Hii ni unataka kuwa mchuuzi wa unprocessed gold au processed, kama ni unprocessed inakubidi uanzie machimbo/migodi ya wachimbaji wadogo ambapo unatakiwa uwe na mwalo na crusher(karasha),ambapo wachimbaji wadogo wanakuwa wakisaga mawe yao hapo mwaloni kwako ,wanaoshea na kupembulia hapohapo kwako so faida yako inakuwa ni ile pile(lundo),na ukiwa na scale(mzani) kuna watakokuuzia hapohapo baada ya kupembua wengine wataenda kuuza wanakojua wao.
Na kama unataka kuwa mchuuzi wa processed gold hapa itakulazimu kuwa leseni kutoka ofisi ya madini mkoa usika, ambapo utakuwa na ofisi yako hapo soko la dhahabu ukisubiri wachuuzi wadogo kutoka "mialoni" wanaokuja kuuza hapo sokoni. Hapa inatakiwa pia uwe na scale ya kupimia uzani(grams) na purity ya dhahabu utakayoletewa. Bei ya dhahabu hutofautiana kutokana na purity yake. Kuna dhahabu inakuwa na uchafu (sanasana copper na madini mengine),so kulingana na purity kiasilimia 70%,80%,90% ndo itatathmini ununue kwa bei gani kulingana na soko la dunia, japokuwa hapa nchini bei elekezi inacheza around 140,000 kwa gram 1 ukiwa soko la dhahabu. Lakini bei inakuwa nafuu ukienda pori ( machimbo ya wachimbaji wadogo)
kumbuka pia bei ina fluctuate.