Kwa ufupi usijisumbue...Kama unanunua angalia selling rate na kama utakuwa na fedha za kigeni kwa ajili ya kuuza angalia Buying rate.
Inaonekana ni kinyume lakini ndio lugha yenyewe.
Wewe ukiwa na tuseme USD unataka kuuza, Benki/Duka la fedha (Bureax de Change) linanunua hizo USD hivyo watatumia Buying Rate ambayo ni ndogo kununua hizo USD zako. Ukiwa unataka kununua USD Benk inakuuzia hivyo itatumia selling rate ambayo ni kubwa.
Mfano halisi.. hii ni quotation nimeichukua kwenye website ya CRDB leo
| CURRENCY | CODE | BUYING | SELLING |
| US$ 50-100 Units | USD | 1,535.0000 | 1,625.0000 |
Sasa, tuseme leo hii una TZS 1,625,000 ukanunua USD 1,000. Kesho ukitaka kuuza kama bei haijabadirika, utauza kwa buying rate maana benki/Bureux itakuwa inanunua kutoka kwako. Hivyo utapata TZS 1,535,000 na kupoteza TZS 90,000. Hivyo ndivyo mabenki na maduka ya fedha wanavyopata faida.
Sasa kwa nini wao wanafanya hii biashara?
· Wao wameruhusiwa kisheria kufanya hiyo biashara. Mtu binafsi huruhusiwi kununua fedha za kigeni kama huna sababu maalum. Kwa benki watahitaji vithibitisho, bureau de change wao taratibu haziwabani sana, watakuuzia japo nao wanatakiwa waombe vithibitisho.
· Wana wigo mpana wa kupata fedha za kigeni kwa bei nafuu. Wananunua fedha kwa bei ndogo kutoka kwa umma na kuuza kwa bei kubwa (angalia tofauti ya buying-selling).
· Wao ni member wa foreign exchange market..soko la fedha hivyo wanao uwezo wa kuagiza na kununua fedha kutoka nje. Mfano halisi ni kwamba fedha za kigeni benki ununua kutoka kwenye mabenki washirika ya nje pesa husika inakotoka. Mfano USD kutoka USA, au GBP kutoka UK.
· Kwa mtu binafsi labda ununue fedha hizi kinyemela ‘black market' kama mipakani wanavyofanya, na baadhi ya wahindi na kuuza kwenye mabenki. Ila niseme watu binafsi ambao hawajasajiriwa ni makosa kufanya biashara hii, serikali inafumba macho tu amabpo inahona hakuna huduma, lakini hairuhusiwi. Pia kama ni mtu wa safari unaweza kuwa unakuja na fedha za kigeni na kiasi na kubadirishia hapa. Kwa hili nisisitize kwamba inabidi uwe mwangalifu kwani kuna nchi ambazo pesa yetu TZS haijulikani au inajulikana lakini haina thamani hivyo unaweza kujikuta unakula hasara.
· Mwisho unaweza kujifunza taratibu juu ya mwenendo wa bei za fesha na kujua ni wakati gani fedha fulani inashuka na wakati gani inapanda. Kwa hili ni vigumu kukueleza kwa ufupi, lakini hapa hakuna nadharia. Mambo mengine ni ujanja na umakini wa mtu, lakini masoko pengine hayatabiriki. Mfano, mwishoni mwa 2011 USD ilipanda mpaka TZS 1840/USD. Mwaka 2012 imeshuka na kuanza kupanda tena, ; leo tunaona 1532-1525. Hivyo ukipiga hesabu zako vibaya, unaweza kuliwa big time.
Mwisho,kama umeipenda hii biashara tafuta mtaji jiunge na marafiki mfungue Bureaux de Change. Mtaji ni mdogo tu , TZS 40M kwa mujibu wa BOT.
Kuna mambo mengi juu ya hii ni elimu, hapa nimejaribu kutoa japo dondoo. Kila la heri!