Biashara ya Hiace Mwanza

Biashara ya Hiace Mwanza

Kwa ufupi usikatishwe tamaa,biashara hii nzuri,waache waoga wa maisha waendelee.
Kwanza inaonekana sio mgeni wa Gari,licha ya kwamba hii itakuwa ya Biashara.
Mie ningekushauri ununue hapahapa TZ sio kuagiza,maana mtaji mrefu,halafu kunamchezo wa kupeana vimeo kwenye gari hizo.
Muhim gari yoyoteni Services,na kupata Driver mzuri,unaweza kutafuta miongoni mwa Family members wako,au tafuta kijana mpeleke chuo kisha muajiri.Au toa Dau kama laki Tano au hata Milioni umchomoe Driver wa mtu umpe gari yako.
Ila siku ikitokea kwako uwe mpole
 
Kama alivyokushauri Zanzibar Spices hapo juu,ni biashara nzuri sana tu tatizo wengi wanasema pasua kichwa maana wanataka kununua Hiace Dungu kwa 7ml na wanategemea faida,Super roof injini 5L ambayo haina uchakavu ushuru wake ni almost 9.5ml mbali ya pesa ya kuinunua unaponunua kama ukiiagiza waambie watoe viti ili ushuru ushuke kidogo maana ikiwa na viti tax inaongezeka.Hiace nzuri kwa biashara inatakiwa kuwa Disel ambayo ni manual japo bei ipo juu,Petrol ambayo ni automatic ni cheap sokoni lakini si nzuri kibiashara,tafuta DUNGU nzuri kwa mtu kama bajeti yako si kubwa.Aksante.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kwenye magari najua tu kufanya service kwenye hizi sedan...vingine dah mi mweupe 100! Naskia ukiwa na dreva mzuri ni bizness nzuri Bzmana

gari litadumu na kibiashara utafanikiwa kama utapata dereva anayeidhamini hiyo gari yako kama ofisi yake na kama maisha yake, sio dereva viroba sana, anagawa sana daywaka, haripoti tatizo haraka pale linapojitokeza.
 
Last edited by a moderator:
Tangu mwanzo ungesema aku Pm tu,maana umezunguuka,sas aku pm kivipi.
Watu mkisikia hela basi mnambinu nyingi sana.
Kwa ufupi watu wanatabia ya kutishana kwenye hii biashara,wakati ukienda Yard na Japan watu kila siku wanaingiza gari njiani.Mke tu ana Stress itakuwa chuma kisichosema.
Acha uoga wa Maisha.Jizake mwanaume.

nia yangu nikumpa mwongozo, sio pesa zake...
 
Ukipata Gari njoo nikupe dereva yeye ni fundi wa magari pia,ukimpata huyo ndoto zako zitatimia.kila la kheri
 
Kama alivyokushauri Zanzibar Spices hapo juu,ni biashara nzuri sana tu tatizo wengi wanasema pasua kichwa maana wanataka kununua Hiace Dungu kwa 7ml na wanategemea faida,Super roof injini 5L ambayo haina uchakavu ushuru wake ni almost 9.5ml mbali ya pesa ya kuinunua unaponunua kama ukiiagiza waambie watoe viti ili ushuru ushuke kidogo maana ikiwa na viti tax inaongezeka.Hiace nzuri kwa biashara inatakiwa kuwa Disel ambayo ni manual japo bei ipo juu,Petrol ambayo ni automatic ni cheap sokoni lakini si nzuri kibiashara,tafuta DUNGU nzuri kwa mtu kama bajeti yako si kubwa.Aksante.
Lucky Sabasaba,wewe najua ni mzoefu wa hii kazi.
Hembu mpe Bei ya gari kwa kuagiza na kununua hapa.Na je wewe ulinunua kwa Agent yupu,au Jamaa zako wa Dubai walikusaidia kuchagua na kutuma?
Hii itatuongoza sote,maana namie nakuja humohumo January mwakani.Maana bodaboda nimo,Carry nimo,sasa nataka nianglaie na huku kukoje,maana ninakaka yangu mmoja anakimeo cha Hiace hicho balaa,kila siku kinaenda ICU ya Garage ukimuambia akiuze anakuambia weee,acha utani hiki kimeo hakiishi Garage lakini kinaingiza pesa nzuri.Yupo anakula route nje ya mji.
Na kila siku ananiambia nunua Dungu inalipa.

