Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Habari mwamaJF; dolevaby. Naomba kama ulifanikiwa kupata maelezo ya kutosha ya hao jamaa (hasahasa mawasiliano) unijuze niwatafute. Tafadhali sana.

Mawasiliano nimeweka hapo post ya Nyuma chek nao km uko DAR nenda pale MLIMANI CITY Ofis yao inaitwa CP 0717 000 772 na 0718 467 878 Kila la heri MKUU
 
Yaah...wanasema huu UNGA watu waliudharau sababu ulikuja kipindi cha Njaa lkn kwa maelezo niliyopewa wanasema unavirutubisho vya kutosha kuliko mahindi Meupe...

Ya una virutubisho balaa, huwezi linganisha na haya mahindi meupe
 
Mawasiliano nimeweka hapo post ya Nyuma chek nao km uko DAR nenda pale MLIMANI CITY Ofis yao inaitwa CP 0717 000 772 na 0718 467 878 Kila la heri MKUU

Kaka nimewapigia ila naona wako busy sana nitajarib tena kuna mtu ashajarib?
 
Rice packaging nayo inawezekana haina tofauti na sembe hata kidogo cha muhimu ni kupata mpunga mzuri na kuukoboa vizuri ili usiwe na chenga nyingi (machine factor) kama ujuavyo bei ya mchele ni maelewano na hupangwa kutokana na kunukia, aina na muonekano wake baada ya kukoboa.

Mchele utapata faida zaidi iwapo utaweka machine ya kukoboa mahali ambapo ni karibu na mpunga unapolimwa c'se kusafirisha mpunga kutoka mbeya/ifakara/shinyanga to dar kuja kuukoboa ni hasara.. c'se unapokoboa gunia moja la mpunga unapata mchele kidogo sana, pumba huwa ni nyingi kuliko mchele na pumba za mpunga si chakula pendwa kwa wanyama sana utaishia kuutupa au kuugawa kwa wafugaji wa kuku (pumba zake ni malazi ya kuu)
Hii kitu nilikuwa naiwaza ila bado sijafanyia maamuzi ya kufanya packing,japo nimenunua mpunga gunia 100 hivi za debe 9@1.Je unafaham biashara hii vema.
 
Hellow wa jf na wazo la kuanzisha biashara ya kusaga unga wa sembe na ku pack kwa ajil ya kuuza, jaman naomben mawazo yenu .
Hujambo,kuna mrejesho wowote ambao unaweza kutueleza, mafanikio,changamoto ulizokutana nazo na unazoendelea kupambana nazo.
 
Kuna mashine za kuchongesha SIDO na nyingine unaweza kununua mojamoja dukan japo vinu huwa vinakuwa vidogo kwa hizi za dukan. Nadhan za kuchongesha ni nzuri zaid coz ni ngumu, bei nafuu na pia unaweza kumwambia mchongeshaji akutafutie zile mota za zamani ambazo zinauwezo mkubwa. Mashine (kusaga & kukoboa) mpya kwa Arusha dukani ni Tshs 4.7mil na SIDO unapata mpaka kwa 4.6 mil.

Kwa wachongeshaji wa mitaani zinapatikana kwa mil3. Mtafute huyu jamaa anachongesha mashine nzuri na anakufanyia installation mwenyewe bure kama utanunua kwake. Anaitwa Tall anapatika Ngarenaro kwa wale wa Arusha. 0754315171.

Wanachokifanya hawa jamaa ni unatafuta mashine mwenyew unayoippenda then unawaonyesha wanalipa hela na wanakufanyia installation kazi inabaki kwako kuwarejeshea hela. Wenye hii kampuni ni wazungu kwa maelezo zaid unaweza kumpgia huyu jamaa wa kizungu.
 
Pia nawashauri hizo business zenu mzirasimishe ili ziwe na mashiko zaidi kwa wadau mbalimbali, na pia msiache kuziandalia Ducuments zenye mashiko ya uanzishwaji, uendelezaji na ufanikishwaji wake. Wakati wengine mnawaza biashara SISI tupo tunawaza pia namna ya KUFANYA nanyi ili mfanikiwa, nazo pia ni biashara, kwani PRODUCTION ni kwa GOODS na SERVICES.

VISIT: KIMI DEVELOPMENT CONSULT LIMITED
 
jamani mimi mwenyewe nipo kwenye mchakato huo huko mkoani njombe nina mashine yangu lakini naomba msaada wa kujua jinsi ya kupata logo yangu na jinsi ya kupata viroba na vibari vya kufanya biashara hiyo
 
Mifuko unayohitaji ni ya aina ya magunia yaani visafeti au mifuko ya plastic tu?

Kama ni plastic tu nitakuafanyia uchapishaji wa nembo yako kwenye hiyo mifuko wasiilana nami kwa pm mkuu
asante mkuu nipo na dar na nimetafuta location maeneo ya kimara kwa ajil ya kufunga mashine but sijapata kampun ya uhakika ya kunitengenezea mifuko kwa ajil ya ku pack.
 
Waonaje hizo debe 100 za mpunga ukazisaga kisha tuungane kufanya hiyo biashara?
hii kitu nilikuwa naiwaza ila bado sijafanyia maamuzi ya kufanya packing,japo nimenunua mpunga gunia 100 hivi za debe 9@1.je unafaham biashara hii vema
 
watafute Hill Packaging .... huyu jamaa mmiliki anaitwa Hillary ni mjasiriamali mzuri sana .... anakiwanda cha kutengeneza viroba kipo mapinga Bagamoyo mwanzo kabisa karibu na bunju

Naomba contact zake please
 
Mkuu naamini ushauri wa wadau utakusaidia, upo mkoa ganinikuandalie mahindi mazuri kwa bei nzuri!
 
Wadau. Nimeisha anza mchakato wa hiyo kitu kwa maana ya jengo ambayo mi nimeiita phase one sasa ndo najipanga kuezeka.

Phase two ni kununua machines ambazo ni full set kusaga na kukoboa pamoja na mizani mikubwa na midogo na packaging materials bila kusahau mahindi ambayo mdo mtaji.

Phase three ni kuanza kazi.

Naomba muongozo au ushauri kwa ambaye either anafanya au anauzoefu na hii biashara japo kwa reaserch ndogo niliyofanya inalipa na nimeamua kuanza at a medium level scale walau nipate market share kias fulan lakin naona changamoto ni nyingi mf kupata mahindi fake, unga au mahindi kuharibika ama kuoza, n.k nk.

Hizo picha ndo mjengo wa kiwanda na bahati nzuri nina eneo kubwa hapa kwangu so nimeona bora nijenge hapa kupunguza gharama na iwe rahisi kusimamia.

Ntashukuru kwa ushauri[/QUOT
Mkuu tunaomba mrejesho tafadhali
 
Mkuu hebu fafanua hapa packeging material(mifuko isiyo na nembo) mashine za kupachikia nembo, na mashine za kushonea, mashine za kubania kwa mifuko ya nilon unazijua bei zake? msaada tafadhali
 
Back
Top Bottom