Biashara ya dawa za kulevya kurejea kwa kasi? Watanzania 2 wakamatwa na Cocaine kilo 2 tumboni Uwanja wa ndege wa Mumbai

Kwa kweli sijaelewa hapa..
Yaani walikuwa wanapeleka barafu kwa eskimos?
 
Hawa watu hua wanaangalia Soko au huenda India ilikua ni Gateway tu.
Duuh... hiyo route itakuwa wenge sana
Miaka ya 80s na 90s, waliokuwa wanaitwa wazungu wa unga, walikuwa wanaenda India kumeza hizi halafu wanaleta Bongo
Kweli muda umeenda sasa imekuwa ni kinyume, basi Bongo imekuwa Drug Hub kama
 
Sukuma Gang wanajaribu kumdiscredit Mama S
 




Nikwamba Vijana hao mnaowaona kwenye HIYO picha Hapo chini wakiwa kwenye ndege Ya Ethiopia wanaitwa Mtwanzi Carlos Adam na Rashid Paul Sayula.

Inasemekana vijana Hawa waliondoka Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa Dar es Salamu Mwl. Julius NYERERE mwezi huu wa April Tarehe 22, 2021 walielekea Mumbai India kupitia Adis Ababa.

Waliondoka nchini wakiwa na viza ya matibabu.

Walipofika Mumbai walitiliwa shaka na kikosi Cha madawa ya KULEVYA Cha India wakawaweka chini ya ULINZI na walipofika hospitali kwa uchunguzi zaidi, walipigwa x-ray nakuonekana wana pipi za cocaine ndani ya matumbo yao.

Walishikiliwa kwa siku 6 toka Tarehe 22 April MPAKA Tarehe 28 chini polisi na vikosi MBALIMBALI vya kiusalama vya India na Baadae walianza kunya pipi HIZO.

Walikunya jumla ya Pipi 151, Rashid alikunya pipi 97 na Mtwanzi nae alikunya 54 zotte zikiwa zenye UZITO wa kilo 2 na gramu 225.

Kwasasa bado wako mahabusu za huko.

Ninawapa taarifa hii ili mjue KAZI yao imeshaanza upya baada ya kufa mnoko.

Chakushangaza zaidi wamepitia uwanja wa ndege huu uliokuwa na ULINZI mkali kabla mnoko hajafa.

Tuliambiwa wafanyabiashara warudi na kuja kuendeleza biashara zao, japo hatukuanbiwa ni biashara zipi?

Wkt huu tukifurahia kuwakamata wa Iran 7 tujue na India WANAFURAHI kuwakamata watanzania 2.


Chanzo ni vyombo vya habari vya India nendeni mka Google mtakutana nayo.
 

Hawa watakuwa walilenga mtafaruku wa kimbembe cha haka ka mafua kuwa ni uchochoro wao wa kutosha.
 
walipenyaje pale JK Nyerere? Hii biashara ngumu sana, tukubaliane kuwa TANZANIA ni border zuri! Hao ndio tuwasahau kabisa na wamekiri.
 
Uhalifu hauwezi kuisha kabisa ila kuna namna ya kupunguza, kipindi cha jei kei wa Tanzania tulikuwa tuna vyumba vyetu maalum vya ukaguzi tunapofika viwanja vya Ndege kwani nchi ilikuwa ni transit...
Naunga mkono hoja. Kuna coordinated effort ama payroll kabisa. Viza za kwenda India walizipataje, Airport mpya yenye vifaa vya kisasa na trained staff jamaa wamepitaje. Hapa lazima kulikuwa na lubricating grease ya kulainisha mikono ya watendaji.

Drug Business its a lucrative and fast paying one haiwezi kuisha haswa kukiwa na mikono ya watawala.
 
walipenyaje pale JK Nyerere? Hii biashara ngumu sana, tukubaliane kuwa TANZANIA ni border zuri! Hao ndio tuwasahau kabisa na wamekiri.
Safari waliyokuwa wanakwenda/nchi
Dhumuni la Safari yao pia,matibabu
Hapo sasa ukiangalia!lazima watakuwa
Walitengeneza mchongo waonekane
Wanakwenda kwenye matibabu,docmnts etc

Kumbuka hawa walimeza na ukimeza kuna asilimia kubwa ya mtu kupita nayo kama uwanjani hakuna xray machine au yawezekana watu walishindwa wahisi kama wana midude mwilini
Sasa kukamatwa kwao inawezekana ilisababishwa na mambo kadhaa,inawezekana walipofika Addis walihisiwa kutokana na mienendo yao
Wakiwa safari/ndani ya ndege au la
Kwa wenzetu ukihisi nchi husika pale wanatuma fax tu za information zako
We ukifika mwisho wa Safari unawekwa chemba,wanakukagua wanakupiga massage
Inawezekana hawa wagonjwa walihisiwa eidha kutoka bongo, au Addis watu walishatuma fax huko india,we unasubiriwa

Ova
 
Dah! [emoji28],wewe unaishi shimoni kiasi kwamba ushindwe kuona kinachoendelea ndani ya jamii mpaka usubili vyombo vya habari[emoji28].Nonsense
Ninachokiandika ndio uhalisia hata jiwe alipokuwepo bado hizi biashara ziliendelea,ss sijui huko zilipopungua ni wap au Nanjilinji Lindi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…