Biashara ya Fuso La Mizigo

Biashara ya Fuso La Mizigo

Wapendwa katika biashara, nataka kununua Fuso la kubeba Mizigo ya Mikoani. Sijawahi kufanya biashara yoyote ya kusafirisha mizigo wala ya magari aina yoyote. Ningependa kujua yafuatayo kutoka kwa watu wenye uzoefu na hii biashara;
1. Uchungu na utamu wa hii biashara.
2. Mambo ya kuzingatia katika kuendesha biashara hii.
3. Ni anina gani Fuso ambayo ndo ina faa kwa biashara ya aina hii.
4. Modification zinazotakiwa kufanyika kwenye gari mara baada ya kununua na wapi zinafanyika.
5. Wapi nitapata gari zuri/ website/link au kwa mtu anayeuza hapa hapa nchini.
6. Return on Investiment ikoje.
7. Mengineyo

Asante sana
iMind
Huko mkoani kanunue plot jenga nyumba upangishe.gharama za ujenzi mkoani zipo chini isipokua nondo na cement na mabati.SHIKA WAZO LANGU gari ni presha tupu TRA POLISI Bima Spare Mafundi watahamia kwako
 
tipa fuso inalipa..ww uko wapi?sbb kila sehemu ina day yake...au nipm
 
Fasta chukua fuso ya mchanga kisha njoo nayo Mwanza uone utakavyooga pesa,hesabu per week ni laki5 na gari hiyo ni malufuku kubeba mawe,ni mchanga na kokoto tu,kama unaona nadanganya fatilia utajua!
 
inategemea na "cubic meters"maana kama una nguvu ya pesa tafuta scania mende hapa hapa dar uone maajabu kwa "siku" hesabu ni 500000/=
 
fasta chukua fuso ya mchanga kisha njoo nayo mwanza uone utakavyooga pesa,hesabu per week ni laki5 na gari hiyo ni malufuku kubeba mawe,ni mchanga na kokoto tu,kama unaona nadanganya fatilia utajua!

laki 5 kwa wiki , nimelogwa ?
 
Sikutishi mdau ila nakwambia niliyoyashuhudia kwa macho yangu.
Jirani yangu ni dereva wa serikali siku nyingii kitengo cha mizigo. ashaendesha malori na katembea karibu mikoa yote ya tz.
Alipopata lidandasi akaamua anunue fuso ili aendelee kujipatia kipato chake cha kila siku.
Akalipeleka jangwani akalikabidhi kwa madalali tayari kulidalalia. Madalali wakamwambia safari inayolipa ni kusini mwa nchi yetu.
Mzee kwa kujiamini akakubari na kurudi nyumbani kujiandaa na safari. kumbuka ni safari ya kwanza kwa gari yake hii mpya. anaendesha mwenyewe kwa hiyo hakuna wasiwasi.
Punde madalali wakampigia simu gari ishapakiwa mzigo akaichukue.
Avofika jangwani (kipindi hicho) halahaulaa gari imekuua ovaloded mpaka limelala upande. Madalali washalamba chao wakaanza mpa maneno matam mzigo wafika huo mbona nyingine zabeba zaidi ya huo.
Mzee wa watu akaondoa gari kishingo upande. Kufika kilimalondo gari ikashindwa pandisha mlima ikarudi nyuma na kupinduka. Mzee alijeruhiw sana. Gari ndio trip yake ya mwanzo. Mzee alianza ugua prehsa, gari ikauzwa scrap. umasikini ukashika kasi, imani za kul0gwa zikatawala. asee nilimuonea huruma. Nakusihi kua makini mdau na hili.
 
Natumai watu wenye kutoa ushauri wote wametoa ushauri na maangalizo mzuri.

Biashara hii inalipa asikudanganye mtu.

Mie mwanzo nili pick Idea ya Boda boda watu wakaponda sana humu na kusema watu wengie wanafanya na zimekuwa nyingi sana mjini hazina isssue na mambo tele,na wengine wakanipa moyo.

Na kuna Member mmoja aliniambia kwamba nianze na Bodaboda 3 ili niweze kuona faidi yake vizuri.
Mbali na vitisho vyoote nikaweka ndoto zangu na ilikuwa mwaka jana,mpaka sasa naendelea vizuri na heasbu nakula 50,000 kwa wiki kwa kila moja.

Nikaweka Carry 3 njiani nakula 20,000 kwa siku.
Changamoto ya gari ni kwamba tafuta Fundi wako maalum ambapo kila kitu atakuwa anashughulikia yeye.Na atakuwa anaijua gari A-Z.
Halafu toa pesa ufungiwe GPRS Car Truck System,mie nilitoa Laki 3 kwa kila Carry moja kwa mwaka.Na ninaweze ku access na kujua gari ipo wapi hata nikiwa huku Zanzibar.

Na kama unae kijana katika familia mwenye Idea ya ufundi jaribu kumpeleka chuo cha ufundi magari kama Veta ili awe msimamizi.Hili nimefanya na imefanikia.Services za Bodadboda na Carry zangu anashugulikia yeye.

Maana gari hilo ndani na mwaka linanunua gari jingine.
Kuna watu wanamiliki gari zaidi ya kumi na walianza na moja kama wewe mpaka wengine wameanzisha Kampuni za usafirishaji.
Na sio kila alieshindwa biashara basi wenzie wasifanye,we ukiacha na ukienda kule kwenye Usajili unakuta wenzio wanasajili magari hayo karibu kila siku.
Changamoto katika biashara ndio fursa kwako.

Kumbuka Mike Iron Tyson aliwahi kusema kwamba Mpira wa miguu ni mchezo hatari sana kuliko ngumi.
Sasa wacheza mpira walishangaa sana na kumuona kituko ila wacheza ngumi wakaona ni kweli.

Tafuta dereva mwenye Mdhamini mwenye mali iliyo sawa na Gari yako na pia ikatie Comprehensive insuarence.
Madereva wapo tele tu na wenywe sifa nzuri.
Pia usimbane sana,mwachie apige gozigozi ndogo za njiani ili yeye apate kidogo na wewe kidogo,kama alivyosema mdau hapo juu kwamba na yeye awe dalali kimtindo.

Umuhim wa Car Truck system ni mkubwa sana licha ya kwamba watu wengi wanaidharau ila matajiri wakubwa karibu wote Gari zao zimefungwa mfumo huu na ni kwamba Dereva atakuwa mkweli kwako kwa kiasi fulani.
Kwanza -
-Dereva akienda kasi itakuambia kwamba Driver wako yupo mwendo kasi
-Itakupa update ya ulaji wa mafuta wa gari yako
-Driver akisimama inakuambia na kukuonyesha
-Ikifika Km za kufanya Services ndogo itakuambia
nk.
 
Wapendwa katika biashara, nataka kununua Fuso la kubeba Mizigo ya Mikoani. Sijawahi kufanya biashara yoyote ya kusafirisha mizigo wala ya magari aina yoyote. Ningependa kujua yafuatayo kutoka kwa watu wenye uzoefu na hii biashara;
1. Uchungu na utamu wa hii biashara.
2. Mambo ya kuzingatia katika kuendesha biashara hii.
3. Ni anina gani Fuso ambayo ndo ina faa kwa biashara ya aina hii.
4. Modification zinazotakiwa kufanyika kwenye gari mara baada ya kununua na wapi zinafanyika.
5. Wapi nitapata gari zuri/ website/link au kwa mtu anayeuza hapa hapa nchini.
6. Return on Investiment ikoje.
7. Mengineyo

Asante sana
iMind

Mkuu kama upo hapa Dar nakushauri ununue Scania Mende za kubebea Mchanga au kokoto haina kupigwa Sound na Dereva au nini hesabu per day ni Ths 250,000 au km uwezo upo zaidi ninue kubwa zake Scania 114 c340 hiyo hesabu kwa siku ni Tsh 700,000.

Mi nasimamia shughuli za mzee ana Deal na Transportation ni hizi Semi Trailler zote ni Transit lakini Biashara za kwenda mbali ni kichefuchefu mkuu, Mungu akijaalia nataka kubadilisha zote ziwe Dar.
Tatizo la Biashara hizi ni kupigwa sound na Dereva kila siku mara mzigo umezidi mizani halafu saa nyingine unakuta gari imeharibikia nje au mkoani huko ni ngumu labda uwe na uwezo wa gari nyingi ambazo unakuwa na Patrol.
 
stata_mzuka ninayo scania tipper cm3 18 tatizo lake nyuma ni single diff japo lina tairi 8,lkn ni 4 tu zina operate je hili linaweza niletea how much per day,ila mchangani haiwezi
 
Last edited by a moderator:
Ukweli utabaki pale tu tiper zinalipa..nanirahisi kumanage ww mwenyewe hapo dar..mm mwenye niliwah kusimamia hapo dar
 
Natumai watu wenye kutoa ushauri wote wametoa ushauri na maangalizo mzuri.

