Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Kama ni duka la vyakula. Bado mtaji wako mdgo ndgu ila unaweza ukaanza na duka la rejareja kwanza wakati unajipanga, wazo lako zuri sana. Keep it up
 
Good one, also this can be considered
 
Unapatikana wapi me nipo arusha nataka unifanyie research ya ɓiashara ya mitungi ƴya gas kwa hapa toun hapA nilipo wachawi wamekua wengi
Mmhh mitungi ya gesi nayo ijapokuwa sawa you can move with this.
 
Shortly ..there is a lot of bizness u can perform with that kind of capital....ts matter of research and good evaluation
 
Hiyo kampuni iko wapi?
 
Nitakupa ABC kwa biashara unayoiwaza sema waweza kuchanganua na kuamua kuongeza mtaji kwa njia nyingine.

MAHITAJI

1. Cheti cha Vipimo toka kwa Daktari anayetambulika na Serikali
2. TFDA certificate cost ~70,000/-
3. Tin number toka TRA na Clearance certificate pia kadirio la kodi si chini ya (360,000+ kwa miezi mi3)
4. Kodi ya nyumba si chini ya 50,000/- kwa mwezi

Kumbuka kuna ununuzi wa Mizani, friji (optional) na kupiga Mbao za kuoneshea bidhaa kama frame haina hivyo vitu.
 
Uko wapi mkuu, nataka wanifanyie market research kwa biashara ya duka LA vifaa vya ujenzi.
 
Biashara Ya Duka Kwa Mtaji Wa Mil 1
Inategemea Na Location Uliyopo
Kuna Location Unaweza Kuwepo Ikawa Ni Mtaji Sahihi Na Kuna Location Ikawa Ni Pungufu

Sema Pia Si Lazima Uanze Na Duka La Frame

Unaweza Kuanza Na Supply. Unaweza Fanya Supply Ya Mchele, Mahindi Au Nafaka Au Bidhaa Nyingine Yoyote Kulingana Na Location Uliyopo.

Nothing Is Impossible.
 
Hongera saana kwa kuwa na nia ya kuanza biashara, kikubwa tambua soko lako, wanahitaji nini, wapi, wakati gani, kiasi gani na kwa njia zipi.
 
Habari wanajamii wenzangu.

Ni mara ya kwanza naposti humu ila huwa nafaidika sana na mawazo yatolewayo hapa.Kifupi nakata kufungua duka mojawapo liwe la vinywaji laini namaanisha wines/ama liwe la nguo na vifaa vya watoto wadogo kama pampers ; wipes ; maziwa n.k

Naomba changamoto na faida za biashara hizi mwenye uzoefu katika hilo.

Nawasilisha.
 
Wakuu habar za midaa hii ya iftar inakaribia,

Nipo hapa nimekuja kuchek maendeleo ya duka langu duka toka 14.12.2015 lkn holaaa wadau linakula tu pesa zangu za kazin nimefukuza vijana wengi tu nikijua naibiwa tu na ni nimejaribu kuhama mara nyingi for location lakini napata gud location tu Dar kinondon

Nikawa napiga stor mbili tatu na mwenyeji hapa namweleza mzee mtaa huu mgumu watu weng lkn sion pesa mzee akacheka tu na kunieleza yafuatayo ndugu hapa kweli ni pagum lkn ni rahisi kivingine si unamwona shirima pale anajaza jiran yangu nae anaduka km langu anauza sn na wateja wanapanga foleni.

Nikasema mzee jamaa hapa nimemkuta lkn wateja wamepazoea mzee kabisha hamna ww siunaona na mwenzako pale anadonoa wateja jiran mwngne nae hola tu km mimi.

Usione watu wana maduka kuna siri nzito agiza bidhaa zako nje ya hapa maduka mengi ya jumla hapa pesa wanachukua mzigo unaisha pesa huoni au kama uko tayar kuna mtu yupo kigoma nikuunganishe nae? Mpaka mwakani utakuwa na maduka kama haya zaid ya manne kanipa na mfano wa mtu

Sasa mimi kama msomi na mshahara napata ila napenda maendeleo ya biashara pia nimeona niwafikishie ujumbe ndugu zangu mnishaur maana naona napoteza pesa zangu kuziweka dukan kila mwezi.

Nawasilisha
 
Usomi kwenye jamii yetu ya kiswahili waga tunauacha chuo linapokuja swala la maendeleo, uzuri ni kwamba wewe mwenyewe ni Shahidi kuwa kwako ndio biashara ngumu ila kwa mwezio biashara nzuri so uamuzi ni wako either uvue koti la usomi na kuvaa gwanda la kazi, kwa sasa business pote ni ngumu ila ugumu unatofautiana kutokana na mwenye hiyo biashara ni nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…