Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Una miumyo mzuri sana
 
Jibu makini
 
Pole sana Mungu alikuandikia hapo Na utafika mbali. JF kuna baadhi ya watu mpaka unajiuliza waliwahi kupitia chuo cha kamati ya Roho mbaya?

Yaani MTU anawaza Negative tu sio posive. Halafu unaweza kuta hata Kiosk hajawai uza.
 
Mimi ushirikina ulinifanya nifunge duka,nilizungukwa na maduka ya washirikina cha moto nilikiona,Najipanga nitafute sehemu nyingine nifungue tena,Vina faida sana hivi vidude ukipata site nzuri!
Pole sana Mungu alikuandikia hapo Na utafika mbali. JF kuna baadhi ya watu mpaka unajiuliza waliwahi kupitia chuo cha kamati ya Roho mbaya?

Yaani MTU anawaza Negative tu sio posive Halafu unaweza kuta hata Kiosk hajawai uza. VP lakini
Ulikutana na vimbwaga gani?
 
Fact.
Hivi aliyesema ukiuza laki 3 unapata tu Elfu 10 faida nani?
So itategemeana Na wingi wa Biashara Na mzunguko?
Kuna watu wanaweza kukatisha tamaa humu.
We acha tu.
Kamati ya Roho mbaya
 
Haya sokoro weito
 
Na mimi nasubiri majibu\ ushauri hapa
 
Safi sana hawa manspaa wanajionaga wao ndo wao
 
Biashara ya duka la rejareja siyo ya kudharau hata kidogo. Inatunza familia kabisa na kusaidia kugharamia baadhi ya matumizi kwenye familia. Watu wengi waliotanguliaga kuifanya hii biashara wako mbali saaana, wenmgine wamejenga na kumudu hadi nyumba 'ndogo nyumba' kwa retail shop.

Wengi wameshaongea mengi mazuri kwenye kurasa zilizopita, na mimi sababu ni mzoefu kiduchu, wacha pia nitoe mawili matatu ambayo sijaona yakiorodheshwa hapa, huenda watu wanafanya katika maduka yao au hawafanyi, kama hufanyi unaweza tendea kazi.

USIACHIE FURSA. Kamwe usiuze 'HAKUNA'
Kitu kikubwa katika maduka ya rejareja ni kuhudmia hitaji la kila mmoja kadri uwezavyo. Kamwe usiuze hakuna ikiwa inawezekana icho kitu/bidhaa inaweza kuuzika katika duka lako. Hata kama mhitaji ni mmoja, mletee anachotaka. Ili mradi kile anachohitaji kipo kwenye uwezo wako na unaridhia kuuzika kwako.

Biashara ya vilevi na sigara.
Siagara, Angalia eneo lako la biashara kama kuna watu wanahitaji sigara wawekee.(ikiwa umeridhia na hufungwi na imani yako pia) Beer unaweza weka bia katika miundo miwili, kuuza take awa y(wanaenda kunywa nyumbani), au kama eneo linaruhusu, kukawa na kasehemu wakawa wanakunywa kwa ndani/bandani (duka-grocery). NB usieke pombe ya banana kama eneo lako ni la wastaarabu).

Pombe za kupima kwa shot
Pima K-Vant, Valuu, Konyagi n.k kuendana na eneo shot 500/1000. Weka vipombe vichupa vidogo: Azura/Rivella/Zed/Highlife/Konyagi ndogo/KVant ndogo, ukinunua kwa caton utapata faida kubwa zaidi, ukinunua kwa maduka ya jumla pia utapata pia.

Mfano kwa maduka ya jumla Azura/Rivella n.k unanunua 1600 unauza 200O kwa piece.
K-Vant unanunua 3000-3100, kuuza ni 4000
Konyagi 2700-2800, kuuza ni 3500 n.k.

Vitu vya kupima pima
Kuna mchangiaji ameshaeleza kuhusu Prestige za kupima kwenye kurasa zilipita. Labda niongezee
Maziwa: Kuna maziwa ya kupima, ya fresh/chai na ya mtindi, itategemea zaidi na eneo ulipo sababu ya usafi/usalama kwa wateja wako. Maziwa bei ya kununua na kuuzia itategemea na maziwa unayapata kwa bei gani. Kuna vitu vingine dukani vinatembea fasta pia, kama unga wa lishe, unaochanganya mwenyewe pia. Ila kwa lengo la kuzungusha hela na kueka ubora unaeza nunua kwa watu na kisha ukaweka marhin kidogo ukauza dukani kwako.

Vitu kama sembe, dona kama unaeza saga mwenyewe, margin inakuwa kubwa zaidi kuliko kununua.

NB: Hakikisha unatoa bidhaa bora inayofanana na hizi unga za special, wateja wengine hawaangalii brand, wanaangalia ubora/ladha basi.

Changamoto:
Changamoto za serikali anzia za kata (Bwana Afya), Manispaa (Ushuru) na TRA -Kodi haivikwepeki, kutana nao utajua jinsi ya kudili nao.

Udokozi wa muuzaji
: Usipokuwa makini na stock zao utashangaa binti/kijana wa dukani anabadili nguo,saa na vitu vingi kwa kukuibia, kama hufanyi stock kwa kubanwa na muda, funga camera hata mbili tu, zinawaogopeshaga kuiba.
 
Asante ndugu
 
Brother
Hongera kwa wazo zuri
Kiukweli natambua japo sio kiundani sana kuhusu duka la vyakula
Yaan reja reja
Kila kitu kina faida yake na hiyo faida ni kuanzia 20 au zaidi
Mm nina duka la vyakula
Nakupa mfano wa vitu vichache vinavyotoka na vina faida zaidi ya 20%
Karanga 50kg ni 125000 nauza 3000*50=150000 faida ni 25000/
Azam poa (unga wa ngano ) nanunua 30 nauza 37500 faida =7500
Makande nanunua 50kg kwa 60,000 nauza 75000
Faida 15000
Sunkist unga wa ngano
Nanunua 28000 nauza 36000 faida 8000
Mafuta ya safi lt 20 nanunua 57000 nauza 70000 faida ni 13000
Huo ni mfano tu vipo vingi vyenye faida pasu kwa pasu
Mfano
Bambino
Wembe
Sindano
Uzi za viatu
Mifuko
Uzi za nguo
Nk
Hivyo usimamizi ukiwa mzuri na location nzuri utapata faida
Ila kumbuka kuuambia moyo wako utulie mjini kuna vya watu
Kila la heri mkuu
 
Naona bora hata duka la vyakula lina maslah kuliko duka la kawaida maana kuna bidhaa inakupa faida ya 8000 sasa kwny duka la kaawaida kuna baadh ya takeaway unanunua sh 417 unakuja kuuza 500 kweli utatoka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…