Biashara ya kubadilisha fedha za kigeni, share your experience

Biashara ya kubadilisha fedha za kigeni, share your experience

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,407
Reaction score
3,260
Wakuu kwa muda sasa limekuwa lina nijia wazo la kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kucheza na rates za maduka ya kubadilishia fedha na mabank

Sina maana ya kuanzisha Bureau De change HAPANA, hapa nawaza inawezekana kama nina mtaji wangu kuwa nacheck na rate za maduka yote ya kubadilishia fedha na mabank kwa siku na kisha kwenda kununua kwenye rate ndogo na kwenda kuuza kwa rate nzuri?.................

Najua humu kuna wataalamu wa kila fani naweza kupata ideas kama inawezekana na inafanyikaje au ni kitu haiwezekani
Msinishangae jamani najaribu kufikiri namna ya kujijasiliamari maana hizi ajira sasa tumekuwa watumwa tunafaidisha waajiri tu

Karibuni kwa mjadala
 
Hiyo bzn mbona kama ni ngumu kidogo! maana source za exchange zinazotumiwa ni moja.nakkama kuna tofauti ni ndogo mno kuwa wewe kupata faida.Usisahau pia kama ni dola zinatofautiana kulingana na denomination zake! sijaona mtu akifanya hiyo ishu Bila duka la fedha, labda kubadilisha kwa kutumia black market.Au waje watu waliobobea kwa mambo yafedha watufafanulie namimi nidese hapo!
 
Kwa ufupi usijisumbue...Kama unanunua angalia selling rate na kama utakuwa na fedha za kigeni kwa ajili ya kuuza angalia Buying rate.

Inaonekana ni kinyume lakini ndio lugha yenyewe.

Wewe ukiwa na tuseme USD unataka kuuza, Benki/Duka la fedha linanunua hizo USD hivyo watatumia Buying Rate ambayo ni ndogo kununua hizo USD zako. Ukiwa unataka kununua USD Benk inakuuzia hivyo itatumia selling rate ambayo ni kubwa.
 
idea nzuri ila inaitaji capital kubwa kidogo maana utakuwa unapata vi percentage kidogo,so ukiwa na hela nyingi it pays,kuna risk pia mkuu,pia inabidi uwe na source nzuri za info,mjini hapa matapeli wengi!!
Gud luck
 
Biashara nzuri sana. Ila inatakiwa uwe na Euros au Dollars nyingi benki.
Kizuri zaidi, badala ya kununua dollars kwa kutumia madafu na kuziuza bei inapopanda, ni vizuri kununua dhahabu na kuweza kuzibadilisha kwa sarafu itayopanda ... eg sometimes Yen hupanda against Euro, au dollars hupanda against Yen bila kuathiri sana exchange btn euro na dollar.
Basically, precious metals kwa sasa hivi zipo more stable than paper money ... u can use'em to make a lot of dough depending on tax policies za bongo na restrictions kuhusu hizo metals.
 
Kwa ufupi usijisumbue...Kama unanunua angalia selling rate na kama utakuwa na fedha za kigeni kwa ajili ya kuuza angalia Buying rate.

Inaonekana ni kinyume lakini ndio lugha yenyewe.

Wewe ukiwa na tuseme USD unataka kuuza, Benki/Duka la fedha (Bureax de Change) linanunua hizo USD hivyo watatumia Buying Rate ambayo ni ndogo kununua hizo USD zako. Ukiwa unataka kununua USD Benk inakuuzia hivyo itatumia selling rate ambayo ni kubwa.

Mfano halisi.. hii ni quotation nimeichukua kwenye website ya CRDB leo
CURRENCY CODE BUYING SELLING
US$ 50-100 UnitsUSD1,535.00001,625.0000

Sasa, tuseme leo hii una TZS 1,625,000 ukanunua USD 1,000. Kesho ukitaka kuuza kama bei haijabadirika, utauza kwa buying rate maana benki/Bureux itakuwa inanunua kutoka kwako. Hivyo utapata TZS 1,535,000 na kupoteza TZS 90,000. Hivyo ndivyo mabenki na maduka ya fedha wanavyopata faida.

Sasa kwa nini wao wanafanya hii biashara?

· Wao wameruhusiwa kisheria kufanya hiyo biashara. Mtu binafsi huruhusiwi kununua fedha za kigeni kama huna sababu maalum. Kwa benki watahitaji vithibitisho, bureau de change wao taratibu haziwabani sana, watakuuzia japo nao wanatakiwa waombe vithibitisho.

· Wana wigo mpana wa kupata fedha za kigeni kwa bei nafuu. Wananunua fedha kwa bei ndogo kutoka kwa umma na kuuza kwa bei kubwa (angalia tofauti ya buying-selling).

· Wao ni member wa foreign exchange market..soko la fedha hivyo wanao uwezo wa kuagiza na kununua fedha kutoka nje. Mfano halisi ni kwamba fedha za kigeni benki ununua kutoka kwenye mabenki washirika ya nje pesa husika inakotoka. Mfano USD kutoka USA, au GBP kutoka UK.

