Biashara ya dagaa

Biashara ya dagaa

Mkuu kwa mfano ukanunua dagaa kisha ukahifadhi mpaka wakati ambao dagaa wanaadimika kutokana na changamoto ya hali ya hewa si unaweza kuuza kwa bei nzuri zaidi?
mkuu kisiwa cha GOZIBA ushafika? Nimeshauriwa nitulie mpaka mvua zikate kwanza kwasababu sasa hivi bei ya dagaa ipo juu itanisumbua kupata mteja sokoni hii ni kweli mkuu?
 
Mkuu kwa mfano ukanunua dagaa kisha ukahifadhi mpaka wakati ambao dagaa wanaadimika kutokana na changamoto ya hali ya hewa si unaweza kuuza kwa bei nzuri zaidi?
Dagaa haitunziki kwa muda mrefu,, ikiwa hivyo inapoteza ubora na kuwa nyekundu.
 
🤣🤣 Dah! Biashara huwa changamoto kweli yani lazima ujitoe kaka, ku compete na watu wanaoleta mzigo mkubwa kwa pamoja sokoni sio rahisi, na kasumba mbaya ni ile ya wafanya biashara kutaka uwaachie mzigo alafu wakulipe baada ya kuanza kuuza, Nakushauri uende kijijini tafuta mzigo quality, njoo nao kidogo alafu uza bei nafuu hata kama hutapata faida, wakishakujua maramoja leta mzigo mkubwa zaidi. Kuhusu soko angalia mzunguko wa general tu usitafute wateja kama huna dagaa mkononi
Unaweza kunichek inbox au uweke namba yako hapa, Maana nimefanya hiyo biashara kidogo angalau
 
Nina mtaji wa kama 1m nimefikiria nianzishe biashara hasa ya dagaa hasa za nwanza zisizo na mchanga

Nahitaji msaada wenu hasa
*Bei ya ndoo na inakuwa kilo ngapi
*Bei ya gunia na linakuwa na kilo ngapi
*Chimbo la kuuzia kwa jumla na rejareja
*n.k hasa kwa wazoefu

Kambi popote
kua makini usijaribu kwenda eneo la kukusanyia mzigo' huku bado haujafanya taratibu za vibali, ushuru na leseni ya biashara ' utakuja kujuta mimi hadi leo nalia na mwenyeji wangu' nilienda kimoyomoyo"
 
Yah umemshauri vyema mkuu..kabla ya kwenda sehemu ya kukusanya mzigo ahakikishe ameweka mpango vizuri wa leseni ya ku deal na biashara ya Dagaa.

Maana bila hivyo,, hataweza kuusafirisha mzigo wake.

KIMOYOMOYO napapata vyema mkuu.
 
Back
Top Bottom