Unajua kwa huku Zanzibar nakumbuka mara ya mwisho kuuliza mwaka jana ilikuwa 23m mpya kwetu used Japan.
Nakama ni ya kununua kwa mtu basi.
Iliyotumika kuanzia Miezi sita ni 18m - 22m
Mwaka 14m - 16m
Miaka Miwili 8m - 12m

Hembu tupe njia nzuri,maana sijawahi kuagiza gari kwa kuogopa,maana kuna watu huwa nawaona huku wanalia wakifika Bandarini,na wengine kwa hasira wanauza hapo hapo,maana kwenye Picha na iliyoletwa sio.Mie Carry nilinunua hapahapa.
 
Wataalamu wa Biashara kama hizi wanatumia njia moja tu.., wananunua gari ingawa used ila ipo katika hali nzuri sana preferably hata injini haijafunguliwa.., wanaifanyia kazi ikirudisha pesa tu wanauza na kuleta nyingine..

Kwa kufanya hivyo wanaepukana na headaches zinazoletwa na gari ikishaanza kuharibika haribika.., gari ikishachoka usishangae badala ya kukuingia ikawa inakutoa.., ukichangaya na uongo wa madereva wakishaona gari ni bovu kila siku itakuwa ni hadithi za traffic alinishika na gari imeua hiki au kile
 
Ni kweli gari unakaa nayo kwa mda fulani kabda ya kuanza matatizo makubwa,ukinunua nzuri wawezakaa nayo ata miaka miwili bila serious problem.Pia unatakiwa iwe clear (lipia kila kitu Bima,Sumatra etc )ili kumnyima dereva nafasi ya kusema leo nimeshikwa sina bima,fire ex etc.Ni biashara nzuri sana kama utapata gari zuri na msimamizi mzuri.
 
Ahsante mkuu, wasalimie huko kwenye marashi ya karafuu
Nasubiri kujua bei ya kununua hiace hapa Tanzania na kuagiza nje

Ram,leu umeongea la maana sana,kitufe cha LIKE kimejifuta, hembu chukua :busu
 
Lucky Sabasaba,bado hujatujibu mie na RAM hapo juu

Kuagiza yataka maandalizi kama nilivyokwambia ushuru wake pia upo juu,mfano 5L manual Disel ya mwaka 2004 mpaka kuitoa lazima uwe na 21Ml,kwa iliyotumika Tz ambayo haijachezewa injini lakini imefanya kazi kidogo wawezaipata kwa 17ml.Kadri bei inavyopungua ndio unapata lililochoka.
 
Asante Lucky 77.
Wewe ulinunua kwa Agent yupi na clearance ulifanya kwa Agent yupi and how long does it take kufika Bongoland.
 
Asante Lucky 77.
Wewe ulinunua kwa Agent yupi na clearance ulifanya kwa Agent yupi and how long does it take kufika Bongoland.

Mimi niliichukulia hapa Dubai ndani ya siku 10 ilikuwa Bongo,kwa Japan yawezachukua wiki 3 inategemea kama Shipping agent akipata meli ya moja kwa moja.Lakini kikubwa wakati wa kununua toa viti ili kushusha ushuru.
 
Ok,kuna kampuni yenye mtandao wa Magari kwa hapo Dubai?Ili tuwe tunatupia macho
Maana wengi huagiza tu na kutumiwa picha.
Na kwa uelewa wako,tofauti ya Gari kuagiza Japan na Dubai ni upi?
 
Duh! Ndio technologia ilikofikia kwetu? Kwanini msiwashauri Wajapan watoe thermostat? Maneno ya kuambiwa bwana... Unabeba kama ulivyodanganywa...

ni kitu kidogo sana haina haja ya kusema wao wakitoe unakitoa hata dakika 10 haizidi
 
Back
Top Bottom