Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Mkuu umefikiria jambo la maana sana kuuza unga wa dona ukizingatia maisha ya Mtanzania yanazidi kuwa magumu kila siku nadhani dona itapata wateja wengi sana kuliko sembe c'se dona bei yake ni rahisi ukilinganisha na sembe, na ukila ugali wake tumbo litajaa muda mrefu .. hii itakuwa mkombozi wa walala hoi na wale wenye kufanya shughuli ngumu.

Kulingana na trend ya soko unaweza kusaga nafaka zingine kama mtama, ulezi etc then ukafanya packaging kama sembe na kuingia sokoni. Nilijaribu kununua ulezi na mtama dar aisee ni uhuni mtupu even though packaging ilikuwa nzuri sana (label ilikuwa "Mama Nora") wamechanganya na sembe. Nipo kwenye mchakato wa kufanya hii biashara miaka 2-3 ijayo
 
Mkuu umefikiria jambo la maana sana kuuza unga wa dona ukizingatia maisha ya mtanzania yanazidi kuwa magumu kila siku nadhani dona itapata wateja wengi sana kuliko sembe c'se dona bei yake ni rahisi ukilinganisha na sembe, na ukila ugali wake tumbo litajaa muda mrefu .. hii itakuwa mkombozi wa walala hoi na wale wenye kufanya shughuli ngumu.

Kulingana na trend ya soko unaweza kusaga nafaka zingine kama mtama, ulezi etc then ukafanya packaging kama sembe na kuingia sokoni. Nilijaribu kununua ulezi na mtama dar aisee ni uhuni mtupu even though packaging ilikuwa nzuri sana (label ilikuwa "Mama Nora") wamechanganya na sembe. Nipo kwenye mchakato wa kufanya hii biashara miaka 2-3 ijayo

Mkuu dona si chakula cha walala hoi kama ambavyo unakielewa na si wewe tu wapo wengi wanadharau hii kitu, ki ukweli dona ndo lenyewe kiafya maana unakula na kile kiini cha njano ambacho kwenye sembe hakipo na hicho ndo chakula cha mwili mengine haya ni makapi tu. Naona una uelewa na biashara hii vipi kuhusu rice milling, kukoboa na kupack pia una ushauri gani?
 
Mkuu kumbuka hii biashara ina base na afya za watu, so unatakiwa ujiandae kikwelikweli, okay.
 
Mkuu dona si chakula cha walala hoi kama ambavyo unakielewa na si wewe tu wapo wengi wanadharau hii kitu, ki ukweli dona ndo lenyewe kiafya maana unakula na kile kiini cha njano ambacho kwenye sembe hakipo na hicho ndo chakula cha mwili mengine haya ni makapi tu. Naona una uelewa na biashara hii vipi kuhusu rice milling, kukoboa na kupack pia una ushauri gani?

Mkuu dona kiafya nalifahamu vizuri sana sema nililiweka kiufupi mno ktk sentence "hii itakuwa mkombozi wa walala hoi na wale wenye kufanya shughuli ngumu." hapo niligusia swala la uchumi na afya.

Rice packaging nayo inawezekana haina tofauti na sembe hata kidogo cha muhimu ni kupata mpunga mzuri na kuukoboa vizuri ili usiwe na chenga nyingi (machine factor) kama ujuavyo bei ya mchele ni maelewano na hupangwa kutokana na kunukia, aina na muonekano wake baada ya kukoboa.

Mchele utapata faida zaidi iwapo utaweka machine ya kukoboa mahali ambapo ni karibu na mpunga unapolimwa c'se kusafirisha mpunga kutoka mbeya/ifakara/shinyanga to dar kuja kuukoboa ni hasara.. c'se unapokoboa gunia moja la mpunga unapata mchele kidogo sana, pumba huwa ni nyingi kuliko mchele na pumba za mpunga si chakula pendwa kwa wanyama sana utaishia kuutupa au kuugawa kwa wafugaji wa kuku (pumba zake ni malazi ya kuu)
 
Habari zenu ndugu.

Kuna uwezekano wa kupata contacts zozote za Bw. Hillary Shoo or contact za kiwandani?

Thanx in advance!!
 
