mwenyewe.

2. Option 2, Tumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, WhatsApp na Twitter.
Ukipata mteja ndio utume mzigo.
Ahsante mkuu nitazifanyia utafiti izo options zote mbele nijue inanifaa ipi.
 
Dah kumbe mkuu, vp kisiwani unamaanisha ukerewe? hiyo elf 40 wanakua wabichi sio ama wameshakaangwa? Naomba unijibu mkuu usichoke.
Advantage ya kwenda visiwani,,ndoo dagaa wabichi utanunua chini ya 10,000,,then unatafuta mmama anakukaangia,unabeba mzigo kuja town
 
Yes ukerewe,lakini ukerewe Ni mjini,viko visiwa vingine arround,
Yes dagaa wamekaangwa tayari 40,000 Hapo kirumba mwaloni
Ahaaa kumbe nikienda mwenyewe visiwani nikaandaa mwenyewe dagaa naweza kutumia gharama ya chini zaidi ya elf 40 sio. Ngoja nijipange mkuu lazima niende. Thanks
 
Advantage ya kwenda visiwani,,ndoo dagaa wabichi utanunua chini ya 10,000,,then unatafuta mmama anakukaangia,unabeba mzigo kuja town
😳😳😳😳 mkuu kumbe huku mjini ilikua nipigwe kinoma yani eti ndoo elf 70 mwisho 65 . Ngoja nijipange niende, vp gharama za usafiri kuanzia mzigo namimi mwenyewe?
 
USHAURI: KAMA HUJUI PA KUANZIA USITEGEMEE FAIDA YA HARAKA

Habari ndugu. Hongera sana kuingia katika ujasiriamali. Hakuna tatizo kusoma vitabu sababu unaongeza elimu. Ila ukweli nikuambie kwamba waandishi wa hivyo vitabu wako kimaslahi zaidi. Huyo mwandishi wa hicho kitabu Kiyosaki anaitwa, yeye kampuni yake inayotoa hivyo vitabu ilifilisika na hadi aka-file bankruptcy. Sasa jiulize mtu anayeshauri vizuri anafilisikaje kama sio uongo tu kaandika.

Kiukweli kujua biashara ni kuifanya. Na utakapoifanya ndio utajifunza. Umetaka faida, napenda kukupa habari mbaya kwamba usitegemee faida hadi baadaye sana kwa hio biashara sababu umeshasema hauna soko na haujui pa kuanzia. Manake utafanya makosa mengi kwanza ya kujifunza ambayo yataleta hasara hadi ukipata mfumo mzuri ndio utapata faida. Kwa hio kama lengo ni faida sasa hivi, tafuta biashara unayoijua vizuri sana, na ambayo tayari una wateja ndio uanze nayo hio. Manake tafuta wateja kwanza kabla ya kuanza. Kama ni dar, usinunue bidhaa tafuta wateja wa uhakika kabisa kabis, ndio upeleke bidhaa upate hela yako. Hongera tena. Ujasiriamali ni mzuri sana, lakini mwanzo una changamoto nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…