Biashara ya Day Care na shule za chekechea Arusha zimeshamiri kulikoni?

Maisha magumu sana, sasa hv mzazi unachagua usiende kazini then ukae na mtoto nyumbani au utafute dada amuachie mtoto nyumbani au umpeleke mtoto kwenye vituo vya kulea watoto (day care)
mwisho wa siku unaona ni bora umpeleke kwenye day care mana kule atapata muda mwingi kukaa na wenzake, kufanya michezo yao, kujifunza mambo mbalimbali, kuzoea mazingira ya kuishi na wengine. Hii ni tofauti na kama ukimuacha mtoto na dada wa kazi mana kuna mambo kama mtoto atakosa.
 
Siku hizi wadada wa kazi ni changamoto sana.zamani ilikuwa rahisi kuwapata kwani walikuwa hawaendi wengi sekondari kama sasa hivi.Lakini kwa sasa unakuta darasa zima wanachaguliwa kwenda sekondari mpaka vijijini huko na wanaobaki kidogo hawana wito na hizo kazi.
 
Daycare zimekuwa nyingi sana. Hakuna mtu wa kulea mtoto Mchana na kila mtu yupo bize na kazi na dada wa kazi ni majanga sana. Daycare zipo nyingi Dar,Arusha, Mwanza na Dodoma.
 
Swali lako limeegemea kikuda zaidi kuliko kuiangalia fursa iliyopo.

Demand ya hivyo vituo ni kubwa na kila mzazi anapeleka mtoto pale ana uwezo napo.

Haiingii akili mtoto under 5 years aanze kutafuna mamilioni kwenda day care, hawahawa wa mitaani wa 30,000/= kwa mwezi au 50,000/= wanatosha.
 
Side effects za jiwe kuwaambia fyatueni watoto wengi ndio zinaanza kuonekana sasa hivi.
Watu wamezaa kwelikweli halafu kulea watoto wao wanashindwa,
Wanakuja wafadhili kuwasaidia kulisha watoto wenu badala mshukuru mnataka hao wafadhili walipishwe makodi ya hovyohovyo.
Kweli mbongo ni sawa na gunia la msumari ukilibeba linakuchoma mgongoni.
 
Changamoto za wadada

Badala ya kukuta mtoto anajua miziki mipya kukata viuno na movie zote za kinigeria bora aende day care

Au hawa wadada ambao anaweza fungia mtoto ndani akasepa heri akashinde huko
 
uzungu mwingi
Si kweli tatizo ni wasichana wa kazi hawana uwezo wa kutunza watoto vizuri, hasa kwa parents ambao kuondoka ni asubuhi kurudi ni usiku. Sasa hizi day care ukipata za uhakika ni msaada mkubwa kwa kukaa na watoto, huku wakipata elimu, michezo na kuichanganya na wenzao.
 
Mlevi mmoja alisikika akisema dawa ni Katiba Mpya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…