Kama alivyokushauri Zanzibar Spices hapo juu,ni biashara nzuri sana tu tatizo wengi wanasema pasua kichwa maana wanataka kununua Hiace Dungu kwa 7ml na wanategemea faida,Super roof injini 5L ambayo haina uchakavu ushuru wake ni almost 9.5ml mbali ya pesa ya kuinunua unaponunua kama ukiiagiza waambie watoe viti ili ushuru ushuke kidogo maana ikiwa na viti tax inaongezeka.Hiace nzuri kwa biashara inatakiwa kuwa Disel ambayo ni manual japo bei ipo juu,Petrol ambayo ni automatic ni cheap sokoni lakini si nzuri kibiashara,tafuta DUNGU nzuri kwa mtu kama bajeti yako si kubwa.Aksante.
Lucky Sabasaba,wewe najua ni mzoefu wa hii kazi.
Hembu mpe Bei ya gari kwa kuagiza na kununua hapa.Na je wewe ulinunua kwa Agent yupu,au Jamaa zako wa Dubai walikusaidia kuchagua na kutuma?
Hii itatuongoza sote,maana namie nakuja humohumo January mwakani.Maana bodaboda nimo,Carry nimo,sasa nataka nianglaie na huku kukoje,maana ninakaka yangu mmoja anakimeo cha Hiace hicho balaa,kila siku kinaenda ICU ya Garage ukimuambia akiuze anakuambia weee,acha utani hiki kimeo hakiishi Garage lakini kinaingiza pesa nzuri.Yupo anakula route nje ya mji.
Na kila siku ananiambia nunua Dungu inalipa.
Unajua kwa huku Zanzibar nakumbuka mara ya mwisho kuuliza mwaka jana ilikuwa 23m mpya kwetu used Japan.
Nakama ni ya kununua kwa mtu basi.
Iliyotumika kuanzia Miezi sita ni 18m - 22m
Mwaka 14m - 16m
Miaka Miwili 8m - 12m
Hembu tupe njia nzuri,maana sijawahi kuagiza gari kwa kuogopa,maana kuna watu huwa nawaona huku wanalia wakifika Bandarini,na wengine kwa hasira wanauza hapo hapo,maana kwenye Picha na iliyoletwa sio.Mie Carry nilinunua hapahapa.