Vyombo vya moto ni shida, mimi pia nimejaribu noah na suzuki carry ni shida.
Pesa yako ni nyingi bro, kwanza sikushauri trekta, wekeza katika biashara ambayo utaanza na pesa ndogo kisha kadri inavotiki unaiongezea pesa
Yan usiweke mayai yote katika kikapu kimoja na usipime kina cha maji kwa miguu yote miwili.
Mimi nakushauri, fanya utafiti mikoa flani flani ujue udhaifu huko kisha wekeza ktk viwanda vidogo vya usindikaji/ uzalishaji
Kwa mf. Kuna mtu alianza iyo kitu kwa mtaji usiozid mil 6
Alinunua mashine ya kusaga, akawa anasaga unga anapaki, anaenda kuuza maeneo yasio na ushindani, eneo alilokuwepo tu watu walikuwa wananunua, akaongeza akawa anapaki na mchele.
Mdo mdo, to shorten a story yupo mbali sana, siku izi mashine yake anapaki mchele katika magunia pia, no nembo, yanaingia dar