Biashara ya dala dala au costa

Biashara ya dala dala au costa

OME123

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
1,497
Reaction score
605
Wana jf nina mtaji wa milion 47 sasa nataka ninunue costa moja au haice 4 au noha.ambapo nimepiga mahesabu kuwa baada ya miaka miwili ntakuwa nimerudisha mtaji wangu.kma kwa siku nategemea kupata 120 000 kwa mwezi 3600 000.je wenye uzoefu na biashara hii naombeni ushauri
 
Aisee sikushauri daladala kaka,
ninafanya hiyo kitu ni Pasau kichwa. Hakunaga Dereva au Konda mwaminifu hata mmoja,

Hiyo 120,000 kwa siku utaipata kwa kipindi kisichofika mwaka mmoja.

Baada ya hapo utaanza kupewa sound za kufa mtu. Yaani niko na Coaster 2 na Hiace 3 lakini amini nakuambia sometimes home nakosa hata 50 ya akiba,
 
Tushauriane sasa mkuu may be biashara gani mkuu coz shughuli zangu.niko tyt sana nakosa muda.coz kila siku saa moja kurudi napo saa moja.so nilidhani usimamizi wa hiace au coaster itakuwa ni rahisi kusimamia mkuu
 
Mwanajamvi temana ama achana kabisa na iyo biashara. Kwani daladala ikipata ajali utaambiwa ni wewe umetoa kafara hata ukijiteteaje yani wabongo nakushaur tafuta trekta ujishughulishe na kilimo.
 
Milion 47m inaweza nununua treckta
 
Biashara ya Trekta nami naifanya pia. Ila Mimi hii biashara nimebugi sehemu mbili anbazo ukiifanya nawe uwe makini usibugi kama Mimi.

Kwanza Trekta nililinunua Jipya kabisa, tena Massey Ferguson ila halikua la Original from UK, Bali under license from Pakistan, yanauzwa Sinza Mori kama waelekea Meeda Bar upande wa kushoto. Ni heri ningenunua Used but original from UK kuliko Mpya but under licensed.

Pili location ya biashara. Mimi nalima Ufuta Lindi, hivyo nalo nililipeleka Lindi. Kule kilimo ni Ufuta tu Mwishoni mwa Mwaka hivyo sehemu kubwa ya mwaka linakaa idle, mzunguko wa hela unakua mdogo. Linabebaga korosho sometimes but kwa trailer ya kukodisha. Hivyo ili uione faida nakushauri uliweke sehemu ambapo wanalima mwaka Mzima. Faida ingine ya eneo hili ni kua ardhi sio ngumu sana hivyo trekta haiumii.

Lakini kwa ushauri zaidi sio lazima utumie zote 47mil ziishe sasa, waweza pia kufuga kama alivyosema mdau hapo juu, kilimo cha mboga mboga na pia kuwekeza Nyingine kidogo hata kwenye kilimo cha miti.

Ila daladala, SIKUSHAURI aisee from vivid experience niliyo nayo sasa!!
 
Daladala utapata presha. ..ukiona simu ya dereva tu we presha. ...mi nimepaki langu baada ya kuibiwa sanaaa, maana wanaiba mpk spare. .wanabadilisha kizima unawekewa kibovu
 
Vyombo vya moto ni shida, mimi pia nimejaribu noah na suzuki carry ni shida.

Pesa yako ni nyingi bro, kwanza sikushauri trekta, wekeza katika biashara ambayo utaanza na pesa ndogo kisha kadri inavotiki unaiongezea pesa

Yan usiweke mayai yote katika kikapu kimoja na usipime kina cha maji kwa miguu yote miwili.

Mimi nakushauri, fanya utafiti mikoa flani flani ujue udhaifu huko kisha wekeza ktk viwanda vidogo vya usindikaji/ uzalishaji

Kwa mf. Kuna mtu alianza iyo kitu kwa mtaji usiozid mil 6

Alinunua mashine ya kusaga, akawa anasaga unga anapaki, anaenda kuuza maeneo yasio na ushindani, eneo alilokuwepo tu watu walikuwa wananunua, akaongeza akawa anapaki na mchele.

Mdo mdo, to shorten a story yupo mbali sana, siku izi mashine yake anapaki mchele katika magunia pia, no nembo, yanaingia dar
 
kwa maoni yote naona ni mema world has change uaminifu wa wewe uwe bize na issue ingine na wengine wakufanyie kazi inaletashida kidogo! nunua ardhi kubwa hata heka 60 pembeni ya jijini itengeneze docs halali ipangie miundombinu barabara au mitaa anzisha nyumba 1 hapo then wait! huku kuwa bize na mambo yako!
 
SOLUTION ! ! SULUHU ! !SOLUTION ! ! SULUHU ! !SOLUTION ! ! SULUHU ! ! La maana fanya uchunguzi ni eneo lipi lina capital gain kubwa kuliko yote kwa bei hiyo hiyo
 
Omunga, hakuna Jambo Zuri Kwenye biashara Kama to have a proper knowledge of what you want to do, research, knowledge and understanding the client, inakuweka katika low risk to loose, if you don't try, then you have done nothing, do what you can do, the rest will come within and it's a better chance to learn something new.

Your passion is your profession Mkuu
 
Nakubaliana na Shakir...daladala ina changamoto sana. Kwa mjini ndo balaa. Gari moja nimebahatika kupata dereva mzuri sana, mwingine pasua kichwa.

Kwa route za kijijini kwenda kurudi inalipa kidogo na gari haichoki haraka.
Mwisho wa siku kila biashara ni ngumu inahitaji kujitoa kweli na vile huna muda wa kutosha changamoto yake ni maradufu.
 
Last edited by a moderator:
Huku kuwa bachelor napo issue sana.sasa nafikiria ningekuwa na msaidizi wa karibu ningefungua duka la open shoes na shoes za kila aina kutoka itally nayo naona km ingeweza kunilipa kwa mazingira niliopo.yaan kwa kweli inahitajika kutulia na kufikiria kwa kina sana wana JF
 
Wana jf nina mtaji wa milion 47 sasa nataka ninunue costa moja au haice 4 au noha.ambapo nimepiga mahesabu kuwa baada ya miaka miwili ntakuwa nimerudisha mtaji wangu.kma kwa siku nategemea kupata 120 000 kwa mwezi 3600 000.je wenye uzoefu na biashara hii naombeni ushauri

Mkuu nakushauri uje Iringa uwekeze kwenye ardhi kwa kupanda miti ya mbao ambayo ni very profitable kwani kama unavyojua mbao zina dili sana,ekari moja kununua ni 150,000.nakuapia hutajutia kwa uamuzi wako mkuu coz haikupotezei muda wa usimamizi na hauibiwi.ukiona umevutiwa zaidi na hili wazo waweza kuni pm nikupe maelezo mengine zaidi
 
Back
Top Bottom