Biashara ya korosho

Biashara ya korosho

Pate_15

Senior Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
156
Reaction score
48
Wapendwa wana jf, habari zenu!
Naomba kufaham bei ya korosho zilizo banguliwa (nuts) kwa kilo moja ni shiling ngapi hapa dar...bei ya jumla na rejareja.

=============================================================================

isack raphael pamoja na kukosa jibu kwenye swali lako hapa JF kwa mwaka mzima, kama hukufaidikiwa pia kupitia vyanzo vingine, hii taarifa mpya itakusaidia

korosho.jpg

Korosho
Na Abdallah Bakari, Mwananchi

Posted Ijumaa,Decemba5 2014 saa 14:18 PM
KWA UFUPI
Akizungumza jana ofisini kwake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini (CBT), Mfaume Juma amesema, mwenendo wa bei katika minada ya Novemba 17 hadi 30 umeonyesha kupanda.

Mtwara. Bei ya korosho ghafi katika soko la minada chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani imeimairika na kufikia Sh1,660 kutoka Sh1,500 kwa kilo katika wiki mbili zilizopita.

Akizungumza jana ofisini kwake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini (CBT), Mfaume Juma amesema, mwenendo wa bei katika minada ya Novemba 17 hadi 30 umeonyesha kupanda.

Tofauti na minada ya awali, bei ilionyesha kushuka kwa kufikia Sh1,500 kwa kilo, hizi wiki mbili bei imepanda alisema Juma na kuongeza;

Kuimarika kwa bei kunatokana na wanunuzi kubaini uhakika wa ubora wa korosho zinazopitia mfumo wa stakabadhi ghalani...pia kutekelezwa kwa makubaliano ya matumizi rafiki ya bandari ya Mtwara, meli za kubeba korosho zimeshaanza kuwasili.

Alisema jumla ya tani 139,123.77 za korosho ghafi zimekusanywa ikiwa ni ongezeko la tani 9,000 la korosho zilizokusanywa katika msimu uliopita hali inayoashiria kuongezeka kwa uzalishaji wa zao hilo.

Msimu 2013/14 tulikusanya jumla ya tani 130,123.77 kiasi hiki kimeongezeka katika msimu huu na hadi sasa tumekusanya tani 139,123.77...bado wakulima wanazo korosho na ukusanyaji unaendelea hii ni dalili njema kwetu.

Mkurugenzi huyo alisema pamoja na mafanikio hayo changamoto inayowakabili wakulima ni kulinda ubora wa korosho zao wakati wa kuhifadhi.

Katika wiki mbili zilizopita tumebaini kupungua kidogo kwa ubora wa korosho kunakosababishwa na baadhi ya wakulima kuweka korosho katika viroba kabla ya kuzipeleka kwenye vyama vya msingi ...viroba vinatunza joto, korosho zinapoteza unyevu ni vyema wakahifadhi kwenye magunia. ya katani au juti alisisistiza Juma

Source: Stakabadhi ghalani yapaisha bei ya korosho Mtwara
 
isack raphael pamoja na kukosa jibu kwenye swali lako hapa JF kwa mwaka mzima, kama hukufaidikiwa pia kupitia vyanzo vingine, hii taarifa mpya itakusaidia

korosho.jpg
Korosho
Na Abdallah Bakari, Mwananchi

Posted Ijumaa,Decemba5 2014 saa 14:18 PM

KWA UFUPI
Akizungumza jana ofisini kwake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini (CBT), Mfaume Juma amesema, mwenendo wa bei katika minada ya Novemba 17 hadi 30 umeonyesha kupanda.

Mtwara. Bei ya korosho ghafi katika soko la minada chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani imeimairika na kufikia Sh1,660 kutoka Sh1,500 kwa kilo katika wiki mbili zilizopita.

Akizungumza jana ofisini kwake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini (CBT), Mfaume Juma amesema, mwenendo wa bei katika minada ya Novemba 17 hadi 30 umeonyesha kupanda.

