Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)


Hiyo mashine ambayo ni ya kisasa haitumii rollers inaitwaje? Na bei zake zipoje?
 
Sasa hivi biashara hii siyo kama zamani. Sasa hivi watu wamegeukia dona baada ya kupata elimu kuwa sembe haina faida mwilini na hivyo haifai kwa afya ya binadamu.
 
Wakuu naomba kupata hali ilivyo katika biashara ya kuuza unga wa mahindi.

1. Hasara na faida zake.
2. Changamoto zake
3. Soko
4. Aina ya mahindi mazuri kununua.
5. Upatikanaji wa mashine za kukoboa na kusaga zenye ubora.

Natanguliza ahsante nyingi.
 
1) Hasara ukiwa mvivu wa kupima mahindi umeliwa
2)) Umeme kukatika ovyo
3) Soko lipo huwez limaliza ila lingi ni la kukopesha
4) Mahind ya Dodoma ndo yanatoa unga mwingi, ya Mbeya na Iringa sio mazur, pumba nyingi sana sababu wanatumia mbolea sana
5) Za kuchongesha ndo nzur kama ni biashara ya kusindika na una mtaji anza na ya kukoboa roller tano na kusaga chukua oversize.

Kama utazihitaji zote mbili kwa mkupuo na stand zake bila motor wala stater nicheck inbox. Motor bei yake kwa hp 50 sasa hivi ni 2.2mil na kwa 40 hp kukoboa ni kama 2mil. Ila kuna mti humu anauza used nimesahau jina ila alikuwa anafanya 40hp kwa 1.8mil pia zipo nyingi used madukan za ujeruman ndo za ukweli ila hata za kichina ni nzur tu ukiwa mtunzaji.
Nb. Sio lazima unapokuwa na mashine lazima kusindika unaweza fa
 
Kuna biashara nilikua naifikiria nifanye..ni ya kukobolesha mahindi alafu na kuuza sembe. Kabla ya kujiingiza kichwa kichwa nimeona niombe ushauri maoni na ujuzi KUHUSU
  • Hali ya soko
  • Mtaji
  • Changamoto
  • Experience kwa waliofanya
 
Soko ni nzuri sana ila jiandae kupata vibali vyote husika..TFDA, TBS, Business Licensing Authoriesties etc
 
Iko vizuri kaka,bt ni lazma upitie hatua kama alivyoshauri mchangiaji aliyetangulia ili usipate vikwazo visivyo na ulazima. Si unajua hicho ni chakula kaka?
 
Hapo kwenye sembe ongeza DONA ni muhimu kwa shughuli za wanaume na ikiwezekana familia nzima watumie dona kuepuka magonjwa ya utapiamlo.
 
Soko ni nzuri sana ila jiandae kupata vibali vyote husika..TFDA, TBS, Business Licensing Authoriesties etc
Ndio kwa baadae !! Kwa sasa nilitaka nianze kidogo kwa kusambaza madukani kwanza kabla cjafanya kitu kikubwa Sijui kama hata hicho kitahitaj hizo process zote Mkuu??
 
By experience!

Nenda mikoa ya Iringa au Mbeya, nunua mahindi moja kwa moja kwa wakulima, sogeza mahindi kwenye mashine ya kusaga iliyo karibu ili kupunguza carriage cost!

NB: Hapa uwe umeshaongea na watu wa mashine, ikiwezekana uwe unawaachia pumba ili gharama ya usagishaji iwe chini zaidi (chini ya 5000/= kwa gunia)

Mahindi yakifika kiasi unachotaka, anza kusaga na kupaki(kwa kuanza unaweza kuwa unatumia mashine ya kushonea ya kukodi na mifuko yenye nembo ya mtu mwingine (mtafute)!

Gharama ya mfuko tupu usio na nembo ni around 200-350 bei ya jumla na 400-600 wenye nembo)

Kipimo kiwe kilo 5, 10, 25 na 50 (gharama ya upakiaji kwa makuli ni around 700 kwa kila kilo 50!

Tafuta magari yanayosafirisha mizigo mikubwa, ongea nao wakuunganishie mzigo wako kwa wasafirishaji wengine (madalali are so good in this)!

Mzigo ukifika mkoa wako wa soko waombe wakushushie sehemu ambayo ni rahisi kwako!

Sambaza mzigo kwa wateja wako!
 

Asante Mkuu kwa msaada wako wa kimawazo
 
Biashara nzuri sana hyo mkuu, na muda mzur wa kununua mahindi ni kuanzia mwez wa 5mpaka wa 7..hiki nikipind cha wakulima weng wanavuna shamban na bei inakua cheap kidogo kwa mbeya lakn sijuh mikoa mingine japokuwa inaonekana kwa huu utawala wa baba jesca anataka kuweka usawa kwa mkulima siyo kama utawala uliopita. Mkulima alikua ananyonywa sana. Point yangu ni kwamba kipind hiki cha mavuno mahind yapo juu sana. Kilo 1 sh 450, wakat huko nyuma kipind cha mavuno kama hiki kilo 1 inakuaga sh 150.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…