Laki tano inatosha kwa kuanzia,itakuwa taratibu kama utakuwa na nidhamu ya fedha.,usilete kwanza mikoani...we we nenda kisiwa goziba,au kimoyomoyo,mlumo,ghana,ukawe unanunua dagaa wabichi unawaanika huko huko wakikauka unauzia huko huko mpaka mtaji utakapokuwa mkubwa kuweza kusafirisha mikoani,
AU huko huko visiwani nunua then safirisha uje uuzie kirumba mwaloni...usihangaike kupeleka mikoani...
Sina uchoyo na wazo la biashara kumsaidia mtu yoyoye.
Mwingine anayehitaji ushauri zaidi wa biashara ya kufanya sema hapa nitakupa cha kufanya ili mradi tu uwe na ule msukumo ndani ya moyo wako kufanya biashara bila kutafuta sababu.