“Tofauti na minada ya awali, bei ilionyesha kushuka kwa kufikia Sh1,500 kwa kilo, hizi wiki mbili bei imepanda ” alisema Juma na kuongeza;

“Kuimarika kwa bei kunatokana na wanunuzi kubaini uhakika wa ubora wa korosho zinazopitia mfumo wa stakabadhi ghalani...pia kutekelezwa kwa makubaliano ya matumizi rafiki ya bandari ya Mtwara, meli za kubeba korosho zimeshaanza kuwasili.”

Alisema jumla ya tani 139,123.77 za korosho ghafi zimekusanywa ikiwa ni ongezeko la tani 9,000 la korosho zilizokusanywa katika msimu uliopita hali inayoashiria kuongezeka kwa uzalishaji wa zao hilo.

“Msimu 2013/14 tulikusanya jumla ya tani 130,123.77 kiasi hiki kimeongezeka katika msimu huu na hadi sasa tumekusanya tani 139,123.77...bado wakulima wanazo korosho na ukusanyaji unaendelea hii ni dalili njema kwetu.”

Mkurugenzi huyo alisema pamoja na mafanikio hayo changamoto inayowakabili wakulima ni kulinda ubora wa korosho zao wakati wa kuhifadhi.

“Katika wiki mbili zilizopita tumebaini kupungua kidogo kwa ubora wa korosho kunakosababishwa na baadhi ya wakulima kuweka korosho katika viroba kabla ya kuzipeleka kwenye vyama vya msingi ...viroba vinatunza joto, korosho zinapoteza unyevu ni vyema wakahifadhi kwenye magunia.” ya katani au juti” alisisistiza Juma

Source: http://www.mwananchi.co.tz/kitaifa/Stakabadhi-ghalani-yapaisha-bei-ya-korosho-/-/1597568/2545840/-/12xrgk0/-/index.html

Hi Wapendwa! Nafanya biashara ya korosho zilizo tayari kuliwa yaani ambazo hazina maganda - cashewnuts- Zenye ubora wa hali juu sana- zipo zilikuwa packed au ukipenda unaweza pack mwenyewe ; Tshs 20,000 kwa kilo; kwa mwenye mahitaji au anayefahamu soko wahitaji ndani na nje ya Tanzania; nb kwa atayenipatia soko kuna commission au tunaweza kuwa pamoja kwa makubaliano kama partiners; asante; below is the samples!
1470396465484.jpg
1470396477546.jpg
1470396487170.jpg
1470396497131.jpg
1470396510491.jpg
1470396525062.jpg
1470396536396.jpg
1470396544169.jpg
1470396565516.jpg
1470396593372.jpg
 
Hii picha ya huyu msanii nimeingiza kimakosa my no 0716 201695 thx
 
OK hizi picha zote zipo kwenye gallery ya whattsapp Wakati naselect nikagusa na hii picha jamaa alinitumia Wakati alifariki kuniambia; nimeshindwa kudelete ila ninamaanisha nilichopost am honest mi siyo muhuni asante
 
homehome boy wa kunyumba km nataka za kupaki mwenyewe una uzaje kwa kilo? uko wapi dar? masasi au mtwara?
 
Wewe nae bhana. Sasa kwanini huondoi hiyo picha ya marehemu hapo?!!!

-Kaveli-
 
Wadau, nahitaji kujua bei za korosho ili ninunue kwa wingi, naomba wahusika wa biashara hii tuanze michakato.
 
Msimu wa Korosho unaanza mwez wa 9 or 10. Mwaka jana kilo 1 ya korosho iliuzwa ghalani Tshs 3500/-. Kwa hali ilivyo mwaka huu ni ngumu sana kuuza/kununua Korosho kweny Kangomba/mtaani
Korosho zote zitauzwa ghalani
 
Kwa taarifa yako,safari hii kangomba itashamiri mno kuliko msimu uliopita.
Utaratibu wa malipo wa msimu uliopita umewaumiza mno wakulima....wengi wao wamefulia mno kipindi hiki cha maandalizi na kuhudumia mikorosho.... Watu wanakula maua
 
Msimu wa Korosho unaanza mwez wa 9 or 10. Mwaka jana kilo 1 ya korosho iliuzwa ghalani Tshs 3500/-. Kwa hali ilivyo mwaka huu ni ngumu sana kuuza/kununua Korosho kweny Kangomba/mtaani
Korosho zote zitauzwa ghalani
Wapi nitapata mkuu
 
Back
Top Bottom