· Kwa mtu binafsi labda ununue fedha hizi kinyemela ‘black market' kama mipakani wanavyofanya, na baadhi ya wahindi na kuuza kwenye mabenki. Ila niseme watu binafsi ambao hawajasajiriwa ni makosa kufanya biashara hii, serikali inafumba macho tu amabpo inahona hakuna huduma, lakini hairuhusiwi. Pia kama ni mtu wa safari unaweza kuwa unakuja na fedha za kigeni na kiasi na kubadirishia hapa. Kwa hili nisisitize kwamba inabidi uwe mwangalifu kwani kuna nchi ambazo pesa yetu TZS haijulikani au inajulikana lakini haina thamani hivyo unaweza kujikuta unakula hasara.

· Mwisho unaweza kujifunza taratibu juu ya mwenendo wa bei za fesha na kujua ni wakati gani fedha fulani inashuka na wakati gani inapanda. Kwa hili ni vigumu kukueleza kwa ufupi, lakini hapa hakuna nadharia. Mambo mengine ni ujanja na umakini wa mtu, lakini masoko pengine hayatabiriki. Mfano, mwishoni mwa 2011 USD ilipanda mpaka TZS 1840/USD. Mwaka 2012 imeshuka na kuanza kupanda tena, ; leo tunaona 1532-1525. Hivyo ukipiga hesabu zako vibaya, unaweza kuliwa big time.

Mwisho,kama umeipenda hii biashara tafuta mtaji jiunge na marafiki mfungue Bureaux de Change. Mtaji ni mdogo tu , TZS 40M kwa mujibu wa BOT.

Kuna mambo mengi juu ya hii ni elimu, hapa nimejaribu kutoa japo dondoo. Kila la heri!
 
hii ni sawa sawa na kununua bidhaa kwa bei ya rejareja na kwenda kuuza kwa bei ya jumla
 
Wewe kama individual kununua foreign currency benki au kwenye duka (bureau de change) unahitaji kuwa na supporting documents kama invoice au passport na visa kwa ajili ya safari. Sasa wewe kwa biashara huwezi kuwa na vitu hivi kwahiyo benki kukuuzia kama individual kuna changamoto kidogo.Unless kama unataka kufanya kama illegal business uwe mjanja mjanja.
 
Mkuu hii biashara ni ngumu sana, ila inalipa kama utafanya exchange kati ya nchi mbili, e.g kenya na tz, thamani ya dola kwetu mathalani iko juu, ila kwa kenye yaweza kuwa chini kidogo, so hapo utapata faida.

Ila biashara nzuri isiyotaka jasho ni ya HISA, ila uwe na fedha za kutosha, una nunua hisa mathalani za TBL kwa 2300, hisa 100,000 (230,000,000) kesho ikipanda kwa shilingi mia unauza zote 2400 (240,000,000).

Hii biashara pia huleta faida ndogo kama unawekeza mtaji mdogo, ila ni nzuri pia, kuna matajiri kama Marekani hasa pale NYSE ndio vijiwe vyao, daily wako hapo.
 
Risk ni kubwa pia faida ni kubwa vile vile kikubwa uwe na mtaji,uwe na akili ya haraka uwe na network nzuri ya wateja wa black market na uwe na urafiki na wafanyakazi wa bank utatoka tena sana ni biashara nzuri especial ukiwa unanunuwa mikoa iliyo karibu na mipaka example tanga,arusha na mikoa mengine halafu uje kuuza kwenye miji mikubwa kibiashara kama dar utapata faida nzuri sana,

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wakuu kwa muda sasa limekuwa lina nijia wazo la kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kucheza na rates za maduka ya kubadilishia fedha na mabank

Sina maana ya kuanzisha Bureau De change HAPANA, hapa nawaza inawezekana kama nina mtaji wangu kuwa nacheck na rate za maduka yote ya kubadilishia fedha na mabank kwa siku na kisha kwenda kununua kwenye rate ndogo na kwenda kuuza kwa rate nzuri?.................

Najua humu kuna wataalamu wa kila fani naweza kupata ideas kama inawezekana na inafanyikaje au ni kitu haiwezekani
Msinishangae jamani najaribu kufikiri namna ya kujijasiliamari maana hizi ajira sasa tumekuwa watumwa tunafaidisha waajiri tu

Karibuni kwa mjadala

Unatakua unatega pale empress cinema ya zamani?
 
kama hizo fedha za kigeni utakua unazitoa mtaani do it.. ila kama unawaza kuzitoa kwenye insitution moja kwenda nyingine itakula kwako ndugu.
 
Unaongelea forex business?