Hii biashara nimewahi kufanya, tatizo niliibiwa nashine zote na wiring pia. Ukweli inalipa hasa ukiwa na soko la uhakika. Zingatia ulinzi wa mali, poa jua ina ushindani mwingi na wateja wengi wa jumla hupenda kupewa kwa credit, sio mbaya ukiwa na wateja waaminifu; kingine cha kuzingatia ni kuwa inaathiriwa sana na msimu, hasa upatikanaji wa mahindi, mahindi mazuri ni ya dodoma hutoa uwiano mzuri sana kwa tani. Kama una mtaji mkubwa kaka nakushauri kila ikifika msimu wa mahindi kushuka bei ununue kwa wingi uhifadhi utafaidika sana. Kumbuka kupanda na kushuka kwa bei ya mahindi na umeme kunaisumbua saaana biashara.
Hongera na nakutakia mafanikio
 
Asanteni kwa hili darasa, kweli nimepata faida kubwa ya nini nifanye kwenye miaka miwili ijayo endapo Mungu atatoa kibali cha mimi kuwa hai.

Natumaini hii project nitaifanyia bagamoyo eneo la mkata.
 
Darasa zuri japo limekaaa kimya muda. Kwa yeyote ajuaye bei za mashine za kusaga na kukoboa.
 
Naona umeamua kuunder estimate ur sales. kg 150? Labda useme kilo 1500.
 
Asante mkuu nipo na dar na nimetafuta location maeneo ya kimara kwa ajil ya kufunga mashine but sijapata kampun ya uhakika ya kunitengenezea mifuko kwa ajil ya ku pack.
Kuna kampuni ya ipo Mbagala kazi yao ni kutengeneza mifuko ya kila aina naweza kuelekeza 0685 31 2326.
 
Wakuu muhimu kujua na bei za mashine za kusaga na kukoboa ili na wengine wenye nia ya kuwekeza kwenye hii biashara kama hii wajipange.
 
I think ni biashara nzuri sana. Mwenye kujua mashine bora na nzuri za kukoboa na kusaga atujuze tafadhali.
 
Wadau naomba anayejua anisaidie bei ya mashine nzuri ya kusaga mahindi na nafaka nyingine ya kukoboa mahindi na ya kufunga mifuko hasa viroba. Zote ziwe zinatumia umeme.

Natanguliza shukrani
 
Wadau naomba anayejua anisaidie bei ya mashine zuri ya kusaga mahindi na nafaka nyingine.ya kukoboa mahindi na ya kufunga mifuko hasa viroba. zote ziwe zinatumia umeme.Natanguliza shukrani

Bei ya kutengeneza kinu cha kusagia mahindi cha panga 8 ni 1.5ml bila mortar (sina uhakika na spelling za mota kwa kizungu) kinu cha kukoboa ni 1.3 mpaka 1.4 bila mortar. Mortar ya 40HP ni 1.3mil that means utahitaji mbili kwa mashine zote i mean kusaga na kukoboa. Bag sealer (mashine ya kuishonea viroba) hizi ni cheap we andaa kama 250000 mpaka 300000 kwa mashine moja ila za india ni nzuri zaidi. If you need more info we ni pm mkuu nipo huko kwa muda sasa.
 
Mashine zipo kwa size,nashauri kwa kusaga sembe kinu cha kusaga utumie size 100,na chakukoboa tumia roller 3 au roller 4,Vinu imara kwa hapa bongo ni vya kuchonga kwenye viwanda vidogovidogo vya bongo ndio vizuri, coz madukani vingi ni vya kihindi mabati yake ni laini mno hua havidumu, lakini pia sijawahi ona kinu cha roller 3 cha India.Mashine zote hizi zinahitaji motor ya hzp 40 ambazo moja ina range 1.3-1.5 Tsh inategemea jinsi utavyoipata,Mimi niko huko kitambo na wiki iliopita nilitengeneza chakusaga size 100 kwa 1.4 na chakukoboa kwa 1.2,vinu hivi vinauwezo wakusaga 1tone/hrs.
 
Mie nahitaji yakukoboa na kusaga je? Naweza tumia mtori moja kwa kusaga na kukoboa?
 
Mie nahitaji yakukoboa na kusaga je?naweza tumia mtor moja kwa kusaga na kukoboa?

Hapo utatengeneza usumbufu wakubadilisha mikanda kila muda,mota moja haitumiki kuzungusha mashine mbili kwa wakati mmoja. Maana yake wakati wakusaga mikanda itakua kwenye mashine yakusaga na ukihitaji kukoboa utoe mikanda uhamishie kwenye mashine yakukoboa, tafuta mota mbili kila mashine na mota yake.
 
Back
Top Bottom