Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Asante sana feity na wadau wengine mliochangia na mtakaoendelea kuchangia. Naamini kweli inaweza ikawa sijawaza vyema sana na ndio maana tunashirikishana wadau kupata mawazo pevu na mbadala, najua huku wako wadau wengi wenye ujuzi, ufahamu, uelewa na moyo wa kusaidia na kushauri. asanteni.
 

Ushauri mzuri sana mkuu ila nawe ni vyema ukashauriwa kama bado una mawazo mgando. Kwanza nikukatishe katika hizi biashara ulizoziita za uchuuzi zimetoa mabillionea kama Amarcio ortega okay tukiachana na hawa turudi kwa hao wazungu uliowasema haawafanyi kuna huyu mfaransa Benard Arnaut njoo mwana mama Lilliane Bettemcount SIJUI HAWA UTASEMAJE WAMEINGIA FORBES KWA BIASHARA ZA RETAILING (UCHUUZI)

Rudi kwetu Tz Mfugale kaanzia biashara ya duka ndio imemfikisha kuwa billionea kwa hiyo ushauri wako una mikingamo kitu ambacho si kizuri kibiashara million moja inatosha kabisa kuanzisha duka KUFIKIA UMILIONEA HIYO NI AKILI YAKO


NGOJA NIKUCHANGANULIE UONE USIJIUNGE KATIKA HAWA WENGINE WENYE KUDHARAU

Kodi ni elfu 50 kwa mwezi utaitoa ya miezi mitatu 150000
Friji laki tatu kubwa
Shelf za kawaida elfu 80
umashamaliza =530,000 jumla kinachobaki mahitaji na katika mahitaji yako usisahau kuweka maji ya kandoro na barafu vyote viwili mtaji wake hauzidi 40,000 yaani kununua deli elfu 20 na inayobaki materials

Kwa hiyo laki nne utanunua mahitaji ya duka laki tano na 70 ya kodi frij shelf na deli la maji kandoro + barafu

BILLONAIRE WENGI DUNIANI HAWATOKI SEKTA YA KILIMO NI SEKTA YA TECHNOLOGIA BIASHARA NA UWEKEZAJI

NA BADILIKA MKUU ELIMU YA DARASANI HAIHUSIANI NA MAWAZO YA KIBIASHARA/UBUNIFU HAYO NI MTU MWENYEWE anajiongoza kiasi gani

hata uwe na masters doesn't mean utaweza kuyatawala mazingira ELIMU KWA MTU YEYOTE INAONGEZA KUJITAMBUA HICHO NI TOFAUTI NA MAFANIKIO

Kama unabisha hebu soma muda gani Marekani/dunia ilibadilika katika kuamini Elimu at what time world rule changed
obviously its 1973
 
Ahsante bora kujua kuliko kujifanya unajua kumbe hujui, mficha uchi
 
Hizo dharau.Wenzio wanalea familia na kujenga kwa biashara hii hii.We bakia na mawazo yako hayohayo
kweli mkuu mkuu duka la rejareja milion 2 zingatia hesebu kkwa mwaka m.6
 
Hii biashara unalipa hasa km utakuwa unakaa mwenyewe dukani! kwani faida yake ni hizo 50 na mia mia...ukimueka mtu kila siku akichukua buku 5 atakuuwa! kaa mwenyewe utaenjoy biashara..pia usiwe na tabia yakufunga funga duka mara kwa mara! hakikisha unafungua duka mapema na unachelewa kufunga! mteja anapenda duka linalofunguliwa mapema utajijengea jina! 10% ndio faida yako
 
Nimeipenda, siri ya biashara yoyote ni kuzingatia muda wa kufungua na kufunga, pili usiwe mambo mengi mara leo upo kesho haupo,, tatu onesha ukali kias kwa anayetaka mazoea ndan ya biashara yako,, nne usibangue mtu yeyote neno ahasante mteja ni zao kuongeza wateja,,, kama unaumwa na umeamua kukaa dukan mteja wako muweke wazi, tano daftari la biashara uiheshim zaid ya pesa uliyoishika andika kila unachotumia toka dukan mwako, itakusaidia kutambua jinsi ya kubana matumizi, KUKATA TAMAA AU KUTOJIHAMIN HUTOWEZA FIKA POPOTE
 
Duh 2milion, unakazi kubwa mana kupiga shelves si chin ya laki sita kwa frem nzuri then jumlisha kodi ya Six month, ununue friji, inabaki tulaki kidogo unless ufungue kiduka mshenzi kama unavijua.

