Biashara ya korosho

Biashara ya korosho

Kwa taarifa yako,safari hii kangomba itashamiri mno kuliko msimu uliopita.
Utaratibu wa malipo wa msimu uliopita umewaumiza mno wakulima....wengi wao wamefulia mno kipindi hiki cha maandalizi na kuhudumia mikorosho.... Watu wanakula maua
Kwa wakati huu, uwezekano wa kupata upo?
 
Kwa wakati huu kupata sio rahisi kiongozi,labda kuanzia mwezi September coz kuna maeneo mavuno yanawahi mno.

More nicheck PM,ndo biashara yangu hii kila msimu
 
Habari wakuu humu.
Ninahitaji kuwa wakala Wa kampuni zinahusika na ununuzi Wa korosho Wa Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kampuni zinazotaka kununua korosho kwa msimu Wa 2017/2018 kwenye mikoa hiyo please tuwasiliane niwafanyie kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikitaka kufanya hiyo biashara naweza anza n'a mtaji kiasi gani
OK,, mtaji ni wewe mwenyewe nguvu zako tu,mtaji mkubwa faida kubwa.So mtaji inaweza kuwa hata laki tano na mpaka billion kadhaa.

Biashara iko hivi:Kipindi msimu unaanza wakulima (tulio wengi) huwa hatuna hata ela ya kununua chumvi halafu kipindi hiki ni kipindi ambacho cha kuokota na kuziweka ili zipelekwe ghalani kwa ajili ya mauzo.Wakulima wanakuwa bize sana kwenye kazi za shamba wakati hakuna ela wanayoingiza.

Hivyo,kwakuwa hali ya uchumi inakuwa ngumu sana kwa kipindi hiki,baadhi hugawa sehemu ya kipato chao huuza nje ya utaratibu Wa Mnada kwa watu wenye ela.Mkulima atakujia atakuambia Nina gunia zangu mbili pale Nina shida ya ela nisaidie.Wewe ukiwa na ela unampa anakupa mzigo.

Kwa mfano Ikiwa umenunua kila kilo kwa Tsh.1300/=,
Ule mzigo wewe ukipeleka mnadani utauza kwa Tsh.3500,utakuwa umepata faida ya sh.2200.

Na kwakutumia mfumo Wa mnada ela haziji haraka kwa wakulima,mfano mkulima amepeleka mwezi Wa kumi sokoni korosho zake lakini mpaka mwezi Wa kumi na moja bado hajapewa ela zake.Kwahiyo mwezi mmoja mkulima hana ela hata kama amepeleka mapema.Hivyo basi watu huuza sana chomachoma.

Na kama mkulima akauza mapema sana mzigo wake na akapata ela kwa wakati anao uwezo Wa kuizungusha hata Mara tatu au tano mpaka msimu unaisha.Kwahiyo ukianza na mtaji Wa kueleweka mpaka unaishia msimu utakuwa umezungusha sana ela yako kwa manufaa.
 
dah;!nmekuelewa sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara mzuri Sana Ila uaminifu ni muhimu saana ni rahis Sana mtu kukudhurumu Kwa style hiyo na huna pakwenda kumshitaki Kwasababu serikali inakataza ununuaji wa style hiyo na mwaka Jana watu wamekamatwa Sana, ni biashara ambayo unapata faida kubwa mno ni zaidi Ya Mara tatu, binafsi nimeifanya mwaka Jana, Ila changamoto Kwa mgeni unapokuja kununua vijijin ni rahisi Sana kukamatwa na dola tofaut na mwenyeji, Ukikamatwa haufungwi ni rushwa tu laki moja had million Inategemea na mzigo ulio nao,

Mtoa Mada weka na hizo changamoto, usiweke faida tuu, binafsi Mwaka Jana kuna watu wamenipiga Sana Japo ni mwenyej wa kijiji husika Ila nimepigwa changa Sana afu Kwa mtu unayemjua...

Kwa mfano inakua Hivi : Umempa mtu kiasi cha laki 5 thaman Ya kilo mia 5 Kwa bei ya 1000 , wewe haupo Karibu Kwa Kuogopa kukamatwa, anachofanya yeye Anaenda kupeleka ghalani ,anakupigia Simu boss nishapima Teyari, anakuletea cheti kinachoonyesha kg 500 Kumbe si kg 500 ni kg 50 , alichofanya ni kuongeza sifuri mbele Ila kg halali ni 50 , Kwa hiyo basi Umakini unahitajika, Japo kuna faida Ya haramu Ila kuna hasara zake, ukimpata mtu mwaminifu ni msimu wako mmoja tu unatoka kimaisha kutokana na mtaji wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu humu.
Ninahitaji kuwa wakala Wa kampuni zinahusika na ununuzi Wa korosho Wa Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kampuni zinazotaka kununua korosho kwa msimu Wa 2017/2018 kwenye mikoa hiyo please tuwasiliane niwafanyie kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unanunulia wapi korosho, Mi nitaenda kununua vijiji vya masasi kama Rivango na Mapili. wewe je?
 
Biashara mzuri Sana Ila uaminifu ni muhimu saana ni rahis Sana mtu kukudhurumu Kwa style hiyo na huna pakwenda kumshitaki Kwasababu serikali inakataza ununuaji wa style hiyo na mwaka Jana watu wamekamatwa Sana, ni biashara ambayo unapata faida kubwa mno ni zaidi Ya Mara tatu, binafsi nimeifanya mwaka Jana, Ila changamoto Kwa mgeni unapokuja kununua vijijin ni rahisi Sana kukamatwa na dola tofaut na mwenyeji, Ukikamatwa haufungwi ni rushwa tu laki moja had million Inategemea na mzigo ulio nao,

Mtoa Mada weka na hizo changamoto, usiweke faida tuu, binafsi Mwaka Jana kuna watu wamenipiga Sana Japo ni mwenyej wa kijiji husika Ila nimepigwa changa Sana afu Kwa mtu unayemjua...

Kwa mfano inakua Hivi : Umempa mtu kiasi cha laki 5 thaman Ya kilo mia 5 Kwa bei ya 1000 , wewe haupo Karibu Kwa Kuogopa kukamatwa, anachofanya yeye Anaenda kupeleka ghalani ,anakupigia Simu boss nishapima Teyari, anakuletea cheti kinachoonyesha kg 500 Kumbe si kg 500 ni kg 50 , alichofanya ni kuongeza sifuri mbele Ila kg halali ni 50 , Kwa hiyo basi Umakini unahitajika, Japo kuna faida Ya haramu Ila kuna hasara zake, ukimpata mtu mwaminifu ni msimu wako mmoja tu unatoka kimaisha kutokana na mtaji wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mgeni changamoto hizo lazima,,,,Ila kwa Mimi ninapoishi sitopata changamoto hiyo kutoka sehemu yoyote...So watu kama wapo humu watafute mwaminifu na Wa eneo husika

Mkuu habari, naomba unijuze. Sina mtaji mkubwa nahitaji kilo 150 tu. Kwa zilizochakatwa tayari au kuondolewa maganda. Je kilo huwa bei gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom