Biashara ya Dhahabu

Biashara ya Dhahabu

Bwenyenye254

Member
Joined
Mar 13, 2021
Posts
52
Reaction score
85
Kwa wadau wote wa biashara ya dhahabu, hasa wale waliobobea katika ununuzi na uuzaji wa dhahabu kwa wingi (Broker na Dealer). Nimekuwa nikifikiria kuanzisha biashara ya ununuzi wa dhahabu hapa Tanzania, na ningependa kusikia ushauri wenu.

Nina bajeti ya takriban shilingi milioni 400 hadi 500 za Kitanzania, na lengo langu kuu ni kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo kwa kiasi kikubwa kila siku.

Nimewei kufanya biashara hii katika nchi zingine ambazo si Tanzania.

Nimefikiria kutumia karasha na mialo kama njia ya kuvutia wachimbaji wadogo wafanye biashara nami. Yeyote atakaye tumia karasha zangu pia atakuwa mteja wangu. Maeneo niliyoangazia zaidi ni Geita, Kahama, na Chunya.
Kwa hivyo budget yangu itatumika kwenye establishing mtandao wa karasha na mialo na pia ununuzi wa dhahabu.

Ningependa kujua kutoka kwenu:
  • Mbinu bora za kujenga uaminifu na mtandao imara wa wachimbaji wadogo.
  • Nini changamoto kuu ambazo ninapaswa kuzingatia katika biashara hii hapa Tanzania?

Nimewahi kufanya biashara hii katika nchi nyingine. Tanzania ina changamoto na fursa zake. Naomba mchango wenu wote ili niweze kuelewa vizuri mazingira ya biashara hii nchini Tanzania.
Ikumbukwe kwamba niitafanya biashara yangu kwa kufuata taratibu na sheria zote za Tanzania.
Karibu kwenye mazungumzo.
 
Ili upate mzigo kwa uharaka inabidi udhamini wachimbaji wadogo ili wakuletee mali. Lakin pia unatakiwa kuwa na subira mana wengine ukishawapa hela hawarudi kabisa na wana kutia loss

Njia nyingine pitia katika migao ya mawe huko kutana na wanao jua mawe mazuri ya dhahabu ili upeleke kwenyewe kwenye mwalo wako.

Dhahabu inataka wadau sana la sivyo unaweza kuwa broker sehemu na watu wasilete mali kwako
 
Tatizo jf siku hizi imekuwa shamba la bibi,,,, mtu unaweza kukaa chini ukajitungia kitu ukakileta hapa watu wakaumiza kichwa kutiririka maujanja na mawazo kumbe chai ! Non sense,,,,

Na mtu unaweza kuwa na jambo serious kweli unahitaji kujua ABC zake lakini watu wakafanya mizaha wakidhani ni Chai vile vile ,,,,, !

Anyway, swali langu ni , je kama unazoefu na hii biashara nchi nyingine mbona maswali yako yamekaa kama hujawahi kabisa kujihusisha na hiki kitu ? Alamsiki
 
Mkuu Hongera.
Your reasoning capacity ni nzuri sana....mzoefu kauliza vipi hayo maswali?
 
Kuna fursa nyingine pia njoo inbox nikupe ujanja ,kama itakupendeza ukiona haifai pia sawa Kila la kheri
 
Tatizo jf siku hizi imekuwa shamba la bibi,,,, mtu unaweza kukaa chini ukajitungia kitu ukakileta hapa watu wakaumiza kichwa kutiririka maujanja na mawazo kumbe chai ! Non sense,,,,

Na mtu unaweza kuwa na jambo serious kweli unahitaji kujua ABC zake lakini watu wakafanya mizaha wakidhani ni Chai vile vile ,,,,, !

Anyway, swali langu ni , je kama unazoefu na hii biashara nchi nyingine mbona maswali yako yamekaa kama hujawahi kabisa kujihusisha na hiki kitu ? Alamsiki
They were not informal markets like in Tanzania. Hope that answers your question
 
Hi! Guys
Nje ya mada kidogo.
Kuna task nimepewa, naomba kuuliza kuhusiana na vifaa vya uchimbaji wa dhahabu.
1.Cyclone ni nini nainafanya kazi gani migodini?
2. Air compressor ya piston 3 na 4 zina uwezo wa kutoa upepo wa bar ngapi kila moja?
3. Ball mill ya tani 3 kwa saa ni bora kuagiza za kichina au kuchonga sido?
4. Pia blower ya 35kw ni bora kuagiza au kuchonga sido?
 
Back
Top Bottom