Biashara ya duka la rejareja siyo ya kudharau hata kidogo. Inatunza familia kabisa na kusaidia kugharamia baadhi ya matumizi kwenye familia. Watu wengi waliotanguliaga kuifanya hii biashara wako mbali saaana, wenmgine wamejenga na kumudu hadi nyumba 'ndogo nyumba' kwa retail shop.
Wengi wameshaongea mengi mazuri kwenye kurasa zilizopita, na mimi sababu ni mzoefu kiduchu, wacha pia nitoe mawili matatu ambayo sijaona yakiorodheshwa hapa, huenda watu wanafanya katika maduka yao au hawafanyi, kama hufanyi unaweza tendea kazi.
USIACHIE FURSA.,,,,Kamwe usiuze 'HAKUNA'
Kitu kikubwa katika maduka ya rejareja ni kuhudmia hitaji la kila mmoja kadri uwezavyo. Kamwe usiuze hakuna ikiwa inawezekana icho kitu/bidhaa inaweza kuuzika katika duka lako. Hata kama mhitaji ni mmoja, mletee anachotaka. Ili mradi kile anachohitaji kipo kwenye uwezo wako na unaridhia kuuzika kwako.
Biashara ya vilevi na sigara.
Siagara, Angalia eneo lako la biashara kama kuna watu wanahitaji sigara wawekee.(ikiwa umeridhia na hufungwi na imani yako pia)
Beer unaweza weka bia katika miundo miwili...Kuuza take away(wanaenda kunywa nyumbani),,,au kama eneo linaruhusu, kukawa na kasehemu wakawa wanakunywa kwa ndani/bandani (duka-grocery). NB usieke pombe ya banana kama eneo lako ni la wastaarabu).
Pombe za kupima kwa shot...pima K-Vant, Valuu, Konyagi n.k kuendana na eneo shot 500/1000
Weka vipombe vichupa vidogo,,,Azura/Rivella/Zed/Highlife/Konyagi ndogo/KVant ndogo, ukinunua kwa caton utapata faida kubwa zaidi, ukinunua kwa maduka ya jumla pia utapata pia.
Mfano kwa maduka ya jumla Azura/Rivella n.k unanunua 1600 unauza 200O kwa piece.
K-Vant unanunua 3000-3100....kuuza ni 4000
Konyagi 2700-2800 ....kuuza ni 3500
n.k ....n.k.
Vitu vya kupima pima...Kuna mchangiaji ameshaeleza kuhusu Prestige za kupima kwenye kurasa zilipita. Labda niongezee
Maziwa: Kuna maziwa ya kupima, ya fresh/chai na ya mtindi, itategemea zaidi na eneo ulipo sababu ya usafi/usalama kwa wateja wako. Maziwa bei ya kununua na kuuzia itategemea na maziwa unayapata kwa bei gani.
Kuna
Kuna vitu vingine dukani vinatembea fasta pia, kama unga wa lishe, unaochanganya mwenyewe pia. Ila kwa lengo la kuzungusha hela na kueka ubora unaeza nunua kwa watu na kisha ukaweka marhin kidogo ukauza dukani kwako.
Vitu kama sembe, dona kama unaeza saga mwenyewe, margin inakuwa kubwa zaidi kuliko kununua NB,,,hakikisha unatoa bidhaa bora inayofanana na hizi unga za special, wateja wengine hawaangalii brand,,,wanaangalia ubora/ladha basi.
MAGENDO:
Kuna watu huwa ni wapagazi/wasambazaji wa ma super dealer, huwa sijui wanaibagaje, ila wanaletaga bidhaa walizokwapaua kwa mabosi zao, sana sana nilichowahi nunua zaidi ni sukari, mchele mafuta na sabuni, bei zao huwa zinakuwa chini sana, mfano mfuko wa sukari wa 50Kg wanakuuzia 85,000. Angalizo, wakidakwa umedakwa, ;JELAAA'
changamoto:
Changamoto za serikali anzia za kata (Bwana Afya), Manispaa (Ushuru) na TRA -Kodi haivikwepeki, kutana nao utajua jinsi ya kudili nao.
Udokozi wa muuzaji: Usipokuwa makini na stock zao utashangaa binti/kijana wa dukani anabadili nguo,saa na vitu vingi kwa kukuibia, kama hufanyi stock kwa kubanwa na muda, funga camera hata mbili tu, zinawaogopeshaga kuiba.