Natumai watu wenye kutoa ushauri wote wametoa ushauri na maangalizo mzuri.
Biashara hii inalipa asikudanganye mtu.
Mie mwanzo nili pick Idea ya Boda boda watu wakaponda sana humu na kusema watu wengie wanafanya na zimekuwa nyingi sana mjini hazina isssue na mambo tele,na wengine wakanipa moyo.
Na kuna Member mmoja aliniambia kwamba nianze na Bodaboda 3 ili niweze kuona faidi yake vizuri.
Mbali na vitisho vyoote nikaweka ndoto zangu na ilikuwa mwaka jana,mpaka sasa naendelea vizuri na heasbu nakula 50,000 kwa wiki kwa kila moja.
Nikaweka Carry 3 njiani nakula 20,000 kwa siku.
Changamoto ya gari ni kwamba tafuta Fundi wako maalum ambapo kila kitu atakuwa anashughulikia yeye.Na atakuwa anaijua gari A-Z.
Halafu toa pesa ufungiwe GPRS Car Truck System,mie nilitoa Laki 3 kwa kila Carry moja kwa mwaka.Na ninaweze ku access na kujua gari ipo wapi hata nikiwa huku Zanzibar.
Na kama unae kijana katika familia mwenye Idea ya ufundi jaribu kumpeleka chuo cha ufundi magari kama Veta ili awe msimamizi.Hili nimefanya na imefanikia.Services za Bodadboda na Carry zangu anashugulikia yeye.
Maana gari hilo ndani na mwaka linanunua gari jingine.
Kuna watu wanamiliki gari zaidi ya kumi na walianza na moja kama wewe mpaka wengine wameanzisha Kampuni za usafirishaji.
Na sio kila alieshindwa biashara basi wenzie wasifanye,we ukiacha na ukienda kule kwenye Usajili unakuta wenzio wanasajili magari hayo karibu kila siku.
Changamoto katika biashara ndio fursa kwako.
Kumbuka Mike Iron Tyson aliwahi kusema kwamba Mpira wa miguu ni mchezo hatari sana kuliko ngumi.
Sasa wacheza mpira walishangaa sana na kumuona kituko ila wacheza ngumi wakaona ni kweli.
Tafuta dereva mwenye Mdhamini mwenye mali iliyo sawa na Gari yako na pia ikatie Comprehensive insuarence.
Madereva wapo tele tu na wenywe sifa nzuri.
Pia usimbane sana,mwachie apige gozigozi ndogo za njiani ili yeye apate kidogo na wewe kidogo,kama alivyosema mdau hapo juu kwamba na yeye awe dalali kimtindo.
Umuhim wa Car Truck system ni mkubwa sana licha ya kwamba watu wengi wanaidharau ila matajiri wakubwa karibu wote Gari zao zimefungwa mfumo huu na ni kwamba Dereva atakuwa mkweli kwako kwa kiasi fulani.
Kwanza -
-Dereva akienda kasi itakuambia kwamba Driver wako yupo mwendo kasi
-Itakupa update ya ulaji wa mafuta wa gari yako
-Driver akisimama inakuambia na kukuonyesha
-Ikifika Km za kufanya Services ndogo itakuambia
nk.