Ok hoja nzuri na inaonesha unataka ufumbuzi wa kibiashara.. zingatia mambo yafuatayo wakati unaanzisha biashara.
1. Aina ya wateja unaowatarget mf wazee, watoto, wanamama, maduu nk..
2. Nyakati husika ya biashara yako.. hapa angalia jinsi gani biashara yako kama inaendana sawa na nyakati zilizopo mfano.. nyakati za magufuli huwezi uza maziwa ya NIDO au aina yoyote ya maziwa ya unga ya bei kubwa pia huwezi uza vitu vyenye bei kubwa zaidi kwa sababu za kiuchumi.
3. Location.. angalia eneo ulilopo je wakazi wengi ni matajiri au masikini au wa kiwango cha kati?? Kama matajiri always wanapendelea kununua vitu kwa pamoja na sio daily kununua kilo ya unga nk. Masikini wao hununua kilo moja moja daily.. hapa itakusaidia kubalance stock/inventory zako.. yaan kama ununuaji wa kilo moja moja basi yafaa ukichukua mzigi uangalie zaidi mauzo ya wiki..
4. Mjue mshindani wako vizuri.. kosa kubwa tulifanyalo ni kwamba hatutaki kujua washindani wetu hutumia mbinu gani ili kufanikisha mauzo.. ukijua hilo utapata njia mbadala ya namna ya kuwapata wateja wapya.
5. Kama ni duka nakushauri deal na watoto wadogo.. kivipi kila mtoto akija kununua kitu iwe unga, sabuni, mafuta nk mpatizie kizawadi kidogo mara nyingi pipi ikiwa ivory au ukiweza hata pipi kijiti za bei rahisi.. hali hii itamfanya mtoto kila atumwapo kwao akimbilie dukani kwako.. mwisho wateja wengi watakupenda kwakuwa tu watoto wao wanafuraha na wewe.
5. Ishi vizuri na muuzaji/mfanyakazi wako.. mwelekeze kuwa duka lile ni kama lake hivyo likifa na yy hatokuwa na kazi hivyo aipende kazi yake.. hapa sasa siku zingine unamruhusu akatembee, unampa zawadi mbalimbali hadi duka likae sawa..
6. Jitahidi kuficha itikadi za chama, dini na ukabila.. hapa wengi hufeli na hupoteza wateja kwa sababu ndogo sana..
NB BIASHARA ZA USHIRIKINA ALWAYS HAZICHANUI VIZURI.. Labda ujigange wewe mwenyewe na duka lako lkn sio dawa ya kuvuta wateja.. hakuna hiyo kitu kakangu
Kwa msaada zaidi nicheki whatsapp 0718007719 free