Biashara mzuri Sana Ila uaminifu ni muhimu saana ni rahis Sana mtu kukudhurumu Kwa style hiyo na huna pakwenda kumshitaki Kwasababu serikali inakataza ununuaji wa style hiyo na mwaka Jana watu wamekamatwa Sana, ni biashara ambayo unapata faida kubwa mno ni zaidi Ya Mara tatu, binafsi nimeifanya mwaka Jana, Ila changamoto Kwa mgeni unapokuja kununua vijijin ni rahisi Sana kukamatwa na dola tofaut na mwenyeji, Ukikamatwa haufungwi ni rushwa tu laki moja had million Inategemea na mzigo ulio nao,
Mtoa Mada weka na hizo changamoto, usiweke faida tuu, binafsi Mwaka Jana kuna watu wamenipiga Sana Japo ni mwenyej wa kijiji husika Ila nimepigwa changa Sana afu Kwa mtu unayemjua...
Kwa mfano inakua Hivi : Umempa mtu kiasi cha laki 5 thaman Ya kilo mia 5 Kwa bei ya 1000 , wewe haupo Karibu Kwa Kuogopa kukamatwa, anachofanya yeye Anaenda kupeleka ghalani ,anakupigia Simu boss nishapima Teyari, anakuletea cheti kinachoonyesha kg 500 Kumbe si kg 500 ni kg 50 , alichofanya ni kuongeza sifuri mbele Ila kg halali ni 50 , Kwa hiyo basi Umakini unahitajika, Japo kuna faida Ya haramu Ila kuna hasara zake, ukimpata mtu mwaminifu ni msimu wako mmoja tu unatoka kimaisha kutokana na mtaji wako.
Sent using
Jamii Forums mobile app