Bwenyenye254
Member
- Mar 13, 2021
- 52
- 85
Kwa wadau wote wa biashara ya dhahabu, hasa wale waliobobea katika ununuzi na uuzaji wa dhahabu kwa wingi (Broker na Dealer). Nimekuwa nikifikiria kuanzisha biashara ya ununuzi wa dhahabu hapa Tanzania, na ningependa kusikia ushauri wenu.
Nina bajeti ya takriban shilingi milioni 400 hadi 500 za Kitanzania, na lengo langu kuu ni kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo kwa kiasi kikubwa kila siku.
Nimewei kufanya biashara hii katika nchi zingine ambazo si Tanzania.
Nimefikiria kutumia karasha na mialo kama njia ya kuvutia wachimbaji wadogo wafanye biashara nami. Yeyote atakaye tumia karasha zangu pia atakuwa mteja wangu. Maeneo niliyoangazia zaidi ni Geita, Kahama, na Chunya.
Kwa hivyo budget yangu itatumika kwenye establishing mtandao wa karasha na mialo na pia ununuzi wa dhahabu.
Ningependa kujua kutoka kwenu:
Nimewahi kufanya biashara hii katika nchi nyingine. Tanzania ina changamoto na fursa zake. Naomba mchango wenu wote ili niweze kuelewa vizuri mazingira ya biashara hii nchini Tanzania.
Ikumbukwe kwamba niitafanya biashara yangu kwa kufuata taratibu na sheria zote za Tanzania.
Karibu kwenye mazungumzo.

- Mbinu bora za kujenga uaminifu na mtandao imara wa wachimbaji wadogo.
- Nini changamoto kuu ambazo ninapaswa kuzingatia katika biashara hii hapa Tanzania?