Biashara nzuri sana. Ila inatakiwa uwe na Euros au Dollars nyingi benki.
Kizuri zaidi, badala ya kununua dollars kwa kutumia madafu na kuziuza bei inapopanda, ni vizuri kununua dhahabu na kuweza kuzibadilisha kwa sarafu itayopanda ... eg sometimes Yen hupanda against Euro, au dollars hupanda against Yen bila kuathiri sana exchange btn euro na dollar.
Basically, precious metals kwa sasa hivi zipo more stable than paper money ... u can use'em to make a lot of dough depending on tax policies za bongo na restrictions kuhusu hizo metals.
 
wewe kama individual kununua foreign currency benki au kwenye duka (bureau de change) unahitaji kuwa na supporting documents kama invoice au passport na visa kwa ajili ya safari. Sasa wewe kwa biashara huwezi kuwa na vitu hivi kwahiyo benki kukuuzia kama individual kuna changamoto kidogo.unless kama unataka kufanya kama illegal business uwe mjanja mjanja.

poa poa
 
Wakuu nimewasoma kwa uzuri kabisa, na baada ya maoni yenu kuyafanyia kazi nimejua kitu kuhusu hii kitu

Kwanza ni ngumu sana kuuza na kununua kwenye Mabank au Bureau de change za hapa Bongo maana zote zinatoa source ya rate sehemu moja BOT
Mfano hizi ni rate za leo kwenye mabank

BUY : SELL
CRDB 1535 : 1625
NBC 1550 : 1615
EXIM 1570 : 1605
T.I.B 1560 : 1595

Sasa ili upate faida ni lazima Bank/Bureau moja iwe kwenye BUY ni kukubwa kuliko kwenye SELL ya Bank/Bureau nyingine.
Maana SELL ni wao wanakuuzia na BUY ni wao wananunua toka kwako,
Kwa mfano huo maana yake wanauza kwa bei nafuu ni TIB, 1595, sasa unatakiwa upate Bank/Bureau itakayo kuwa ina nunua zaidi ya bei hiyo. kama unavyoona rate ni hakuna ya mwisho ni EXIM 1570.
Mfano ikitokea kuna Bank/Bureau ina BUY labda 1600 basi hapo unaweza kupiga bao

Pili vikwazo vya upatikanaji wa pesa zenyewe haswa kwenye maBank wanataka uwe na uthibitisho wa nini unakwenda kuzifanya, Bureau angalau wao hawana kiivyo

Tatu ni biashara illegal hata kama utaifanya basi ni kimagumashi

Hata hivyo nimeambiwa hakuna kinachoshindikana Bongo mambo yote ni michongo tu
Unatakiwa kuwa mjanja kwa kujuana na wafanyakazi wa mabank ambao watakupa special rate ikiwa unakuwa na Account kwao
Pia kuwa na network ya black market ambapo utapata kwa rate powa na kwenda kuziuza kwa mabank

Pia waweza kufuatilia kwa ukaribu trend ya dola inavyopanda na kushuka then unaweza kununua kama zinakuwa chini na kuuza zitakapopanda(risk ni kubwa ila ukipiga unapiga kweli)

Njia nyingine niliyopewa juu juu ni kwamba unaweza kucheza sarafu za aina mbali mbali, unaweza kununua euro kisha ukazi peleka kwenye Kenya shilingi then ukazileta kwenye paundi kisha ukazileta kwenye dola, na ukirudi kwenye shilingi unapata kitu bila jasho

Im still working on it, maoni zaidi yanahitajika wadau
 
BUY : SELL
CRDB 1535 : 1625
NBC 1550 : 1615
EXIM 1570 : 1605
T.I.B 1560 : 1595

Sasa ili upate faida ni lazima Bank/Bureau moja iwe kwenye BUY ni kukubwa kuliko kwenye SELL ya Bank/Bureau nyingine.
Maana SELL ni wao wanakuuzia na BUY ni wao wananunua toka kwako,
Kwa mfano huo maana yake wanauza kwa bei nafuu ni TIB, 1595, sasa unatakiwa upate Bank/Bureau itakayo kuwa ina nunua zaidi ya bei hiyo. kama unavyoona rate ni hakuna ya mwisho ni EXIM 1570.
Mfano ikitokea kuna Bank/Bureau ina BUY labda 1600 basi hapo unaweza kupiga bao

Paulss,

Sisi watu wa Finance tunaamini kwamba hamnaga nafasi ya kutengeneza pesa kwa kuuza na kununua kama usemavyo wewe kwakuwa kwenye soko kuna wachezaji wengi na opportunities unazoziona wewe na wengine wataziona. Sasa imagine wote tumeshaona TIB wanauza bei poa si kila mtu atataka apate Dollar kutoka TIB? Na muda gani utachukua TIB kuona kwamba demand imepanda ghafla na wao waongeze bei? mwisho wake wote wanarudi pale pale bei zinakuwa sawa kwenye soko huria.

Michezo kama hii sisi tunaamini kwamba ni zero sum game hamna cha ku gain.Maana unaweza kupata Dollar kutoka TIB unafika Kariakoo kwenye Bureau unakuta bei ishabadilika zamani na wewe una dollar zako mfukoni. Risk ipo kubwa sana.
 
nimependa mchango wenu mzuri sana kwa sisi tusio na uelewa abt masuala ya pesa
 
Paul S.S ulishapata ufumbuzi wa hili swala, hasa swala la kununua na kuzibadilisha badilisha kupeleka katika euro au pound then unazirudisha katika tshs
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom