Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Kujua faida kwakwel ni ngumu mno....kujua kama kuna faida n kuangalia maendeleo ya biashara....kwamba vitu vikiisha hela ya kununulia ipo....na pia ukiongeza vitu biashara bado inakuw imesimama

Just hua tunajua faida kwa kuangalia maendleo ya duka....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu faida ya duka la rejareja ni kati ya 10% hadi 18%. Na hilo ni duka gani uuze 300,000 kwa mwezi? Mi nina duka la mtaji 2 mil nauza kati ya elfu 40 hadi 60 kwa siku pia nina genge nauza elfu 25 hadi 40 kwa siku. Na trend ya msuzo inakuwa positively

Kuuza laki 3 kwa mwezi maana yake unauza elfu 10 kwa siku. Hapo unakuwa ulifungua duka bila kupata ushauri au kupiga hesabu zako vizuri
Hivi zile friji za kuweka dukani nje kwako unaweka vinywaji kama yorgut,soda,energy yanauzwa sh ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha cajojo we unajuaje faida tuambie

Sent using Jamii Forums mobile app
Mm mpk leo mume wangu ananiambia eti sijapata faida wala nisiweke hela eti ni faida najidamganya so hela zote nazirudisha kwenye kununua bidhaa i mean nanunua na pia naongezea bidhaa mpya. So mpk sasa hivi sijajua ntatoaje faida nilitamani na mm kujua hilo somo
 
Njooni tuelimishane jamani halafu yule mdau alietupa moyo na list ya biashara hataki hata kujibu pm jamani it means yy ameshakua mzoefu sana angekuja kutusaidia
 
Nilitaka kufanya maamuzi ya haraka na sikuwa na mda wa kusubiri japo kuna waliojitokeza kunisaidia na nawashukuru sana. Sio kwamba sikujua kuwa nitapoteza elfu 40 ila kama kuna mtu angejitokeza na kunipa vitu nilivyotaka sikuwa na hiana kumpa hiyo pesa maana nilishapanga kufanya hivyo na najua angepoteza muda wake na rasilimali kuifanya hivyo.
Sema uko vizuri maana naona and umefikia mpaka kutathmini Break Even Point
Najua utakuwa unasimamia Duka mwenyewe kwa 100% hebu niambie likija suala la business expansion let's say una maduka mengine 2 au 3, ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm mpk leo mume wangu ananiambia eti sijapata faida wala nisiweke hela eti ni faida najidamganya so hela zote nazirudisha kwenye kununua bidhaa i mean nanunua na pia naongezea bidhaa mpya. So mpk sasa hivi sijajua ntatoaje faida nilitamani na mm kujua hilo somo
Unaweza kupercent kabla ya kununua mzigo mpya na kuhifadhi kiasi cha hiyo percent na baada ya mwaka au mwezi....
Au, waweza andaa excel sheet na kujua bei ya manunuzi na mauzo ukajua faida......
Au, wengine ufanya kwa kila siku kutenga kiasi pembeni bila kuathili bidhaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kupercent kabla ya kununua mzigo mpya na kuhifadhi kiasi cha hiyo percent na baada ya mwaka au mwezi....
Au, waweza andaa excel sheet na kujua bei ya manunuzi na mauzo ukajua faida......
Au, wengine ufanya kwa kila siku kutenga kiasi pembeni bila kuathili bidhaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu
 
Natamani kufahamu unafanya vipi hesabu za dukani kwa ulichouza na kujua kujua faida hasa kama umemweka kijana?unacontrol vipi sales zako za kila siku
Nilisema mwanzo kuwa ninatumia programme inaitwa daily sales records, hii ni online programme na kila kijana akiuza anaandika na mimi kazi yangu nikifika dukani ni kuingiza hizo data kwenye programme. Programme inakuwa na bei ya kununulia na bei ya kuuzia hivyo inakuwa rahisi kujua kwa siku umeuza kiasi gani na imekupa faida kiasi gani. Lakini hii haitoshi kujua kama umepata faida siku hiyo, nina daftari la matumizi dukani ambalo hujazwa kila matumizi yanayofanyika dukani. Mfano kama kwa siku nimeuza bidhaa za thamani ya 40,000 na faida labda ikawa 12,000 baada ya kutoa bei ya kununulia then natoa matumizi kwa siku hiyo na hii inanisaidia sana kujua kwa siku nimeingiza kiasi gani. Ikifika mwisho wa mwezi pia nafanya hesabu kwa mwezi maana ninakuwa na data za kila siku hivyo inanirahisishia kujua faida kwa mwezi.
 
Hiki kitu kinanishinda hata mimi ndugu yaani kupanga mahesabu kilichotokea, kilichoingia na kilichobaki
Faida hasara na baki

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni rahisi sana. Kwa mtu anayeanza unachotakiwa kujua ni bidhaa hizo umezinunua kwa bei gani (cost of goods) na unatakiwa kuziuza kwa bei gani(sales). Kingine unatakiwa kujua gharama ambazo unaziingia kwa siku kwenye duka (running cost) tofauti na zile za manunuzi ya bidhaa za kuuza. Baada ya hapo kama umeleta mzigo uko dukani andaa stock ya vitu vyote kwenye daftari ikiwa na bei zake za kununulia (cost of goods) na bei za kuuzia(sales price). Hii stock itakupa thamani ya bidhaa ulizonazo dukani. Kila ukiuza andika pembeni hiyo bidhaa na bei yake ya kuuzia kwenye daftari la mauzo na kama kuna gharama umezingia dukani ziandike chini kwenye daftari la matumizi.

Kujua faida
Ikifika jioni fanya mahesabu kujua leo umeingiza kiasi gani kwa kufanya hivi. Mfano kama umeuza sabuni ya Jamaa kipande kimoja kwa shilingi 500 tafuta bei(cost of goods sold) ya kununulia ya hicho kipande ambayo unachukua bei ya mche mmoja unagawa kwa tano kama unakata vipande vitano au 6 kama unataka vipande 6. Mfano kama mche mmoja ni 1800/- kwa hiyo kila kipande kinauzwa kwa bei ya jumla 360/-na wewe ukiuza 500/- unakuwa na faida ya 140/-. Kwa kila bidhaa fanya hivyo na tafuta jumla ya faida kulingana na bidhaa ulizouza. Baada ya hapo kwa siku hiyo husika jumlisha matumizi(running costs) ya dukani ya siku, mfano chakula, kama umekunywa maji ya dukani ni matumizi pia (andika 500 kama umekunywa maji ya jero), umeme kama umelipa siku hiyo, usafiri wa kwenda na kurudi dukani nakadharika. Chukua jumla ya matumizi kwa siku alafu itoe kwenye ile faida hapo juu kujua kwa siku wewe umeingiza faida kiasi gani.


Kujua Kilichobaki

Ili kujua kilichobaki ndani ya duka (existing inventory) lazima utoe idadi ya bidhaa uliyouza kwenye stock yako. Mfano kama ulinunua mche mmoja na sasa umeuza kipande kimoja cha jamaa, ukitoa utabakiwa na vipande 4 kwenye stock. Kwa mantiki hiyo utakuwa umebakiwa dukani na bidhaa zenye thamani ya shilingi 500x4 = 2000 ambayo gharama ya bidhaa hii iliyobaki (cost of goods) ni 1440(360*4). Hii itakusaidia sana hasa kujua bidhaa ambayo inapungua dukani ili ujue unavyotaka kwenye kuhemea mzigo mwingine utaenda kuchukua bidhaa zipi.

Shida kubwa ni kuweza kuandika kila kitu unachouza na kuweka record ya matumizi. Kuna wakati wateja wanakuwa wengi kiasi kwamba huwezi kuandika kwanza ndo umhudumie ni kama utamchelewesha na ataenda kwingine. Wazungu wao na hata sasa kwenye supermaket wanascan zile bidhaa unavyozinunua hii unawasaidia sana kujua kwa siku wameuza nini na kwa kiasi gani maana inatunza kumbukumbu. Mtaani kwetu huwezi kuscan robo kilo ya maharage na pipi moja ya tofi. Sio lazima uandike vyote ila unaweza kutunza kumbukumbu unapokuwa na wateja wengi na kuandika baada ya kuwa umewahudumia. Ila wauzaji wengi ni wavivu wa kuandika na inanishangaza sana maana ndo kazi yako hiyo hakuna nyingine kwa nini usiandike sasa kama wewe maisha yako ndo hayo kila siku. Tujifunze kujituma na kufuata kanuni za biashara hata kama ni ngumu zinasaidia sana hasa hili eneo la kujua faida na hasara.
 
Kujua faida kwakwel ni ngumu mno....kujua kama kuna faida n kuangalia maendeleo ya biashara....kwamba vitu vikiisha hela ya kununulia ipo....na pia ukiongeza vitu biashara bado inakuw imesimama

Just hua tunajua faida kwa kuangalia maendleo ya duka....

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna urahisi sana wa kujua hili soma hapo juu
 
Mm mpk leo mume wangu ananiambia eti sijapata faida wala nisiweke hela eti ni faida najidamganya so hela zote nazirudisha kwenye kununua bidhaa i mean nanunua na pia naongezea bidhaa mpya.

So mpk sasa hivi sijajua ntatoaje faida nilitamani na mm kujua hilo somo
Soma hapo juu jinsi ya kujua faida. Ila mume wako atakuwa anakuambia kuwa hujaweza kupata faida kwa maana nyingine. Ili useme umeweza kupata faida ni pale ambako faida unayoipata umerudisha pesa uliyoiwekeza. Mfano mimi niliwekeza 6 million na kwa miezi mitatu ya operation nilikuwa na kiasi cha 800,000 kama faida yaani hapa nimetoa pesa ya manunuzi na gharama za uendeshaji duka.

Hivyo nitaweza kusema nitapata faida pindi hii 800,000 itakapofikia 6,000,001. Nimeweka shilingi 1 maana ndo faida hapo unaanza kuiona. Ukifika hapo ndo panaitwa break even point. So mume wako anaweza kuwa anazungumzia hapa labda hajataka kukuwambia vizuri uelewe. Nini maana ya hii; hii ina maana kwamba unapoanzisha biashara kwa maoni yangu sasa ni lazima biashara uilenge iwe ni ya mda mrefu na sio ya mda mfupi. Ya mda mrefu kwa sababu sio rahisi kuweza kurudisha 6,000,000 kwa miezi miwili au mitatu kwa sababu ni biashara mpya pengine na wateja sio wengi wanaoijua na pia hata wewe hujapata uzoefu wa kuiendesha na kuisoma vizuri.

Ni kipindi ambacho pia utajikuta unaingia tena gharama nyingine kuongezea pesa kutoka mfukoni mwako kipindi ambacho biashara haijaanza kuwa na mzunguko mzuri wa kurudisha gharama zake. Mwambie honey just be patient faida itapatikana tu. Na mwambie hapa ndo na mimi napata mahari pa kwenda kama wewe unavyoenda kazini au kwenye kazi zako nisibaki nyumbani tu.......
 
Natamani kufahamu unafanya vipi hesabu za dukani kwa ulichouza na kujua kujua faida hasa kama umemweka kijana?unacontrol vipi sales zako za kila siku
Ni ngumu sana kufanya stock taking dukani labda uwe mtaalam haswa ukimkabidhi fanyeni stock ukiongeza mzigo unaongeza kwenye stock mwisho Wa mwezi mnafunga stock nayo pia itakuwa ngumu maana maduka yanafungwa SAA tano au sita hiyo inamaanisha mkeshe mkifunga stock which ni ngumu ukubali kuibiwa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom