Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali lako limeegemea kikuda zaidi kuliko kuiangalia fursa iliyopo.wakuu habarini za muda huu. Naomba kujua mwenye uzoefu wa hii biashara ya shule ya chekechea na day care anipe muongozo.
Naombeni kujua ni vigezo gani vinahitajika na mfumo wake wa elimu ukoje maana nimekaa arusha miaka miwili sasa lakini kila kukicha unakuta makaratasi njiani kila mahali ni day care na chekechea.
Je, hizi shule zimesajiliwa? na je zinalipa kodi? nauliza hivi kwakuwa hii biashara imeibuka kwa kasi ya ajabukwakuwa kuna moja nilikuta juzi maeneo ya sanawari wanachukua watoto kwa shilingi elfu kumi kwa mwezi huku wakisambaza vipeperushi na kuwaambia wananchi kwamba watoto watakuwa wanapata chakula bure kwakuwa mfadhili wao ni mzungu hivyo atawahudumia kwa mahitaji yote.
Hoja yangu kubwa ni kutaka kujua hawa wazungu wafadhili wanaosema watatulishia watoto bure Je wao wanapata nini kutoka kwetu?
Je, Serikali yetu inafuatilia kwa karibu hawa wazungu wafadhili wanaokuja kujificha kwenye vituo vya yatima na day care na chekechea kama kweli nia yao ni msaada au kuna biashara nyingine imejificha kwa undani? Na je TRA wanakusanya kodi zao au wanawaacha tu kwakuwa ni msaada?
Pia day care zingine na chekechea zina wafanyakazi wa nje ya nchi kama wazimbabwe, waganda na wakenya sasa vipi kuhusu vibali vya ajira kwa raia wa kigeni Uhamiaji wanawafuatilia watu wote wanaomiliki hizi day care na chekechea? Kwakuwa nyingi zimekuwa kichaka cha kuficha wahamiaji haramu na biashara zingine za ajabu.
Huwezi kusema unawasaidia wazazi wasiojiweza bila kuwa wazi kwamba wewe mfadhili unapata nini kutoka kwenye nchi yetu hii ya tanzania.
Kibaya zaidi wengine wameenda mbali kwa kukodisha nyumba mitaani na kufungua mashule. Nisaidieni kunielewesha kwamba ukitaka kufungua shule ni vigezo gani unatakiwa kuwa navyo na hizo day care ni masharti gani yanahitajika?.
Nawasilisha mada.
Si kweli tatizo ni wasichana wa kazi hawana uwezo wa kutunza watoto vizuri, hasa kwa parents ambao kuondoka ni asubuhi kurudi ni usiku. Sasa hizi day care ukipata za uhakika ni msaada mkubwa kwa kukaa na watoto, huku wakipata elimu, michezo na kuichanganya na wenzao.uzungu mwingi