Mkuu Ibravo,
Kwanza kabisa nikukaribishe humu maana unaonekana umejiunga humu this month hivyo you are still junior member, kwa kifupi humu kuna changamoto nyingi na shauri nyingi ambazo hata nyingine zinaweza kukukatisha tamaa kabisa au hata kujuta kuwa hivi nani alikushauri kuingia humu na ku-post threads za hovyo hovyo (wachangiaji wengine wanaweza kuziona hivyo), leo nikupe changamoto moja juu ya hii thread uloleta hapa:
Ibravo, sina nia ya kukukatisha tamaa juu ya mpango wako wa kuanzisha biashara ya duka hilo kwa capital hiyo ambayo umebahatika kuipata, ila to be honest nimeshangazwa na kusikitishwa na wazo hili kutoka kwako (msomi/graduate mtarajiwa). Naomba niseme wazi kuwa elimu unayosoma haijakusaidia chochote na nadhani ulikuwa unapoteza muda huko au labda ulikosea fani ulokuwa unasomea, wapo vijana wengi wanaenda vyuoni kusoma kwa mkumbo tu bila kujua anakwenda kusomea nini hasa. Lakini nadhani hapa ni uelewa wako tu ndo maana una wazo la kujiajiri, vinginevyo ningekulaumu kwa namna tofauti.
Nina imani watajitokeza wana JF wengi ambao wakisoma mchango wangu huu hawatanielewa, ila acha tu niseme ulonilazimisha kusema hasa baada ya kusoma uzi wako Ibravo.
Hata kama tunasema UJASIRIAMALI, inawezekanaje MSOMI/GRADUATE mtarajiwa unatoka chuoni unapewa mtaji wa mil 1, then unakurupuka na wazo la kufungua duka la kuuza UNGA, MCHELE n.k (UCHUUZI)? hivi hapa tutasema shule/elimu imekusaidia??? Na hapa niseme kuwa kama vijana wengi mnaenda vyuoni mnalipa fees huko miaka 2,3-4 nakuendelea, mnamaliza mnakuja na mawazo ya namna hii huku mitaji ya kiasi hiki mnabahatika kupata then niseme wazi kuwa elimu itakuwa haijawasaidia. Haya ni mawazo MGANDO, mtu unataka kufanya kitu kwa mazoea tu kwa kuwa watu wanafanya, huu si UJASIRIAMALI, ujasiriamali ni uwezo wa kubaini fursa kulingana na mtaji ulionao.
Nafurahia sana na watu wanaokuja humu kuuliza ili wapate mawazo kutoka kwa wachangiaji wanaJF great thinkers, wengine wanaenda mbali zaidi kwa kutamka kiasi (initial capital) alichonacho na anaomba ashauriwe afanye shughuli gani, watu wanatoa ushauri ktk shauri hizo wanasema AKILI YA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO, then unapata shughuli ya kufanya. Ibravo nimesema sina lengo la kukukatisha tamaa ila nakueleza tu ya moyoni, wewe umeleta hapa wazo ambalo tayari unalo kichwani ndo maana watu wameshindwa kukushauri ila nina imani wengi wamekushangaa GRADUATE mtarajiwa unaleta wazo la namna hii hapa. Shughuli unayotaka kufanya hata ambaye hajasoma anafanya tu, ni UCHUUZI huo. Nilitegemea msomo uje na wazo tofauti kabisa kwa mtaji huohuo kwa kuwa kwa mjasiriamali wa kweli mil. 1 ni mtaji tosha tu.
Baada ya kukueleza haya sasa nakupa wazo, unaweza kulichukua au ukaliacha integemea kama umenielewa au utaniona nimeku-dis sana; Kwanza kabisa kwa kuwa umesoma inabidi uwe na mawazo mchemko si mgando, inabidi uwe tayari kutoka mjini kwa kuwa kwa wazo lako ulilo nalo unaonekana unaishi ama unataka kuishi mjini tu, kwa mjasiriamali hili halimfungi kwa namna yoyote.
Pili inabidi uondokane na mawazo ya biashara hizi za UCHUUZI, jaribu kufikiria mawazo ya ki-uzalishaji zaidi, (kilimo, ufugaji, viwanda n.k) na siyo duka, kwa mtazamo wangu miye kuwa na duka la kununua na kuuza (UCHUUZI) ni uvivu wa kufikiri tu, hivi uliona wapi Mzungu anauza duka bwn? Hizi ni kazi za Wahindi, ni wavivu wa kufikiri tu. Sisemi Wazungu ndo bora sana ila walio wengi wana mawazo bora, yeye anafikiria akutengenezee SIMU, uwasiliane na jamaa zako, ukishaona umuhimu wake utamtafuta tu ununue kwake na hapo utaona WAVIVU WA KUFIKIRI aka WACHUUZI wanapanga foreni kiwandani kwa Mzalishaji kuweka order ya handsets za simu, JAMAA ANAPIGA HELA. MZALISHAJI anatengeneza kitu BORA kwa kuwa anajua WAVIVU WA KUFIKIRI/WACHUUZI watamsaidia (bila wao kujua) kuuza bidhaa zake.
Ibravo nimesema sikukatishi tamaa ila ningekukubali kama ungekuja hapa na wazo kuwa kwa kuwa umeenda shule basi ungeuliza humu kuwa una mtaji wa hela hiyo (1mil) then unataka kulima Mahindi, Mpunga n.k (kwa kuwa unaonekana una interest na vitu hivyo) then upate sasa mawazo ya GREAT THINKERS. Asikwambie mtu, KILIMO ni moja ya UZALISHAJI na si UCHUUZI, wewe lima tu kitaalamu, vuna mazao yako, utaona WACHUUZI wanakuja wenyewe kutaka kuuza bidhaa zako, we unapiga hela tu unakuna kitambi (unajua tena wabongo kwa vitambi) na nikupe siri, Tsh. 1,000,000/= kuwekeza kwenye kilimo ni mtaji mkubwa mno (kama upo tayari kuondokana na mawazo ya kukaa mjini).
Huku kwetu kukodi heka moja ni Tsh. 30,000 hadi 45,000 kwa mwaka na huku kwetu kwa mwaka tunalima mara mbili (mvua za vuli na masika), kwa hela ulonayo utakuwa na heka za kutosha, sema anza na heka 5 ambayo itakugharimu Tsh. 225,000/= kukodi tu mashamba. kulima kwa tractor kila heka moja ni tsh. 40,000 x 5= 200,000/= zinazobaki fanya matumizi mengine kama palizi, mbolea na matumizi mengine kama hayo, hapa bro unazungumzia miezi mitatu tu kama ume time mvua za vuli tayari utakuwa na magunia yako 5x15= 75 ya mahindi, huku kwetu wakati wa msimu wa mavuno gunia la mahindi linauzwa Tsh. 45,000/= x 75= 3,375,000/=, kumbuka hapa umelima mvua za vuli tu, utaingia tena shambani mwezi Feb ili u-tme mvua za masika, na hakuna tena gharama ya kukodi maana ni ileile ulolipa awali, mwezi wa sita tena unavuna mazao yako unasubiria WACHUUZI tu, unapiga hela. Mkuu ukikomaa ki-jasiriamali baada ya miaka michache nina uhakika mashamba hutakodi tena, utakuwa na ya kwako, utaanza ufugaji, maana kuna uzi wa MALAFYALE Jukwaa la Ujasiriamali unasema 'Kilimo na Ufugaji kwa pamoja vinalipa' nenda kasome pale uone GREAT THINKER wanavyokuwa na mawazo ya ki-GT.
Kwa leo mkuu.