Location ni sehemu yenye makazi mengi ya watu tena wa hali ya kati sio Wale wa super market, au shughuli nyingi za watu.

Kinachopelekea hasara ni matumiz kuzid faida na bidhaa kuisha muda pia kuwa makin na watoto wa kike
 
Mimi pia nina wazo la kufungua duka la namna hii, ila ninampango wa kuajir mtu coz mm ni mtumishi mahali pengine, mtaji wangu ni 5m, nishawah kukaa dukan kwa wazaz, naomba kujua kwa uzoef wako kama hiyo hela itatosha.
 
Pesa hiyo mil 5 inatosha sana cha msingi weka bidhaa zile zinazouliziwa usiende jitwisha mavitu ambayo yatauzika baada ya mwaka mmoja bora uanze kwa kuweka kidogokidogo huku ukiangalia kipi kinatoka haraka na kipi kinauliziwa sana.
 
Mimi pia nina wazo la kufungua duka la namna hii, ila ninampango wa kuajir mtu coz mm ni mtumishi mahali pengine, mtaji wangu ni 5m,nishawah kukaa dukan kwa wazaz ,naomba kujua kwa uzoef wako kama hiyo hela itatosha

Inatosha
 
Vitu vya Msingi

1. Location

Angalia sehemu utaweka hiyo biashara yako kuna watu wa aina/kipato gani hii itakusaidia hata kujua ni bidhaa za aina gani uweke dukani

2. Usimamizi
Nani atakuwa dukani full time
Nani atafanya manunuzi
Nani atakeep records/files zile muhimu 6 ambazo

1.File la mauzo
2.File la Manunuzi
3.File la Gharama za uendeshaji
4.File la Bank
5.File la TRA
6.File la Mikataba/Mengineyo

3.Mahusiano/Mawasiliano
Ili ufanikiwe lazima uwe na Mawasiliano na Kauli nzuri na wateja au jamii inayokuzunguka ukiwa na mahusiano mazuri kwa Upande wa suppliers unaweza pata hata bidhaa on credit

4.Timing
Nature ya biashara hizi zinahitajika kila saa hivyo UKICHELEWA kufunga na UKIWAHI kufungua una nafasi kubwa ya kufanikiwa. Timing vile vile inahusiana na ununuzi wa baadhi ya bidhaa ambazo ni za msimu Ukiziwahi waweza hata kuzinunua kwa half price.

Thank You
 
Mr/mrs thanks so much bro, umebadili fikra zangu za maisha
 
Unapatikana wapi me nipo arusha nataka unifanyie research ya ɓiashara ya mitungi ƴya gas kwa hapa toun hapA nilipo wachawi wamekua wengi.
 
Kwanza nakupongeza sana kwa wazo lako. Ushauri wangu kwa pesa uliyo nayo lima kilimo cha uyoga. Nenda kwa wataalam wa kilimo wakufunze ukulima huu wa Uyoga kwakua umsomi mafunzo hayatazidi wiki na gharama yake ni nafuu mno sh.20,000' utakua umejifunza ukulima na jinsi ya kudhibiti magonjwa ya Uyoga na wadudu waharibifu wa Uyoga.

Then gharama ya mbegu shilingi elfu 5,vyumba viwili cha giza na cha mwanga utalima humo na kuuza mahotelini na kwa Catering kwa bei nzuri utashangaa unaingiza pesa kiulaini tena ukiwa kivulini. Ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…