Biashara ya Insurance Agency

Biashara ya Insurance Agency

moreen mollo

Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
15
Reaction score
8
Habari za mahangaiko ya kila siku wana JamiiForums na wapenzi wa jukwaa la Biashara na Ujasiriamali.

Nimekuja kwenu kuomba ushauri na sitaki kuwachosha, naenda moja kwa moja kwenye mada.

Ninafikiria kufanya biashara ya kuwa na ofisi ya kukata Bima za aina mbalimbali pamoja na Huduma ya LATRA.. Lakini nimekosa muongozo na kujua kipi kinahitajika, ninaomba muongozo wenu wadau. 🙏 🙏

Natanguliza shukurani zangu.
 
Umesoma insurance ?kama haujasoma tafuta mtu aliyesoma ,utatumia cheti chake wakati wa usajili,utaamua uwe naye au utumie umlipe utumie cheti chake ,Kisha utaenda kwenye kampuni husika unavyotaka uwe agent wao,milembe ,,bumaco n.k.watakupa form zao utajaza na hatua zingine watakuelekeza
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako...Je naweza kuwa na Kampuni tofauti tofauti za Bima ndani ya Ofisi moja?
 
Ili ufungue uwakala wa bima inabidi ufanye yafuatayo:-

. sajili jina BRELA
. uwe na cheti cha bima
. fixed deposit ya Tshs 1,000,000/=
. C.V ya principal officer wako
. uhakiki wa uraia wa mkurugenzi wa wakala na principal officer wako aidha kwa kuwa na cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria
. ukate bima ya proffessional indemnity
. uwe na mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi na kampuni husika ya bima
. uthibitisho wa kutokuwa na hatia wa mkurugenzi na principal officer

Hivyo vitu ukimalizana navyo unaenda TIRA unalipia:-

application form Tshs 25,000/=
registration fee Tshs 500,000/=
annual fee Tshs 50,000
 
Ahsante sana nimekuelewa [emoji120]
 
Insurance agency unatakiwa kuwa wakala wa kampuni moja kama nakumbuka vizuri .... Insurance broker ndio anaweza kuwa wakala wa kampuni ya bima zaidi ya moja.
 
Pia Kuna TIN Namba, leseni ya municipal.... Utatakiwa kufungua Account ya insurance agency yako bank.
 
Back
Top Bottom