Biashara hii inalipa asikudanganye mtu.

Mie mwanzo nili pick Idea ya Boda boda watu wakaponda sana humu na kusema watu wengie wanafanya na zimekuwa nyingi sana mjini hazina isssue na mambo tele,na wengine wakanipa moyo.

Na kuna Member mmoja aliniambia kwamba nianze na Bodaboda 3 ili niweze kuona faidi yake vizuri.
Mbali na vitisho vyoote nikaweka ndoto zangu na ilikuwa mwaka jana,mpaka sasa naendelea vizuri na heasbu nakula 50,000 kwa wiki kwa kila moja.

Nikaweka Carry 3 njiani nakula 20,000 kwa siku.
Changamoto ya gari ni kwamba tafuta Fundi wako maalum ambapo kila kitu atakuwa anashughulikia yeye.Na atakuwa anaijua gari A-Z.
Halafu toa pesa ufungiwe GPRS Car Truck System,mie nilitoa Laki 3 kwa kila Carry moja kwa mwaka.Na ninaweze ku access na kujua gari ipo wapi hata nikiwa huku Zanzibar.

Na kama unae kijana katika familia mwenye Idea ya ufundi jaribu kumpeleka chuo cha ufundi magari kama Veta ili awe msimamizi.Hili nimefanya na imefanikia.Services za Bodadboda na Carry zangu anashugulikia yeye.

Maana gari hilo ndani na mwaka linanunua gari jingine.
Kuna watu wanamiliki gari zaidi ya kumi na walianza na moja kama wewe mpaka wengine wameanzisha Kampuni za usafirishaji.
Na sio kila alieshindwa biashara basi wenzie wasifanye,we ukiacha na ukienda kule kwenye Usajili unakuta wenzio wanasajili magari hayo karibu kila siku.
Changamoto katika biashara ndio fursa kwako.

Kumbuka Mike Iron Tyson aliwahi kusema kwamba Mpira wa miguu ni mchezo hatari sana kuliko ngumi.
Sasa wacheza mpira walishangaa sana na kumuona kituko ila wacheza ngumi wakaona ni kweli.

Tafuta dereva mwenye Mdhamini mwenye mali iliyo sawa na Gari yako na pia ikatie Comprehensive insuarence.
Madereva wapo tele tu na wenywe sifa nzuri.
Pia usimbane sana,mwachie apige gozigozi ndogo za njiani ili yeye apate kidogo na wewe kidogo,kama alivyosema mdau hapo juu kwamba na yeye awe dalali kimtindo.

Umuhim wa Car Truck system ni mkubwa sana licha ya kwamba watu wengi wanaidharau ila matajiri wakubwa karibu wote Gari zao zimefungwa mfumo huu na ni kwamba Dereva atakuwa mkweli kwako kwa kiasi fulani.
Kwanza -
-Dereva akienda kasi itakuambia kwamba Driver wako yupo mwendo kasi
-Itakupa update ya ulaji wa mafuta wa gari yako
-Driver akisimama inakuambia na kukuonyesha
-Ikifika Km za kufanya Services ndogo itakuambia
nk.

mkuu nimeipenda hyo car track system nawezaje ipata? kama vipi naona tuwasiliana through kagwe75@gmail.com
 
Kampuni nyingi wanatoa huduma hii.
Ila wasiliana na huyu hapa chini,maana yeye anafunga hadi kwenye bodaboda,Magari madogo na Makubwa.na bei zake zipo chini sana.
Niliwahi kumuona ITV kipindi cha Asubuhi walikuwa wanahoji huduma zake.Is very Friendly Guy
Director:BENEDICT 0712-447423
 
Links nzuri yakupata gar nzuri embu waone hawahapa jf SOKWE pm him.anakampun yake japan nayy yuko huko.pia kun b4ward.
Ona vijana mnavyolemaa.
Hii b4ward, Uta-google hadi kesho kutwa Bila mafanikio.

Kampuni aliyomaanisha Jamaa inaandikwa
'Be forward'
 
Back
Top Bottom