HABARI ZENU WAKUU
Ni Muda WA Miezi Mitano sasa Toka nihitimu Chuo pale Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino (Mwanza) Tawi kuu. Namshukru Mungu nkapata Degree yangu ya Kwanza ya Falsafa na Elimu , lakini kwa kipindi chote hicho mpaka Sasa hivi nafanya Temporary work kwa Rafiki yang kipenzi (Boss Fulani) mmiliki WA Magari kadhaa ya mizigo na Mnunuzi WA Tani za Dagaa kutoka mikoa ya Mara na Mwanza.
Kiukweli Nje ya Business ya Magari ya Mizigo ( Semi - Trailers) especially Scania R 420 , 114 n.k Jamaa hyu Business ya Dagaa inamlipa Sana kuliko Magari na PIA sisi kama wasimamizi wake Maisha yanaenda japo kazi Ni Ngumu ILA masilahi yapo .
Biashara hii Dagaa hufanywa kwa kuchukua Dagaa kutoka huku na kupelekwa Dar , Congo,Tunduma, Arusha na kwingineko Na inalipa Sana ukizingatia yafuatayo, Mtaji,Soko,Muda WA kusimamia na juhudi na watu (Social capital), n.k
Mimi kesho na kesho na kesho ntaka Nijipange na nianze Mdogo mdogo
Karibuni Musoma karibuni Kwenye Dagaa. Tafadhali Mchanganuo kama ifuatavo ; Dagaa inayonunulia Ni Dagaa chafu (Chakula ya kuku) na Dagaa safi Chakula ya Binadam
1. Chakula ya kuku Inauzwa kwa Dumu Yan ndoo ya Litre 20 , Mara nyingi dagaa hii ya Chakula ya kuku huuzwa kwa Tsh. Elfu 10,000/= mpaka Elfu sita na Mia Tano kwa Kama Dagaa imepatikana nyingi Sana bei yake hususha Automatically Kwan kwenye Masoko Hufurika Sana.
Uandaaji Chakula ya kuku huandaliwa kwa kuwekwa kwenye Gunia kubwa ambapo Kila gunia hubeba Dumu 21 na @ Gunia likipimwa hutoa kilo kuanzia 120- 95.
Usafiri Baada ya kuandaliwa na kuwa tyr hupakiwa kwenye Magari ya mizigo na kupelekwa Kwenye Masoko kama vile Dar, Congo,Tunduma, Arusha n.k . bei ya Usafiri Inategemea Mzigo Wako na PIA Maelewano na Mwenye Gari lakini kama Semi- Trailer lenye Contena Kama vile Scania R420 Mara nyingi hubeba Gunia 270 na hapo hutegemea upakiaji WA Makuli husika Na bei hapa Kwa Gari huwa Ni one million and point six 16000,000/=.
Bei kiwandani dagaa hizi huuzwa kwa kilo ambapo
Kilo Ni 3500- 2500 Inategemea Upatikanaji WA Bidhaa na Kiwanda husika.
Kwa hyo gunia Lenye Dumu 21, Na lenye Thamani ya Tsh. 210000= na Gharama ya 25000 Uaandaji usafiri , ushuru na Mengineyo na lenye kilo 120 Ambapo @ kilo 3500- 2500 .
Hapo ukipiga Hesabu utakuta kwamba Ni
120*3500= 420000
420000- 235000= 185000
Au 95*2500= 237500 Kama Dagaa umeinunua kwa bei nzuri na umebana Mapato saswa Sawa. Masoko kwa Dar ndo habari yake Kwan ndo Viwanda vingi vya Chakula ya kuku hupatikana Hasa kwa Falcon, Kitunda kwa Matinde few to mention just Na hapa kwenye vizuri kufatilia mwenyewe kuepusha madalali na matapeli WA mujini , Nakaribisha Kitu Maswali, Matusi,Kejeli na Mengineyo Mchana Mwema